figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
1. MAHAKAMA KUU YA TANZANIA -TANGA YAWALINDA MADIWANI WA CUF KUTOKANA NA UHUNI WA LIPUMBA NA GENGE LAKE:
2. YAIZUIA NEC NA MAMLAKA ZOTE KUTANGAZA NAFASI WAZI NA KUZIJAZA:
3. WASOMI MAWAKILI JUMA NASSORO NA DAIMU HALFANI WAENDELEA KUMBURUZA, NA KUMFUNDISHA TAALUMA YA SHERIA WAKILI MASHAKA NGOLE:
Issued on: 28 July, 2018
MBELE YA MHESHIMIWA JAJI BENHAJJ MASOUD Mahakama Kuu–Tanga imetoa AMRI ya kumzuia Lipumba, Sakaya, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga na Mamlaka zingine zote ikiwemo NEC kuendelea na hatua zozote za kutaka kutangaza uwepo wa nafasi wazi za Udiwani kutokana na madai ya kuwavua Uanachama na Uwakilishi wa Wananchi [Udiwani] waombaji [Applicants] Rashid Jumbe Hamza [Diwani wa Kata ya Mwanzange, Fatuma Maine Hamza [Diwani Viti Maalumu], na Halima Juma Mbwana [Diwani Viti Maalumu] mpaka pale shauri la Msingi [Miscellaneous Cause No. 2 of 2018] litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Maamuzi hayo yametolewa Alhamisi Tarehe 26/7/2018 mbele ya Mawakili wa Jiji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatia maombi madogo [Miscellenous Civil Application No. 30 of 2018] yaliyowasilishwa Mahakama Kuu na Waombaji [Applicants] kuomba kibali kwa ajili ya kuomba AMRI ya Mahakama Kuu kuzuia utekelezwa wa madai ya kuvuliwa Uanachama kwa wahusika [“…PREROGATIVE ORDERS OF CERTIORARI AND PROHIBITION…”]
Shauri hilo limepangwa kutajwa Agosti 6, 2018. Madiwani wa CUF wanawashtaki Magdalena Sakaya, Lipumba, Mashaka Ngole, Halmashauri ya Jiji la Tanga [Tanga City Council], Mkurugenzi wa ya Jiji la Tanga [Executive Director Tanga City Council] pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali [The Honourable Attorney General]. CUF imewakilishwa na Wasomi Mawakili Juma Nassoro na Daimu Halfani ambao wameendelea kumburuza, kumshughulisha na kumfundisha Taaluma ya Sheria Wakili wa Lipumba Mashaka Ngole.
Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad amewaondoa hofu Wanachama, na Viongozi wote wa Chama kiserikali [Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitingoji] kuwa “CUF itaendelea kuwatetea na kuwalinda dhidi ya kundi la Wahuni waliopandikizwa na vyombo vya dola kutaka kukivuruga Chama”. Amesema “CUF itaendelea kutumia njia za Kisheria kudai Haki na kuwahakikishia kuwa CUF ndio itakayoibuka MSHINDI, kwani HAKI haizami hata siku moja”.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa
SALIM BIMANI
MKURUGENZI -MHUMU
Pia soma =>Mkurugenzi wa Jiji la Tanga awafukuza udiwani, madiwani wanne wa CUF, baada ya kupokea barua ya Magdalena Sakaya

Last edited by a moderator: