Mahakama ya Iraq yasitisha shughuli zake Wananchi wakisisitiza kuvunjwa kwa Bunge

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mahakama nchini Iraq imezisimamisha shughuli zake ikiwa ni baada ya wafuasi wa kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa Moqtada al-Sadr kuongeza shinikizo lake kutika kuvunjwa kwa bunge, ukielezwa kuwa mgogoro mkubwa tangu uvamizi wa Marekani.

Katika siku za hivi karibuni kiongozi huyo amesababisha uwepo wa hali ya wasiwasi kwa kuamuru maelfu ya wafuasi kuvamia na kudhibiti bunge na hivyo kuzuia uundwaji wa serikali ikiwa takribani miezi 10 tangu kufanyika kwa uchaguzi.

Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi, ambaye amekatisha ziara yake nchini Misri ili aweze kushughulikia mgogoro huo, amezitaka pande zote kuwa tulivu na kurejea wito wake wa mazungumzo ya kitaifa.
 
Mrusi kafanya yake tena, dah! Mbona mwaka huu hadi Joe Biden naye atajiuzulu khaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…