Dar es Salaam. Mpenzi wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa, Josephine Mshumbusi ameshinda rufaa ya kupinga talaka yake, iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe wa ndoa, Aminiel Mahimbo.
Josephine kwa sasa amekuwa akiishi na Dk Slaa na tayari wamefanikiwa kupata mtoto mmoja, lakini harakati zao za kufunga ndoa zimekwama baada ya kupingwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Rose Kamili akidai kuwa ana ndoa halali na Dk Slaa.
Mahimbo alikata rufaa hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akipinga hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Sinza iliyotoa talaka kwa Josephine dhidi yake, mwaka 2012.
Pamoja na mambo mengine, Mahimbo katika rufaa yake hiyo namba 32/2012, alikuwa akidai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha kiasi cha kuifanya Mahakama ya Mwanzo Sinza kutoa talaka hiyo.
Hata hivyo jana, Hakimu Aniseth Wambura aliyesikiliza rufaa hiyo, aliitupilia mbali ombi hilo akisema kuwa ameridhika na hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Sinza kwamba kulikuwa na ushahidi wa kutosha kutoa talaka kwa Josephine.
My Take:
Huyu Kiogozi wetu ana wapenzi wawili ndani ya chama kimoja? Huyu mbuge wa vitu maalumu na josephine mtaalamu wa mambo ya technologia africa hii haiwezi kuwa ni tatizo katika kutekeleza majukumu yake? Wapi muongozo wa maadili kwa wanachama wa chadema?