Mahakama Moshi yaruhusu kilimo kuendelea kwenye shamba la Mbowe

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,795
71,214
"Mahakama kuu masijala ya Moshi (Moshi Registry), imeruhusu shughuli za kilimo kuendelea kwenye shamba la kampuni ya Kilimanjaro Veggies inayomilikiwa na FREEMAN MBOWE Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, huku kesi ya msingi ikisubiriwa kusikilizwa dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Bw.Gelasius Byakanwa.

Katika kesi hiyo ambayo Kilimanjaro Veggies inadia fidia ya Millioni 549 kufuatia shamba lake kuingiliwa na kuharibiwa miundombinu yake na mshitakiwa huyo.

Aidha, Kampuni hii ya Kilimanjaro Veggies inawakilishwa na Wakili Menraid D'souza. Uamuzi huu wa kuruhusu shughuli za kilimo kwenye shamba hilo umetolewa na Jaji Sumari wa Mahakama Kuu Moshi.

Maombi mengine yaliyomo kwenye kesi hiyo ni pamoja na kuondoa zuio lililowekwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai la kuzuia shughuli za kilimo kwenye shamba hilo.

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 13. JULY 2017. Kesi hii inafuatiwa baada ya kitendo cha Mkuu wa Wilaya hiyo cha tarehe 12, June 2017 cha kuvamia na kubomoa miundombinu na mazao ya shamba linalomilikiwa na kampuni hiyo lililopo kijiji cha Nshara ambapo ni nyumbani kwa Mhe.Mbowe.

======

Moshi. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ameiomba Mahakama imuunganishe Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika kesi ya madai ya fidia ya Sh549 milioni iliyofunguliwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Kiini cha kesi hiyo ni hatua ya Byakanwa, kudaiwa kuharibu miundombinu ya umwagiliaji ya shamba (green house) la kampuni ya Kilimanjaro Veggie Ltd (KVL) linalomilikiwa na Mbowe, Juni 19.

Mbowe, ambaye ni mbunge wa Hai na mkurugenzi mwendeshaji wa KVL, amemshtaki mteule huyo wa Rais kama mtu binafsi.

Ombi la kutaka AG aunganishwe, liliwasilishwa mahakamani jana na wakili Modestus Njau anayemtetea Byakanwa mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Aishiel Sumari.

Kwanza wakili huyo aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa sababu ndiyo kwanza alikuwa amepewa kazi hiyo juzi, hivyo alikuwa bado hajapitia nyaraka za kesi hiyo na kuwasilisha majibu yake.

Pia, aliomba AG aunganishwe akisema mkuu wa wilaya hawezi kushtakiwa binafsi kutokana na Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997, kifungu cha kwanza na cha pili, ambavyo alisema vinataja kazi za mkuu wa wilaya.

Wakili huyo alisema hata amri ya kwanza, kanuni ya tatu ya Sheria ya Uendeshaji Mashauri ya Madai (Civil Procedure Code), Sura ya 33 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, inahusika katika kesi hiyo.

Katika maelezo yake, wakili huyo alisema Byakanwa alikuwa akitekeleza wajibu wake kama mkuu wa wilaya na si mtu binafsi kama ambavyo ameshtakiwa na Mbowe.

Hata hivyo, wakili wa Mbowe, Meirad D’souza alisema ombi la kuunganishwa kwa AG limekuja mapema kwa vile jana ndiyo ilikuwa iwe siku ya kwanza ya kusikiliza maombi na si kesi ya msingi.

Jaji Sumari alikubali ombi la kuahirishwa kwa kesi na kumuamuru mdaiwa kuwasilisha majibu pinzani ya kiapo kabla au Julai 27 na maombi ya Mbowe yatasikilizwa Agosti 14.

Katika hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani na wakili D’Souza wa jijini Arusha, Mbowe analalamikia kitendo cha Byakanwa kuingia kwa jinai katika shamba hilo na kufanya uharibifu.

Katika kesi ya msingi, Mbowe anasema Byakanwa hakuwa na mamlaka ya kisheria kufanya alichokifanya na kuiomba mahakama itoe zuio la kudumu kwa Byakanwa kutoingilia shughuli za KVL.

Pia, anaiomba Mahakama imuamuru Byakanwa kumlipa fidia maalumu ya Sh549.3 milioni inayotokana na uharibifu wa mali, usumbufu na hasara ambayo KVL imepata.

Kampuni hiyo inaiomba mahakama imuamuru Byakanwa kulipa riba ya asilimia 25 ya fedha hizo na pia aamuriwe kulipa gharama ya kesi hiyo.

