Mahakama yaingilia Bunge kuzuia suala la Escrow lisijadiliwe!

Nadata sana kwasababu hili suala liliibuliwa bungeni na likaamua kupitia kamati kuwa suala hili lifanyiwe kazi na CAG pamoja naTAKUKURU baada ya taasisi hizo kumaliza kazi wakaleta taarifa zao ndani ya bunge na taarifa hizo zinakatazwa zisijadiliwe sasa sintofahamu yangu ni kwamba lini taasisi hizo za TAKUKURU na CAG walipeleka watuhumiwa mahakamani na ni wakina nani?? na imefunguliwa lini????
 
This is too much... Najaribu kuitafakari ya kauli ya Pinda.. Kama amesema iachiwe mihimili mitatu ifanye kazi bila ya kuongiliana... Basi hivyo angeiambia mahakama kwa kaliacha bunge liendelee na kazi zake... #WanalindanaKiaina
 
Mtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama?
acha ujuhaa mahaka haina uwezo wa kuizuia bunge....bunge iko juu! ni hapa tu ndyo wanafanya upuuzi huo......
mahakama kuingilia bunge .........ni sawa na kuaema bunge limevuliwa chupi
 
Somalia ni nchi ambayo mifumo yote ya utawala imesambaratika, tofauti na ilivyo kwa Tanzania. Cha ajabu mambo yanayotokea Tanzania hayana tofauti na nchi ambayo haina serikali. Maliasili hazitusaidii, mfano kwenye migodi ya madini kuna viwanja vya ndege, ndege zinatua usiku na kuruka usiku. Mbuga za wanyama halikadhalika mambo ni hayo hayo.

Wizi/ufujaji wa mali za uma umekithiri, leo hii tunasikia ya ESCROW lakini kumbukeni kuna zile 300bn za uswisi sijui iliishia wapi, wizi kwenye rada, misamaha ya kodi nk, Nchi yetu inahuzunisha, ila ipo siku atapatikana mtu wa kuikomboa hii nchi, hata kama sio leo lakini ipo siku. Mungu ibariki Tanzania
 
Hivi ni nini kimetuloga siye Wadanganyika, EPA, Twiga, Richmond na sasa EScrow na bado hatujua picha lijalo.... Cha kustaajabu kundi lile lile la wezi linapewa/linajipa madaraka ya kuendelea kutudanganya.... Kuna wakati natamani kwenda front ila sina Imani na Wadanganyika wenzangu hasa nikikumbuka ya Ulimboka na wengine waliolazwa milele. Kuna day tutapata uhuru wetu kamili nikiwa hai au mfu nitaomba muda wa kusheherekea.
 
Mtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama?

Majibu yako yalinifanya nipuuze sana hoja zako na kukaa mbali na jukwaa hili ila after all this long time bado hujatembea? Utakuwa kilema wewe siyo mzima.
 
Unadhani alipokwenda kuandika katiba ya CCM alikuwa mjinga! Alijua wazi sheria zikifuatwa atakuwa hana pa kujificha.

Kaondoa suala la maadili katika katiba. Halafu huyu ndiye anapewa dhamana kubwa kama hiyo.
Kama Taifa tumekwama kabisa, kama hospitali hazina dawa halafu wakuu bado wanapiga danadana ni hatari.
 
chegreyson, msingi yawezekana ni huu hapa;

0L7C0548.jpg

"ni bora kuzuia maana wakiliongelea inaweza kuwa balaa zaidi".
Na baada ya kutoleta maelekezo kwa walio chini yake ndio wakagundua kuwa; inabdi walau Mtanzania mmoja afungue kesi kuzuia badala ya mahakama kuandika moja kwa moja. Na baada ya kusikilizia upepo wakaamua kukana uwepo wa baru hiyo!!
Hivi huyu naye alitumia gharama za walipa kodi kwenda kupanga hayo!?

 
Uma mkuu unauwezo na haki ya kukataa uamuzi wowote wa ki-pu-mba-vu unaotolewa Mahakamani na kuendelea kutekeleza kile wanacho kiamini.Kiujumla msingi wa tafsiri ya sheria ni lazima uondoe absurdity katika maamuzi yake .

Kama tafsiri yeyote ya Mahakama itakuwa na absurdity ndani yake kuna alternatrive mbili kwanza kwenda Mahakama ya Juu au pili wananchi kukataa kufuata hicho kilicho amriwa .Hawana Magereza ya kufunga wananchi wote.
Changamoto ni kuwafanya wananchi waungane kuukataa uamuzi huo wa Mahakama.
 
Yaani wewe umefungua akaunti ili kuwatetea hapo na kuleta uchonganishi wa mengi na wengine. Acha upuuzi huu
 
hio barua iko wapi? Watu wanaropokwa tu Lissu alitaka kutoka povu aonekane yeye Mungu wa sheria.
Mbona barua tele hapa Jf zinaletwa kama attachments mbona hii hatuion?
 
Kinacho nitatanisha si mahakama kuingilia bunge ila ni jinsi mahakama inavyoweza kutoa uamzi. Kwa uelewa wangu finyu hata kama kesi ipo mahakamani, nilitarajia mahakama haiwezi kutoa uamuzi bila ya kuwepo na mshitaki na mshitakiwa. Kwa maneno mengine ni kusema mhimili mmoja wa serikali 'executive' umepeleka maombi mahakamani kutaka escrow isijadiliwe na hivyo mahakama ikatoa maamzi...labda wabunge kama kweli mwaipenda nchi yetu tungeni sheria inayoizuia 'executive' kuwazuia ninyi 'legislators' kufanya kazi yenu. Mawazo yangu, kama ni mwanasheria mkuu amepeleka pingamizi hilo mahakamani, maana yake kapata baraka za 'executive' maana ni mmoja wao...kwa hiyo tusitafute hela zilikoenda ila tusema waliozichukua wanajaribu kuzuia wengine wasijue kilichotokea...halafu ukishayatafakari...fanya uamzi kuanzia sasa na kesho na siku zijazo. ....
 
tpaul

Hebu tumia akili kidogo. Kwani hizi hela zilitengwa kwa ajili ya kununulia dawa???

Kwani hela za dawa zinatoka m@k@li0n! mwa mamayo? Wafadhili wameahidi kutoa Tsh bilioni 1 baada ya skendo hii ya Escrow kupata ufumbuzi. Ucheleweshwaji au uchakachuaji wowote wa wa hitimisho la skandali hii, maana yake ni kwamba nchi itachelewa kupata fedha hizo au itazikosa kabisa. Na kwa kuwa fedha hizi ndizo zinzotumika kugharamia huduma za jamii (kama vile dawa, nk) maana yake ni kwamba watu wataendelea kufa! Umeelewa sasa? Sasa nikuulize: Wewe unadhani watu wanaokufa hospitalini kwa sababu hospitali hazina dawa unadhani fedha za kununulia dawa zitatoka wapi ili kunusuru hali hii?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom