Mahakama: Dr. Slaa ruksa kuoana na Josephine

Mahakama: Dr. Slaa ruksa kuoana na Josephine

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Posts
4,781
Reaction score
3,213
Kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa na Aminiel Mahimbo vs Josephine Mushumbusi kesi ya rufaa ya kupinga talaka iliyotolewa na mahakama ya mwanzo Sinza katika kesi ya ndoa namba 4/2012 , baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali na mahakama ya hakimu mkazi mahakama ya wilaya ya kinondoni ndugu Wambura, katika kesi ya rufaa namba 32/2012.

Ametoa uamuzi huo baada ya kuridhika kwamba kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwa mahakama ya mwanzo kutoa talaka hiyo na hivyo Josephine ni mtalikiwa rasmi.

Kutokana na hukumu hiyo, Josephine ana haki ya kuolewa na mtu mwingine kwa kuwa ni mtalakiwa.
attachment.php

Dar es Salaam. Mpenzi wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa, Josephine Mshumbusi ameshinda rufaa ya kupinga talaka yake, iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe wa ndoa, Aminiel Mahimbo.

Josephine kwa sasa amekuwa akiishi na Dk Slaa na tayari wamefanikiwa kupata mtoto mmoja, lakini harakati zao za kufunga ndoa zimekwama baada ya kupingwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Rose Kamili akidai kuwa ana ndoa halali na Dk Slaa.

Mahimbo alikata rufaa hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akipinga hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Sinza iliyotoa talaka kwa Josephine dhidi yake, mwaka 2012.

Pamoja na mambo mengine, Mahimbo katika rufaa yake hiyo namba 32/2012, alikuwa akidai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kiasi cha kuifanya Mahakama ya Mwanzo Sinza kutoa talaka hiyo.

Hata hivyo jana, Hakimu Aniseth Wambura aliyesikiliza rufaa hiyo, aliitupilia mbali ombi hilo akisema kuwa ameridhika na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Sinza kwamba kulikuwa na ushahidi wa kutosha kutoa talaka kwa Josephine.

Hakimu Wambura alisema katika hukumu hiyo,baada ya kupitia hoja za mrufani na za mjibu rufaa pamoja na mwenendo wa kesi ya msingi,amekubaliana na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Sinza kuwa ni sahihi.

Katika kesi ya msingi Josephine, alidai talaka kutoka kwa Mahimbo, pamoja na kudai kuwa Mahimbo hakuwa mwaminifu kwa kuwa alikuwa akitoka nje ya ndoa na kwamba alikuwa amemtelekeza bila kumpatia mahitaji na huduma za msingi, huku akimtesa.

Hakimu Wambura katika hukumu yake jana kwenye rufaa hiyo alisema, kutokana na sababu zilizotolewa na Josephine katika kesi ya msingi ni dhahiri kuwa hapakuwa na ndoa na kwamba mahakama haiwezi kuwalazimisha watu ambao hawapatani kuishi pamoja.

"Baada ya kusikiliza hoja za mrufani na mjibu rufaa ,mahakama hii imekubaliana hoja za mjibu rufaa (Josephine), kuwa kwa tabia ile mbaya na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake hapakuwapo na ndoa baina yao.", alisema Hakimu Wambura.

"Hivyo mahakama hii inatangaza kuwa hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa sahihi," alisema kwa msisitizo Hakimu Wambura.

Wakili wa Josephine, Philemon Mutakyamilwa alisema kuwa amefurahishwa na hukumu hiyo akidai kuwa mahakama hiyo imetenda haki kwa mteja wake.

Licha ya kupangua kikwazo hicho, Josephine bado anakabiliwa na kikwazo kingine kilichomweka njia panda katika mipango yake ya kufunga ndoa na Dk Slaa

Josephine na Dk Slaa walitarajia kufunga ndoa Julai 21, 2012, lakini imekwama baada ya Rose Kamili kufungua kesi Mahakama Kuu akiipinga kwa madai kuwa ana ndoa halali na Dk Slaa.

Pamoja na pingamizi hilo, Rose anamtaka Dk Slaa amlipe Sh50 milioni kama fidia ya kujihudumia pasipo matunzo ya mumewe huyo, huku pia akimtaka Josephine amlipe Sh500 milioni kama fidia ya maumivu aliyoyapata kutokana na kitendo chake cha kuingilia ndoa yake.

Kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2012, inasikilizwa na Jaji Lawrance Kaduri, na itatajwa tena mahakamani hapo Julai 17, mwaka huu.

Ee Mungu ahsante kwa kutenda haki.Watanzania wanaunga mkono maamuzi haya ya mahakama.
 