Mbali na kesi ya msingi, Mbowe amewasilisha maombi namba 51/2017 akiambatanisha kiapo cha kutaka kesi hiyo isikilizwe chini ya hati ya dharura.

Mbali na kung’oa miundombinu, Juni 13, Mamlaka ya Taifa ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), iliitoza KVL faini ya Sh18 kwa kuendesha kilimo ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji.

Mamlaka zinadai kuwa shamba hilo lililopo Kijiji cha Nshara Machame, liko ndani ya mita 60 kutoka katika Mto Weruweru, kitu eambacho ni kinyume cha sheria

Chanzo: Mwananchi
The High Court of Tanzania Moshi Registry has granted an interim order allowing Kili Veggies Limited a Company owned by Hon.Freeman Aikaeli Mbowe to resume it agriculture activites on its farms which was earlier stoped by the orders of Hai District Commissioner Mr.Gelasius Byakanwa. In a rulling divered by Honorable Sumari, Judge of the Moshi Registry High Court following an application filed by the company through the services of Mr Menraid D'souza Advocate in the matter which the District Commissioner is sued in his personal capacity.

Kilimanjaro Veggies is claiming some of Tshs.549 Million against the DC who, according to the claims of the company, the DC had trespassed and destroy the green house infrastructure of the farm owened by the company without any legal or administrative justifications.

Hapo awali Mkuu wa Wilaya ya Hai, aliamuru Shamba hilo kuharibiwa.

Habari zaidi soma=>Mkuu wa Wilaya ya Hai, aamuru shamba la Freeman Mbowe la Mbogamboga liharibiwe, Mbowe alaani!
 
Wewe unashangiria Mbowe Kuharibu Chanzo cha maji!
Kweli Kibendera ni kibendera tu





"UKISHINDWA KUPAMBANA NAO UNGANA NAO"
Kwahiyo wewe na huyo DC ndio mnajua zaidi uharibifu wa chanzo cha Maji kuliko jaji? Ngoja hizo milioni 500 huyo DC atakamuliwa zitoke kwenye any tundu possible.
Alikuwa anaona sifa kuvunja mabomba huku anajipiga selfie sasa atajua kwa nini nyeti za kuku hazionekani mpaka uje upepo
 
Kuna kosa la kiufundi ambalo watu wanaounga mkono Upinzani waache kulifanya mara moja. Ni kweli kuwa Mahakama za Tanzania wakati mwingine zinafanya maamuzi kwa shinikizo la kisiasa, lakini si sahihi kusema kwamba mahakama imeelekezwa cha kufanya kwa kuwa tu walioko madarakani ni CCM na wapinzani wameshindwa kesi husika.

Leo Mbowe kapewa zuio na kuruhusiwa kuendelea na kilimo, jee wale wanaoishutumu mahakama kwa kuingiliwa na CCM katika hili watasemaje? Hoja yangu hapa ni rahisi, kama kuna kesi dhidi ya wapinzani inapoamuliwa kinyume cha matarajio, basi zijengwe hoja zenye mashiko badala ya kuishia kusema mahakama haiko huru.

Kuna ushahidi kwamba Kesi nyingi za kisiasa ambazo watu wa Upinzani hushindwa, hushindwa si kwa sababu mahakama haiko huru, bali hushindwa kwa kuwa CCM inalindwa na sheria mbovu wanazozilinda zisibadilishwe. Mahakama hutumia sheria kufanya maamuzi na kama sheria hizo ni mbovu basi na maamuzi ya mahakama yatakuwa ni mabovu vile vile.

Sherehe ya leo iwe mwanzo wa kuamini kwamba mahakama ziko huru lakini zinafungwa kwenye baadhi ya mambo hasa yahusuyo uhuru wa kujieleza kwa kuwa huko kuna sheria mbovu na mbaya sana zinazowapa walioko madarakani fursa ya kusikilizwa na mahakama.

Kesi ya Mgombea Huru, Mita miambili, nguvu za RC na DC, kesi ya kuhoji mamlaka ya bunge na nyingine zote chanzo cha kushindwa si mahakama bali sheria ambazo zinalindwa kwa udi na uvumba na CCM zisibadilishwe milele. Na ndiyo maana waliikataa Rasmu ya Katiba ya Jaji Warioba kwa kuwa walijua kwamba kwa Katiba ile sheria hizo zingefutiliwa mbali!
 
Hongera kwa kamanda wa anga atlast

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom