Mahakama Moshi yaruhusu kilimo kuendelea kwenye shamba la Mbowe

Uthibitisho kuwa anachafua mazingira ni upi?

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
Wivu na Roho mbaya ya Kikolomije, Roho za Visasi kwa kuwa ni Mpinzani. Upande wa pili yupo Mzungu wa Maua anapeta.
 
Wewe unashangiria Mbowe Kuharibu Chanzo cha maji!
Kweli Kibendera ni kibendera tu

"UKISHINDWA KUPAMBANA NAO UNGANA NAO"
Wewe unakijua chanzo cha mto Weruweru? Kama hikijui kafanye utafiti kwanza.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Sophist Hapa ndipo hoja yangu ilipo.
Mkuu kuna watu wanaamini hisia zao kuliko uhalisia. Na kwa kuwa wanakuwa wameruhusu akili iendeshwe na hisia hawawezi kukuelewa. Nimeona jinsi ambavyo umekuwa fair ktka maelezo yako kwenye post zako. Hujawa upande mmoja, umejaribu kuonesha kasoro za pande zote. Anayesoma ili aelewe ataelewa, lakini anayesoma ili akujibu.....!!
 
Kuna kosa la kiufundi ambalo watu wanaounga mkono Upinzani waache kulifanya mara moja. Ni kweli kuwa Mahakama za Tanzania wakati mwingine zinafanya maamuzi kwa shinikizo la kisiasa, lakini si sahihi kusema kwamba mahakama imeelekezwa cha kufanya kwa kuwa tu walioko madarakani ni CCM na wapinzani wameshindwa kesi husika.

Leo Mbowe kapewa zuio na kuruhusiwa kuendelea na kilimo, jee wale wanaoishutumu mahakama kwa kuingiliwa na CCM katika hili watasemaje? Hoja yangu hapa ni rahisi, kama kuna kesi dhidi ya wapinzani inapoamuliwa kinyume cha matarajio, basi zijengwe hoja zenye mashiko badala ya kuishia kusema mahakama haiko huru.

Kuna ushahidi kwamba Kesi nyingi za kisiasa ambazo watu wa Upinzani hushindwa, hushindwa si kwa sababu mahakama haiko huru, bali hushindwa kwa kuwa CCM inalindwa na sheria mbovu wanazozilinda zisibadilishwe. Mahakama hutumia sheria kufanya maamuzi na kama sheria hizo ni mbovu basi na maamuzi ya mahakama yatakuwa ni mabovu vile vile.

Sherehe ya leo iwe mwanzo wa kuamini kwamba mahakama ziko huru lakini zinafungwa kwenye baadhi ya mambo hasa yahusuyo uhuru wa kujieleza kwa kuwa huko kuna sheria mbovu na mbaya sana zinazowapa walioko madarakani fursa ya kusikilizwa na mahakama.

Kesi ya Mgombea Huru, Mita miambili, nguvu za RC na DC, kesi ya kuhoji mamlaka ya bunge na nyingine zote chanzo cha kushindwa si mahakama bali sheria ambazo zinalindwa kwa udi na uvumba na CCM zisibadilishwe milele. Na ndiyo maana waliikataa Rasmu ya Katiba ya Jaji Warioba kwa kuwa walijua kwamba kwa Katiba ile sheria hizo zingefutiliwa mbali!
mkuu umeandika kwa busara sana, ila kuna baadhi ya kesi huwa zinaonekana dhahiri kuwa kuna maelekezo kutoka juu ndio maana huwa tunasema hivyo, mfano kipindi Lema yuko mahabusu alikuwa ananyimwa dhamana na hakimu hatoi sababu ya kumnyima dhamana, au kesi ile Mbunge wa Kilombero.
NB: UMEANDIKA KWA BUSARA SANA NA SIAMINI KAMA WEWE NI CCM
 
Wewe unashangiria Mbowe Kuharibu Chanzo cha maji!
Kweli Kibendera ni kibendera tu

"UKISHINDWA KUPAMBANA NAO UNGANA NAO"
Acha kutumika
Unahakika ni chanzo cha maji?,hilo eneo alipewa na nni

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Hapa patamu sana. Lazima huyo mknd akamuliwe hizo pesa zipitie kwenye qumer yake. Aliharipu mazao ya KUB kisiasa, sasa atayalipa kiuchumi.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Lowasa pia chadema waliimba miaka 20 kuwa fisadi ghafla wakasema lowasa mtakatifu na jina lake wakaliondoa list Of shame huyo jaji hukumu yake aliyotoa jaji mkuu atoe ufafanuzi Kama imezingatia sheria zote ikiwemo ya mazingira
Hii inahusianaje na vandalism ya miundombinu na kesi mahakamani?

Sent from my SM-J710F using JamiiForums mobile app
 
Wewe unashangiria Mbowe Kuharibu Chanzo cha maji!
Kweli Kibendera ni kibendera tu

"UKISHINDWA KUPAMBANA NAO UNGANA NAO"
Umeliona hilo shamba liko kwenye chanzo cha maji?

Sent from my ALE-UL00 using JamiiForums mobile app
 
Kuna kosa la kiufundi ambalo watu wanaounga mkono Upinzani waache kulifanya mara moja. Ni kweli kuwa Mahakama za Tanzania wakati mwingine zinafanya maamuzi kwa shinikizo la kisiasa, lakini si sahihi kusema kwamba mahakama imeelekezwa cha kufanya kwa kuwa tu walioko madarakani ni CCM na wapinzani wameshindwa kesi husika.

