Mahakama: Rostam anakamatika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama: Rostam anakamatika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 26, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Mahakama: Rostam anakamatika


  [​IMG]
  Na Ezekiel Kamwaga - Imechapwa 16 February 2011

  [​IMG][​IMG] [​IMG]


  SIRI kuhusu ushiriki wa Rostam Aziz, mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa Igunga, katika ufanikishaji mkataba tata wa Dowans, zinazidi kuanikwa.
  Nyaraka kadhaa za Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), iliyoketi jijini Dar es Salaam, zinaonyesha Rostam ndiye alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa katika “dili” la Dowans Holdings SA na hata Richmond.

  “Itoshe tu, kwa ajili ya kuweka rekodi sawa, kusema kuwa tumebaini kwamba Bw. Aziz alikuwa na ushawishi mkubwa, hata kama hauonekani wazi, kwenye mchakato mzima wa suala hili na hadi kufikia hapa tulipo sasa kwenye mgogoro huu,” inaeleza hukumu ya ICC katika kifungu cha 156, kilichopo ukurasa wa 38.

  Majaji watatu waliosikiliza shauri hilo – Gerald Aksen kutoka Marekani, Swithin Munyantwali kutoka Uganda na Sir Jonathan Parker wa Uingereza – wanasema, “…baada ya kusikiliza kwa makini maelezo ya Henry Surtees, Mtunza Fedha wa kampuni ya Caspian (inayomilikiwa na Rostam Aziz), tumeridhika kwamba Surtees ndiye aliyekwenda Marekani kujadiliana na wamiliki wa Richmond na alitumwa kufanya kazi hiyo na Bw. Rostam Aziz.”

  Akiwa mwajiriwa wa Caspian, Surtees alifunga safari ya kwenda Houston, Texas, nchini Marekani tarehe 7 Oktoba 2006 kuzungumza na wawakilishi wa kampuni ya Richmond na Portek International Limited.
  Lakini katika maelezo yake ya awali kwa mahakama hiyo, Surtees kama Rostam, alificha taarifa sahihi juu ya aliyemtuma. Awali alidai kuwa aliombwa na kampuni ya Al Adawi kwenda Houston kwa ajili ya kuangalia na kuchambua uwezo wa kifedha na kibiashara wa Richmond iliyokuwa imepewa zabuni ya kufua umeme wa dharula nchini.

  Hata hivyo, alipobanwa na wakili wa TANESCO kutoka kampuni ya Reed LLP ya Uingereza, Anthony White, kueleza ni nani hasa kutoka Al Adawi aliyemtuma kwenda Houston, Surtees “alijiumauma” na kutaka kukwepa kujibu swali hilo kabla ya kumtaja Rostam.

  Wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini wanasema kutajwa kwa Rostam katika hukumu ya Dowans kuwa ndiye alifanikisha mkataba huu, kumeondoa moja kwa moja kiwingu kilichotanda juu ya ushiriki wake katika suala hilo.

  Tarehe 3 Mei 2009, Rostam alilitangazia taifa kupitia mkutano wake na waandishi wa habari katika hotel ya Kilimanjaro Kempinski, kutoifahamu Dowans; kutohusika na Richmond na kutojua lolote juu ya wizi wa Sh. 40 bilioni uliofanywa na kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd., ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Mahakama ya ICC ilielezwa kuwa siku moja kabla ya Surtees kwenda Marekani, Mwanasheria wa TANESCO, Subira Wandiba aliandikia Richmond kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya kushindwa kutekeleza mkataba wake.
  Kampuni ya Richmond iliahidi kuleta nchini majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura Novemba mwaka 2006, lakini hadi Oktoba 2006, kampuni hiyo ilikuwa haijaweza kuzalisha hata megawati moja za kuingiza katika Gridi ya Taifa.

  Katika mazingira hayo ya safari hiyo ya Surtees ya tarehe 7 Oktoba, 2006, ICC ilifikia maamuzi ya kuona kuwa Dowans ilinufaika na Rostam kuwa na uwezo wa kupata taarifa za ndani ya serikali na ndiyo maana ilifanya haraka kwenda Marekani mara baada ya barua ya TANESCO.

  “Tunakubaliana na maelezo ya Surtees kuhusu mkutano wa Oktoba mwaka 2006 uliofanyika Houston. Tunaona kwamba mkutano huo wa Houston uliitishwa na Rostam mwenyewe mara baada ya kuwa amefanya mawasiliano ya namna fulani na Gire (Mohamed, anayetajwa kuwa mmiliki wa Richmond). Hata hivyo, si kazi ya ICC kwa sasa kujua nini hasa Rostam na Gire walizungumza,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

  Katika hatua nyingine mahakama imeeleza kuwa Surtees alishindwa kujibu swali kuhusu vipi yeye – mwajiriwa wa Caspian – aliweza kufanya kazi kwa niaba ya Dowans Holding SA (DHSA), wakati hakuna mahali popote panapoonekana kuwapo ubia kati ya Dowans na Caspian.
  Kwa mujibu wa ICC, Surtees alieleza kuwa alichojua ni kwamba anayetajwa kuwa mmiliki wa DHSA, Brigedia Suleiman Al Adawi, ni rafiki na mshirika wa kibiashara wa Rostam na kwamba mwanasiasa huyo alikuwa akimsaidia tu rafiki yake kupata kazi hiyo ya kuuza umeme nchini.

