ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Mmiliki wa mtandao wa kubadilishana mafaili kwenye intaneti unaojulikana kama MegaUpload ambao umefungiwa Bwana Kim Dotcom amepata ushindi mkubwa mahakamani. Mahakama ya New Zealand imeamuru Kim Dotcom arudishiwe mali zake zote zilizizotaifishwa mwaka 2012. Mali hizo zilitaifishwa na serikali ya New Zealand kutokana na shutuma dhidi ya mtandao wa Megaupload kuwa unaruhusu watu kubadilishana mafaili yenye haki miliki ikiwa ni pamoja na filamu, muziki na programu za kompyuta, huku Kim akijiingizia mamilioni ya fedha. Kim Dotcom alikana mashitaka hayo, hata hivyo serikali ya New Zeaaland ilikuwa inaendelea kushikilia mali zake zilizotaifishwa.
Miongoni mwa mali zilizotaifishwa ni pamoja na magari 18 ya kifahari ikiwemo gari aina ya Pink Cadillac ya mwaka 1959, na gari zilizo na pleti namba za binafsi zinazosomeka HACKER, MAFIA, EVIL na STONED. Mali nyingine zilizotaifishwa ni nyumba za kifakhari (mansion) pamoja na fedha taslim. Wachambuzi wanakisia utajiri wa Kim Dotcom unapindukia Dola za Kiamrekani Milioni 200. Mbali na mali hizo Kim pia anamiliki boti ya kifakhari (Luxury Yacht) yenye urefu wa futi 240.
Kim Dotcom alibadili jina rasmi na kisheria na kuanza kutumia ubini wa Dotcom mwaka 2005 alipokuwa akiishi Hong Kong, mwaka huo huo alianzisha Megaupload, mtandao huu ilidumu miaka 7. Jina lake la kuzaliwa ni Kim Schmitz. Miongoni mwa majina yake mengine ambayo amewahi kutumia au anajulikana kwa majina hayo ni Kimble na Kim Tim Jim Vestor. Wakati Kim anatambuliwa kama mhalifu, binafsi anajitambua kuwa ni mjasiri amali wa dijitali.
Januari Mwaka 2012 mtandao wa MegaUpload ulifungiwa, siku ya kuazimisha mwaka mmoja tangu kufungiwa kwa mtandao huo Kim Dotcom alianzisha mtandao mwengine unaojulikana kama Mega. Mega ni site inayotoa huduma ya Mawingu (cloud) yenye kinga (privacy) ya hali ya juu ambapo watumiaji wanakwepa wanayoyafanya kujulikana na majasusi wa serikali mbali mbali Duniani.
Mara baada ya ushindi huo Kim Dotcom aliandika kwenye Twitter Mimi na Mona tunarudishiwa mali zetu.. Mona ni mke wake ambapo wana jumla ya watoto watano. Mbali na kesi hii Kim anakabiliwa na kesi mbali mbali ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya serikali ya Marekani, ambapo mwezi Julai mwaka huu mahakama za New Zealand itasikiliza ombi la serikali ya Marekani ya kutaka Kim apelekwe huko ili akashtakiwe, iwapo atatiwa hatiani huko marekani Kim Dotcom anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela. Tayari Kim alishahukumiwa kifungo cha nje mara mbili huko nyuma kwa makosa ya hacking, na kusambaza mafaili yenye haki miliki nchini Ujerumani. [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD][/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Nyumba (Mansion) anayoishi Kim Dotcom[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Chanzo: gajetek habari