Leo Mbowe kapewa zuio na kuruhusiwa kuendelea na kilimo, jee wale wanaoishutumu mahakama kwa kuingiliwa na CCM katika hili watasemaje? Hoja yangu hapa ni rahisi, kama kuna kesi dhidi ya wapinzani inapoamuliwa kinyume cha matarajio, basi zijengwe hoja zenye mashiko badala ya kuishia kusema mahakama haiko huru.

Kuna ushahidi kwamba Kesi nyingi za kisiasa ambazo watu wa Upinzani hushindwa, hushindwa si kwa sababu mahakama haiko huru, bali hushindwa kwa kuwa CCM inalindwa na sheria mbovu wanazozilinda zisibadilishwe. Mahakama hutumia sheria kufanya maamuzi na kama sheria hizo ni mbovu basi na maamuzi ya mahakama yatakuwa ni mabovu vile vile.

Sherehe ya leo iwe mwanzo wa kuamini kwamba mahakama ziko huru lakini zinafungwa kwenye baadhi ya mambo hasa yahusuyo uhuru wa kujieleza kwa kuwa huko kuna sheria mbovu na mbaya sana zinazowapa walioko madarakani fursa ya kusikilizwa na mahakama.

Kesi ya Mgombea Huru, Mita miambili, nguvu za RC na DC, kesi ya kuhoji mamlaka ya bunge na nyingine zote chanzo cha kushindwa si mahakama bali sheria ambazo zinalindwa kwa udi na uvumba na CCM zisibadilishwe milele. Na ndiyo maana waliikataa Rasmu ya Katiba ya Jaji Warioba kwa kuwa walijua kwamba kwa Katiba ile sheria hizo zingefutiliwa mbali!
Angalia kesho utajua kuwa serekile yako ilivyo na uchama

Sent from my ALE-UL00 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo wewe na huyo DC ndio mnajua zaidi uharibifu wa chanzo cha Maji kuliko jaji? Ngoja hizo milioni 500 huyo DC atakamuliwa zitoke kwenye any tundu possible.
Alikuwa anaona sifa kuvunja mabomba huku anajipiga selfie sasa atajua kwa nini nyeti za kuku hazionekani mpaka uje upepo
Yule DC Alitarajia Magufuli atapjgia simu jaji, mahaji wameshamshtukia Magu.Ndio naana hawapokei simu zake siku hjzi.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Mabashite ya ccm tabu kweli huyo raisi atakuja kaa pembenI si Mungu wala si raisi wa maisha
Anayeruhusiwa kusaini mtu anyongwe hadi kufa ni raisi tu sio jaji. Jaji aliyetoa hii hukumu ni kuwa kasaini hati Ya kifo Kuwa ruksa mtu kufa kwa uchafuzi wa mazingira wa mto hadi kesi ya msingi isikilizwe. Hajazingatia sheria Ya mazingira huyo jaji. Jaji mkuu ingilia kati hukumu aliyotoa ni sawa Na kuindinisha hukumu Ya kifo kuwa ruksa watu kuFa na uchafuzi wa mazingira hana mandate Ya kusaini hati Ya kifo huyo jaji
 
Bora kuna judge huyu anajitambua. Hasara za kukurupuka. Tunaendelea next..... tutafanikiwa tu!
 
Ajabu ni kwamba Mkuu wa Mkoa mpya wa Kimanjaro,Anna Mghwira, alipongeza uamuzi wa kuharibiwa shamba hilo.
 
"Mahakama kuu masijala ya Moshi (Moshi Registry), imeruhusu shughuli za kilimo kuendelea kwenye shamba la kampuni ya Kilimanjaro Veggies inayomilikiwa na FREEMAN MBOWE Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, huku kesi ya msingi ikisubiriwa kusikilizwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Bw.Gelasius Byakanwa.

Katika kesi hiyo ambayo Kilimanjaro Veggies inadia fidia ya Millioni 549 kufuatia shamba lake kuingiliwa na kuharibiwa miundombinu yake na mshitakiwa huyo.

Aidha, Kampuni hii ya Kilimanjaro Veggies inawakilishwa na Wakili Menraid D'souza. Uamuzi huu wa kuruhusu shughuli za kilimo kwenye shamba hilo umetolewa na Jaji Sumari wa Mahakama Kuu Moshi.

Maombi mengine yaliyomo kwenye kesi hiyo ni pamoja na kuondoa zuio lililowekwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai la kuzuia shughuli za kilimo kwenye shamba hilo.

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 13. JULY 2017. Kesi hii inafuatiwa baada ya kitendo cha Mkuu wa Wilaya hiyo cha tarehe 12, June 2017 cha kuvamia na kubomoa miundombinu na mazao ya shamba linalomilikiwa na kampuni hiyo lililopo kijiji cha Nshara ambapo ni nyumbani kwa Mhe.Mbowe.

The High Court of Tanzania Moshi Registry has granted an interim order allowing Kili Veggies Limited a Company owned by Hon.Freeman Aikaeli Mbowe to resume it agriculture activites on its farms which was earlier stoped by the orders of Hai District Commissioner Mr.Gelasius Byakanwa. In a rulling divered by Honorable Sumari, Judge of the Moshi Registry High Court following an application filed by the company through the services of Mr Menraid D'souza Advocate in the matter which the District Commissioner is sued in his personal capacity.

Kilimanjaro Veggies is claiming some of Tshs.549 Million against the DC who, according to the claims of the company, the DC had trespassed and destroy the green house infrastructure of the farm owened by the company without any legal or administrative justifications.

The case is following the act of the Hai DC who on the 12 June 2017 entered into the Companies farm in Mbowe's home Nshara Village where he ordered a total destruction of the green house farm claiming the same to be polluting a nearby river water.
Mimi nimwana CCM, kitendo cha Mkuu wa Wilaya ni cha mtu asiyeenda shule.
Kisiasa na kibinadamu hakina mantiki.
 
Back
Top Bottom