Mahakama ya Kadhi: Wabunge wafanya vurugu wakati wa Semina

Sehemu kubwa ya kazi ya Mahakama ya Kadhi ni katika suala la mirathi. Ifuatayo ni namna Shariah inavyotaka mali ya mfiwa kugawanywa.Islamic Inheritance Calculator

Ukiangalia mlolongo wa warithi, huyo mjane na watoto wake watabaki na nini? Na kama mjane si Muislamu, Sharia haimtambui katika mirathi. Huyu atakimbilia wapi? Ndugu wa marehemu waislamu si wataweza kutumia Mahakama hizi kuwanyima haki ya urithi wajane ambao sio waislamu?

Au suala la umri wa msichana kuolewa. Kumbuka Muislamu wa Mombasa ametufundisha kuwa kwa Muislamu hakuna sheria iliyokuwa juu ya Sharia. Sasa kama Muislamu atadai kuoa binti wa miaka sita na kukutana nae kimwili atakapofikisha umri wa miaka tisa, Serikali itakuwa na haki ya kumzuia?

Amandla.......
 
hapana hiyo imekataliwa jana na rais. Haina tatizo ni uelewa tu.tuombe suala hili lipite salama kuna hatari ya nchi kuingia kwenye machafuko.


binafsi sina shida , tatizo lilikuwa mwanzoni ni nani atazigharimia maana lilileta shida. Shida iliyopo kwa sasa kadhi kutambuliwa ndani ya katiba.
 
Oyayaaaaaaaa........kinanuka sasa hivi.acheni hii mambo wajameni.viongozi wa jukwaa la amani mutahukumiwa siku moja kwa kushindwa kumshauri waziri mkuu.kucheza mpira wa miguu siyo umoja.........nb Simba vs Yanga.. .hakuna umoja.Uuuuuuwuhiiiii mnatuchinja jamani......tamaaa ya madaraka ...tusifike pabaya.
 
ewe mkristo tambua ya kwamba mahakama ya kadhi itawahusu waislam na kuhusu gharama za uendeshaji ni zao wenyewe kama serikali ilivyosema. Kwanini mnapenda kuwanyima haki zao waislam. Hivi ni kweli mahakama ya kadhi italigawa taifa kwa lipi hasa hebu tuseme ukweli. Mimi naona endapo mahakama ya kadhi haitopita basi ndio itakuwa sababu ya taifa kuwa na mpasuko kati ya waislam na wengine. Ndg zangu tuache chuki yani unakuta mtu anabisha tu.
 
Pinda ana matatizo yake binafsi naye anataka uraisi kwa kuwalaghai waislamu.ilikuwa hakuna haja ya semina tena kwani jana bwana mkubwa wao alishafunga mjadala.
 
Ndugu,

Unafikiri n kwanini mambo yenu ya dini yawe ktk katiba ya nchi?

Kwani mnashindwa nini kuianzisha bila kutaka ridhaa ya makafiri?

Hapo hakuna kutaka ridhaa ya makafiri hapo tunataka sheria kama inakubaliwa tuanzishe basi itambulike rasmi na si kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Endesheni mambo yenu wenyewe proudly christian

Hivi kuna mambo yanaendeshwa kiholela bila taratibu na nchi kufahamu, hovyohoyo tu jaribu uone defender! Hata ya kwenye familia yako yote yanaongozwa na sheria za nchi. Hata halmashauri za wilaya wanasheria zao ndogondogo ambazo serkali kuu inazitambua. Nasi tunachoomba ni serkali kuitambua na njia nzur ya kuitambua nikuingiza katika sheria ya mahakama ili ikitafsliwa kuwa Mahakama ni ....hatujaomba kuendesha au kuanzishwa na serikali.
 
Ushasema mswada, kwani ule mswada ulitaka upelekwe Kiarabu?

Wanaojiona hawafai kuujadili kwanini wanaujadili? si wasepe tu?

kama hawana chakuchangia kwanini wanachangia? walilazimishwa?

Hapo umenena vizuri. Nakupongeza kwa busara zako. Hata na sisi tulishangaa kuona wanashirikishwa kwa jambo ambalo hawalifahamu.

Tunawapenda na tunawatakia mafanikio mema, mpate mahakama nzuri ya kuweza kuwasaidia.
 
Mahakama ya kadhi ipo na inafanya kazi mwenye kutaka kulithibitisha hilo aende Bakwata makao makuu Kinondoni.Wanachotaka waislam ni kutambulika kikatiba dhidi ya maamuzi na hukumu zinazotolewa juu ya masuala yanayohusu mirathi,ndoa na mali za wakfu .Kwa Mfano leo kesi inaenda kwa kadhi inatolewa hukumu (kwa mujibu ya matakwa ya dini ya kiislam) halafu mahakama ya serikali inatengua.
Waislam wanachodai ni kutambulika si jinsi ya kuindesha au kuwahukumu wasiokuwa waislam.Ni hilo tu wasomi wa kikristo wanashindwa kulielewa.

ngoja na mimi niulize swali. ninani atakayekuwa anamteua kadhi mkuu. na kama ni Rais ikitokea Rais akawa mkristo anaweza kuteua kadhi kwa kiislam I nakubaliana?
 
Lakini hii inafaida gani?

Hivi hiki ndo kipaumbele chenu cha maisha?

Unaonaje nguvu hii ingetumika kudai huduma bora za afya... Elimu bora na miundombinu?
hoja kabambe sana ! huyu kikongwe akirudi tena basi atakuwa ruhani ; si mtu wa kawaida .
 
Back
Top Bottom