Mahakama waiondoa kesi dhidi ya Godbless Lema

Mahakama waiondoa kesi dhidi ya Godbless Lema

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba kesi iliyokuwa inamkabili mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema imefutiliwa mbali na mahakama leo jijini Arusha baada ya Jamhuri kupeleka maombi ya kufuta kesi hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa kwa shinikizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo kwa madai kwamba Lema alichochea vurugu kwenye chuo cha Uhasibu Arusha na pia Lema anadaiwa kumtukana mkuu huyo wa mkoa.

Lema anadaiwa kutamka maneno kwamba..Mkuu wa mkoa anakuja kama anaenda Send-off..Maneno ambayo polisi wanadai yalichochea uvunjifu wa amani.

Mahakama imefutilia mbali kesi hiyo kwa madai kwamba Lema hana kesi ya kujibu.

Kama kawaida umati wa wafuasi wa CHADEMA ulifurika mahakamani na kushangilia kwa nguvu mara baada ya hukumu hiyo.
 
Breaking News!!
Kesi ya Uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mbunge Lema imefutwa!

Kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili Lema Mbunge imefutwa na mahakama Kuu Arusha,kwa mujibu wa makosa ya jinai Mahakama imefutilia mbali mashitaka yaliyofungulia;
Leo waliokuwa wakitakiwa kutoa ushidi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na OCD,;'
images
Z



 
Hii sio habari kwani tangu mwanza watu wote MAKINI na wenye AKILI TIMAMU tulijua kwamba kutamka maneno eti "Mkuu wa mkoa anakuja kama anakwernda kwenye sendoff" ni uchochezi. Mapunguani tu ndiyo yalikuwa yanajiaminisha kwamba maneno hayo ni uchochezi.

Habari tunataka kujua Mulongo atalipa shilingi ngapi kama gharama za kesi na usumbufu kwa Mhe. Mb Godbless Lema. Pesa za mazuzu huliwa kwa mtindo huo.
 
Licha ya mbwembwe nyingi za kwenda kumkamata Lema kama vile gaidi ambapo vilienda gari za polisi zaidi ya kumi saa nane usiku wakiwa na mbwa silaha za kivita na kuruka ukuta ili kuingia kumkamata Lema na kama haitoshi wakatishia kupiga bomu mlangoni kwake kama hatafungua, leo kesi hiyo mwanasheria wa serikali ameomba kesi hiyo ifutwe, huu ni mwendelezo CCM kuwafungulia kesi za kipumbavu viongozi/ wabunge wa chadema wakiamini kuwa ni kuwazoofisha lakini wamekuwa wakibwagwa mahakamani kirahisi sana kutokana na kesi zao kutokuwa na kichwa wala miguu mfano kesi za hivi karibuni niili ya Sugu kumwita waziri mkuu Mizengo kayanza Peter Pinda kuwa ni -------- baada ya kutoa kauli ya kipumbavu bungeni kuwa watakao kataa kutii amri ya polisi wapigwe tu bila kujali polisi hao hao ndiyo wanao tuuzi a bangi mitaa, ndiyo hao hao waoua tembe wetu kwa kushirikiana na kinana, ndiyo hao hao wauuza sembe na kuwalinda watuhumiwa wa sembe, ndiyo hao hao wanao bambikiza watu mafuvu, ndiyo hao wanao teka wakenya na kuwaelekeza maneno ya kuongea kisha kuwaamru wakatubu..

Leo ilikuwa kesi ya kamanda Godbless lema kuwagalagaza ni kwenye kesi ya kumwambia mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo kuwa alienda kwenye msiba wa chuo cha Uhasibu kama anaenda kwenye Send Off....
 
Sipati picha mpaka 2015 hawa magamba watakuwa wamefungua kesi ngapi za uongo dhidi ya Chadema ila naamini haki ya mtu haipotei huenda ikacheleweshwa tu,. Mkuu wa mkoa majukumu yako ya msingi inaelekea yamekushinda sasa unataka kushinda mahakamani na kesi zisizokuwa na vichwa wala miguu!! Mahakama zetu zinatumika vibaya mno,.
 
Kila siku chadema wanashinda hizi kesi ndiyo kusema hawa wanaozifungua hawajuia sheria au ni majuhu?

Maana hata zile kesi alizoagiza katibu mkuu wa ccm kipindi hicho zifunguliwe zidi ya wabunge wa chadena nazo cdm imeshinda karibia 75%, ni lini tutakomesha ujinga huu wakupotezeana mda?
 
Back
Top Bottom