Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Jumanne Agosti 12, 2025 inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mapingamizi ya upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, yanayolenga kupinga matumizi ya mashahidi wa siri.
Katika mapingamizi hayo, upande wa utetezi unapinga mashahidi kutoa ushahidi bila mshitakiwa kuwaona moja kwa moja, na badala yake kusikia sauti pekee. Utetezi umedai kuwa utaratibu huo unakiuka haki za mshitakiwa kupata utetezi wa haki.
Kesi hiyo itasikilizwa mbele ya Jaji Elizabeth Mkwizu.
=========================
Mahakama Kuu yapigilia msumari uamuzi kufichwa kwa mashahidi wa Jamhuri katika kesi ya Lissu
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo, Jumanne, Agosti 12, 2025, imetupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi wa Tundu Lissu katika kesi ya marejeo (judicial review) iliyolenga kupinga matumizi ya mashahidi wa siri.
Katika mapingamizi hayo, upande wa utetezi ulipinga uhalali wa mashahidi wa siri katika kesi ya kuchapisha taarifa inayomkabili Tundu Lissu katika Mahakama ya Kisutu, ambapo Jamhuri iliwasilisha ombi la kuficha baadhi ya mashahidi.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Elizabeth Mkwizu, huku upande wa Lissu, kupitia Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala, ukieleza kutoridhishwa na uamuzi huo.