-Leo Asubuhi mahakama imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Aminiel Mahimbo.Mnakumbuka Josephine aliomba talaka na mahakama ikaamuru apewe baadae Aminiel Mahimbo alikata rufaa.

-Matrimonial Appeal number 32/2012, Aminiel Mahimbo Vs Josephine Mushumbusi,Rufaa ya kupinga Talaka iliyotolewa na mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya Ndoa number 4/2012 imetupiliwa mbali Leona hakimu Mkazi Wambura wa mahakama ya Wilaya ya Kinondoni,Ikitoa hukumu kwenye sababu za rufaa hakimu wa wilaya ameridhika kwamba kulikuwepo na ushahidi wa kutosha kwa mahakama ya mwanzo kutoa talaka kwa wadaiwa.

-Haki ya mtu haipotei,haki inaweza kuchelewa tu.
 
Safi,Hongera Kamanda wa mstari wa mbele.

Angalizo,

hali ya Mtwara ifatiliwe kwa ukaribu kuliko wakati wowote.Kuna uelekeo mkubwa haki za binadamu zinavunjwa tena dhahiri.Bila kusimama na wananchi hao wakati huu nadhani matokeo yake tunayajua.
 
Hahahha mkuu umenikumbusha mbali sijui Makamba na Ma-CCM yaliyo-capitalize kwenye mambo binafsi ya watu watajiskiaje sasa.Walionywa lakini!
 
Kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa na Aminiel Mahimbo vs Josephine Mushumbusi kesi ya rufaa ya kupinga talaka iliyotolewa na mahakama ya mwanzo Sinza katika kesi ya ndoa namba 4/2012 , baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali na mahakama ya hakimu mkazi mahakama ya wilaya ya kinondoni ndugu Wambura, katika kesi ya rufaa namba 32/2012.

Ametoa uamuzi huo baada ya kuridhika kwamba kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwa mahakama ya mwanzo kutoa talaka hiyo na hivyo Josephine ni mtalikiwa rasmi.

kutokana na hukumu hiyo Josephine ana haki ya kuolewa na mtu mwingine , kwa kuwa ni mtalakiwa.

Why today?
 
Suala la Dr.Slaa lilikamatiwa bango sana, je hao wanaojiita viongozi wanaweza thubutu kuweka wazi vyeti vya ndoa zao?
 
Duh, Kwani walikuwa hawajaoana?.

Kumbe walikuwa/wanaendelea kuzini kulingana na macho ya imani ya Roman catholic church?.

Sijui kanisa nalo lina sheria ya double jeopardy kwa haya makosa mawili 1)Kuasi Upadri 2)kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto kabla ya kuoana.
 
Baba, rais wangu...chukua kwa amani huyu mama yetu, ni first lady wetu...
 
haaaahaaaaaaaa.........commentator "the babuus make the incredible shot to the far post"
 
Duh, Kwani walikuwa hawajaoana?.

Kumbe walikuwa/wanaendelea kuzini kulingana na macho ya imani ya Roman catholic church?.

Sijui kanisa nalo lina sheria ya double jeopardy kwa haya makosa mawili 1)Kuasi Upadri 2)kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto kabla ya kuoana.

CCM sijui mtafanyaje tena
 
Haya Ritz kaolewe na mahimbo sasa yupo single .. Si ulikuwa unalalamika kuwa kaibiwa mke
 
Last edited by a moderator:
Duh, Kwani walikuwa hawajaoana?.

Kumbe walikuwa/wanaendelea kuzini kulingana na macho ya imani ya Roman catholic church?.

Sijui kanisa nalo lina sheria ya double jeopardy kwa haya makosa mawili 1)Kuasi Upadri 2)kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto kabla ya kuoana.

Ngoja tutoke mtwara kwanza msituchanganyie habari.Tuangalie wanaenda kukatwa mapembe ni kina nani.au kama wanaenda kujikata wenyewe.Then nitarudi kwa swala jema la rais wangu slaa.
 
Mods, bana siku zote hii issue ilikuwa kule jukwaa la siasa leo baada ya hii propaganda kushindwa mahakamani wanaona sio huko tena , why?
 
Duh, Kwani walikuwa hawajaoana?.

Kumbe walikuwa/wanaendelea kuzini kulingana na macho ya imani ya Roman catholic church?.

Sijui kanisa nalo lina sheria ya double jeopardy kwa haya makosa mawili 1)Kuasi Upadri 2)kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto kabla ya kuoana.
p
na wewe bana , siku zote ulikuwa unasema oohhh kaiba mke , leo unataka na kanisa liwasaidie kwenye propaganda ......Mwampamba na Shonza , Nnape na Mwigulu sijui watakuwa na lipi tena la kuongea mitaani baada ya hukumu ya leo ,
 
Back
Top Bottom