Mahakama waiondoa kesi dhidi ya Godbless Lema

Mahakama waiondoa kesi dhidi ya Godbless Lema

Hii sio habari kwani tangu mwanza watu wote MAKINI na wenye AKILI TIMAMU tulijua kwamba kutamka maneno eti "Mkuu wa mkoa anakuja kama anakwernda kwenye sendoff" ni uchochezi. Mapunguani tu ndiyo yalikuwa yanajiaminisha kwamba maneno hayo ni uchochezi.

Habari tunataka kujua Mulongo atalipa shilingi ngapi kama gharama za kesi na usumbufu kwa Mhe. Mb Godbless Lema. Pesa za mazuzu huliwa kwa mtindo huo.

Ndiyo maana wanafungia magazeti yanayoelimisha na kuwafumbua macho watu wajue utendaji wa serikali yao. Kila uozo unaofunuliwa eti ni uchochezi wa kuwagombanisha watu na serikali!

Ni wakati umefika KATIBA mpya itamke wazi kuwa serikali itawajibika kwa wananchi na si kinyume chake kama ilivyo sasa.
 

Chezea cross examinations za kina Kibatara na Tundu Lissu...Nani yuko tayari kuumbuka?
Heri nusu shari kuliko shari kamili...

Hapana chezea kabisa cross examination ya hao jamaa,kwenze kesi ya ubunge wa lisu kuna shahid alidai amechoka kuulhzwa maswal,mwingne akadai anaenda msalani akasepaa!
 
Kwani hapo awali Mulongo alikuwa anafanya kazi gani kwa wanaomfahamu vizuri? Nina mashaka naye.
 
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba kesi iliyokuwa inamkabili mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema imefutiliwa mbali na mahakama leo jijini Arusha baada ya Jamhuri kupeleka maombi ya kufuta kesi hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa kwa shinikizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo kwa madai kwamba Lema alichochea vurugu kwenye chuo cha Uhasibu Arusha na pia Lema anadaiwa kumtukana mkuu huyo wa mkoa.

Lema anadaiwa kutamka maneno kwamba..Mkuu wa mkoa anakuja kama anaenda Send-off..Maneno ambayo polisi wanadai yalichochea uvunjifu wa amani.

Mahakama imefutilia mbali kesi hiyo kwa madai kwamba Lema hana kesi ya kujibu.

Kama kawaida umati wa wafuasi wa CHADEMA ulifurika mahakamani na kushangilia kwa nguvu mara baada ya hukumu hiyo.

Badilisha heading! Sema MAHAKAMA YAKUBALIANA NA MH, LEMA, Mkuu wa Mkoa alikuwa anatembea kama anakwenda kwenye Send off
 
Back
Top Bottom