Mahakama yaingilia Bunge kuzuia suala la Escrow lisijadiliwe!

Mtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama?

waliliamuaje mkuu? hawajakuta ufisadi ndani yake? hebu tupe mhutasari wa kilichoamuliwa.
 
Miongozo iliyoombwa na Kafulila na wabunge wengine kuhusu mbinu zilizopo kutumia Mahakama kutaka kuzuia hoja ya Escrow isijadiliwe bungeni, Naibu Spika Ndugai katumia hekima haswa kwa kutoa nafasi kwa baadhi ya wabunge kukishauri kiti.
Hapo ndipo Bunge lilipozizima kwa hoja kali, wakipinga Mahakama kuingilia Bunge. Nimependa michango ya wote waliochangia kwa kweli.
My take: wale waliobeza taarifa hizi zilipoletwa humu JF, sasa limetua Bungeni, naomba michango yenu.
Cc; Lumumba Buku 7Fc.

cc FaizaFoxy MSALANI Ritz MwanaDiwani Mamndenyi, na wachumia tumbo wote wa lumumba
 
Last edited by a moderator:
Mahakama haizuii bunge bali kujadili suala lililopo mahakamani ni kuingilia uhuru wa mahakama, na kuathiri utoaji wa haki katika suala hilo.

suala lipi lililo mahakamani? je, hayo mashtaka yanahusu ukwapuaji wa fedha za escrow? ni kina nani wanashtakiwa katika ufisadi huo? acheni kupayuka jambo usilolijua ndugu yangu.
 
kama JAMBO hili litapita bila kujadadiliwa kisa MAHAKAMA,na UTAWALA ukabaki kama ulivyo,basi nchi hii haina aja ya kuwa na wapinzani,haiwasaidii watanzania,watakua wanakula ruzuku za bure tu
 
Dada SIMIYU kuna mihimili mitatu kwenye nchi yetu ambayo haiingiliani.Hivyo bsai ujue mahakama imekiuka sheria ya nchi,imeziba haki ya msingi ya BUNGE.Kumbuka BUNGE siyo serikali na liko kwa ajili ya kuisimamia serikali na siyo serikali kuisimamia BUNGE.

Na hii itaonodka tu pale mtakapokubali MAWAZIRI wote wasiwe wabunge ili BUNGE lirudi kwenye hadhi yake.Simiyu watanzania tunahitaji kujua ukweli na uwongo wa hawa waliozoa pesa wakishirikiana na SIngasinga.Tetea TAIFA lako,na kumbuka TAIFA kwanza vyama vyetu baadaye.Hakuna chama kitakachoishi milele lakini TAIFA litadumu milele na milele.Pole kama tunakukwaza kwa hili.Yawezekana dada umepatepo huko.Hongera sana,ila kula lakini tetea taifa lako siku zote za maisha yako,ili watoto na wajukuu zako wakufurahie na kukukumbuka milele.

mkumbushe dada Simiyu Yetu kwamba mpaka sasa hv hospitali hazina madawa na kadri hii skandali inavyozidi kuchelewa ndipo tunakosa fedha za kununulia dawa. tunaumia wote bila kujali vyama vyetu.
 
Last edited by a moderator:
Kuna uwezekano mkubwa Pinda siyo mhusika kwenye hii ishu ila kuna watu anataka kuwaokoa maana anapigana kufa kupona

na inawezekana ni watu wa kundi lake la urais ambao anaona wakichafuka naye atachafuka pia. lakini hapa toto la mkulima limegota na kwa msimamo huu wa kutetea WEZI urais atausikia redioni tu.
 
kama mahakama haitaki swala hili lijadiliwe bungeni inataka likajadiliwe wapi,wapi wananchi wa nchi hii wataupata ukweli wa jambo hili?
 
Mtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama?

Mkuu. Hawajadili maamuzi ya mahakama bali wanataka kujadili ripoti ya CAG ambayo kwa taratibu na kanuni za bunge walielekezwa na bunge kuchunguza ufisadi huo na kisha ripot hyo kupelekwa kwa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali na mashirika ya umma PAC!
 
mkuu wa nchi anahusika moja kwa moja kwenye huu wizi, pamoja na ile downns . Mungu ibariki tanzania , Eeee Mungu uwanyakue mapema iwezekanavyo hawa wezi kabla nchi haija ingia kwenye matatizo.
 
