Kumbuka, Caspian walipewa mkataba wa kujenga misingi na viegesho vya yatapokaa hayo majenereta.
Na RA kama mfanya biashara ana haki ya kufatilia ni nani anapewa mkataba ili na yeye apate kazi.
ni kawaida kabisa ya mfanya biashara yeyote wa kimataifa duniani kutafuta mwenyeji wa kuwasimamia na kuwaongoza wapi pa kwenda nani wa kumuona.
Hakuna kampuni ya nje inayofanya kazi Tanzania bila kuwa na mwenyeji. Na si lazima mwenyeji awe ni mmoja wa wwamiliki kwa sheria za Tanzania.
Kwani Richmond au Dowans mwenyeji wao akiwa Rostam, kuna kosa? Kama RA kamtuma mfanyakazi wake kwenda kuwaona Richmond kwa kutaka kujuwa uwezo wa hawa Richmond, kumbuka aliemtuma ni mtunza fedha wake! Huoni kuwa hapo RA kafanya jambo la maana kama mfanya biashara?
Kama RA kamtuma mfanyakazi wake kwenda kuonana na Richmond kwa ajili ya kumuwakilisha Dowans, jee hapo kuna kosa?
RA "anakamatika", ni nani asiekamatika Tanzania? Labda Rais tu. Lakini, kukamatika si lazima uwe na hatia. Mpaka sasa sijaona wapi RA ana hatia au Adawi au Dowans.