  Hata hivyo, Surtees alipoulizwa tena na White kutaja mahusiano ya kibiashara kati ya Rostam na Al Adawi, alishindwa kueleza, badala yake akaishia kusema, “Mahusiano hayo ya kibiashara nilielezwa na Rostam mwenyewe.”

  Tangu kuibuka kwa sakata la Dowans, Rostam amekuwa akikana kuhusishwa kwake na kampuni hiyo, akisema alichofanya ni kukubali kupewa nguvu ya kisheria (Power of Attoney) na Dowans.
  Kwa nguvu ya kisheria aliyopewa, Rostam ndiye mwenye mamlaka ya kukusanya fedha, kuajiri, kudai na kufungua kesi zinazohusu Dowans, jambo ambalo si la kawaida kwa watu wanaopewa nguvu za kusimamia kampuni.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Watu wote wananiboa tu.. sasa kwendaa kwa Surtee huko Houston Tarehe 7 Oktoba 2006 na kusainiwa kwa mkataba kati ya Dowans na Richmond 14 Oktoba, 2004 hakuna uhusiano wowote? Nashangaa kwanini hii hoja hailetwi mbele kuhojiwa? Inaboa kweli. I'll have to do this mimi mwenyewe.
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Si nackia Dowans wamesamehe deni dogo wanadai deni kubwa tu?
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kama RA hawezi kukamatwa na kushitakiwa kwa uhujumu wa uchumi ni lazima JK aachie ngazi apende asipende.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  hakuna deni linalohitajiwa kusamehewa.
   
 6. T

  Tofty JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kusema ukweli naombea kungekuwa na watu wenye utayari wa kulifuatilia hili suala kwani legally inawezekana kabisa!
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi ndo hapo napotaka kutapika na hili liserikali la JK jamani
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hivi usalama wa taifa wanasubiri nin i si wammalize tu huyu mwarabu RA?
   
 9. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani wananchi ndo tunafuata sheria lakini siyo UWT wala viongozi wetu wa ngazi juu. Kwa hiyo wenye mamlaka ya kuwashitaki hawa wanaovunja sheria za nchi yetu ni sisi wenyewe wananchi. Kazi kubwa ni namna ya kuwashtaki na kudeal nao.
   
 10. s

  sdkifaa Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 14, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wananchi wengi wangependa kuona mtu akitiwa kikaangani juu ya swala la dowans pasipo kuzingatia if rostam goes down many society highlly influencial people (vigogo) will follow!..so kuna nguvu nyingi sn inayotumiwa na watu hao wenye pesa kufichia makucha swahiba wao uyo!..tusitumie nguvu nyingi kuukata Mbuyu kwa kiwembe instead maamuzi magumu kwa serikali yetu yanatakiwa kuchukuliwa haijalishi kama demokrasia itapindishwa!..wakati kama huu namkumbukaga sana mwalimu Nyerere coz hakusita kuwachinjia baharini mafisadi Papa hata kidogo hasa wale wenye kutilia shaka mustakabadhi wa maendeleo ya Taifa na Amani..ikibidi kufilisiwa kwani utajili wao wamejilimbikizia kwa njia za udanganyifu na jasho la watu maskini so kwakuwa filisi kiuchumi nakimadaraka kutapisha uchunguzi kufanyika nakuludisha jasho la wananchi kwa walengwa! ni mtazamo tu!
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Haya ndiyo chadema, katika zunguka yao, wawambie wananchi ingawa nao baadhi wameshalambishwa!
   
 12. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hivi mwanasheria tuliowasomesha bure enzi za nyerere na hao wanaokopeshwana hawalipi fedha zetu hamna uzalendo wa kulitetea taifa na uzulumati huu
   
 13. k

  kayumba JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Hiyo ni kuchochea udikteta!

  Usalama hawaitajiki kwa hili, kinachotakiwa ni polisi kukamata na mwanasheria wa serikali kumpeleka mahakamani PERIOD
   
 14. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Haya Bana.:A S 13:
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Majaji watatu waliosikiliza shauri hilo – Gerald Aksen kutoka Marekani, Swithin Munyantwali kutoka Uganda na Sir Jonathan Parker wa Uingereza – wanasema, "…baada ya kusikiliza kwa makini maelezo ya Henry Surtees, Mtunza Fedha wa kampuni ya Caspian (inayomilikiwa na Rostam Aziz), tumeridhika kwamba Surtees ndiye aliyekwenda Marekani kujadiliana na wamiliki wa Richmond na alitumwa kufanya kazi hiyo na Bw. Rostam Aziz."
  The evidence against Rostam is simply overwhelming...............................
   
 16. n

  ngoko JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watawezaje wakati yeye ndiye anawapa command ? Kabla hawajafanya jambo lolote lazima lipate baraka za RA la sivyo watekelezaji watawekwa kwenye vijiwe visivyokuwa na urafiki na mifuko yao
   
 17. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kama RA na JK ni marafiki, basi tegemea RA na Usalama wa Taifa kuwa kitu kimoja pia.
  just simple and clear
   
 18. e

  emma 26 Senior Member

  #18
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa anatakiwa kufirisiwa na kufungwa maisha.kwan mpaka sasa anayetuzungusha ni yeye tu.na ametuona sisi wajinga.ndo maana anatuzugusha tu
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Do some editing pls ni usalama wa viongozi wa CCM sio wa TAIFA.
  Watu wanahujumu uchumi wetu wazi wazi bado wanawaangalia tuu katika hili tutamkumbuka sana Mwalimu J.K.
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo bwana ni mjanja sana!
   
Loading...