Mimi sio mwana sheria,hivyo wana sheria nisaidieni.Msingi wa jaji mkuu kuzuia bunge lisijadili akaunti ya escrow ni nini?Kuna kesi ipo mahakamani?Maana msingi mkuu wa tuhuma ya uchotaji wa fedha za escrow ni hukumu ambayo mahakama kuu ilitoma,na wajanja,wakatumia nakala ile kuiba .Baada ya wizi ule tumaona majina ya majaji kupata mgao,na mpaka sasa hakuna aliyekamusha,wala hatujaambiwa kama kuna kesi ipo mahamani.Ndio maana naomba msaada,wa kisheria na kikanuni kama mahakama inaweza kuupangia mhimili wingine kazi ya kufanya
Pili mimi naoma kuna tatizo kubwa kubwa benki kuu,maana wizi wote mkubwa wa nchi hii unafanikishwa na benki katika mazingira tata na mbaya inakuwa karibu na uchaguzi mkuu.
 
chegreyson, msingi yawezekana ni huu hapa;

0L7C0548.jpg

mkumbushe dada Simiyu Yetu kwamba mpaka sasa hv hospitali hazina madawa na kadri hii skandali inavyozidi kuchelewa ndipo tunakosa fedha za kununulia dawa. tunaumia wote bila kujali vyama vyetu.

Kaka ataelewa tu,maana tulipofika wenyewe CCM wamesema taasisi zinazoaminika ni mbili tu,hizi nyingine WATANZANIA hatuna IMANI nazo,ataelewa tu,si unajua MVINYO ukinywa mwingi lazima ulewe.
 
Hivi Bunge si ni mhimili huru wa serikali?Sasa Mizengo anapozengua kumbe bunge lisiingilie mahakama,kwani mahakama inaruhusiwa kuingilia bungq?!!!!
WIZI MTUPU.
 
mkumbushe dada Simiyu Yetu kwamba mpaka sasa hv hospitali hazina madawa na kadri hii skandali inavyozidi kuchelewa ndipo tunakosa fedha za kununulia dawa. tunaumia wote bila kujali vyama vyetu.

tpaul

Hebu tumia akili kidogo. Kwani hizi hela zilitengwa kwa ajili ya kununulia dawa???
 
Last edited by a moderator:
Ni nani anaamua kuwa uamuzi huo ni haramu? Hapo ndiyo penye tatizo.

Uma mkuu unauwezo na haki ya kukataa uamuzi wowote wa ki-pu-mba-vu unaotolewa Mahakamani na kuendelea kutekeleza kile wanacho kiamini.Kiujumla msingi wa tafsiri ya sheria ni lazima uondoe absurdity katika maamuzi yake .

Kama tafsiri yeyote ya Mahakama itakuwa na absurdity ndani yake kuna alternatrive mbili kwanza kwenda Mahakama ya Juu au pili wananchi kukataa kufuata hicho kilicho amriwa .Hawana Magereza ya kufunga wananchi wote.
 
unajua hawa maCCM ni MABWEGE sana. hili suala ni very urgent lakini wanataka kulifukia huku wakijua fika kwamba WAHISANI wanataka majawabu haraka watoe hela. sijui wanataka tuendelee kufa kwa njaa na maradhi mpaka lini. hospitalini hakuna dawa huku wao wakiumwa tezi dume tu wanakimbilia marekani!

hiviii inawezekanaje sisi watanganyika miaka yoooote tuwe tunaishi kwa kutegemea HISANI ya wakubwa???
hili jambo nadhani 2015 tulifanyie kazi nadhani TWAWEZA sisi wananchi kufanya maamuzi magumu na mazito ili tutoke kwenye hii kasumba ya OMBAOMBA TEGEMEZI.
Namshukuru sana Kwa mara ya kwanza mh. NAIBU SPIKA BW. NDUGAI kukubali na yeye kujiwekea KUMUBUKUMBU itakayo mfanya akumbukwe na vizazi vijavyo kwa kukubali kulishughulikia suala la WIZI WA FEDHA ZA WANANCHI kupitia ESCROW ACOUNT.
humu JF kuna wapambe wa LUMUMBA ST waliotengeneza tena kwa kujidai kuwa MH KAFULILA ataumbuka sasa na tuone aliesema TUMBILI na wabunge nani ZAIDI nani atamwagwa. MACHO YETU LEO NI MJENGONI TU MPAKA KIELEWEKE.
 
Back
Top Bottom