Mahafali ya CHASO Dodoma kufanyika tarehe 23 July 2016

Kwa taarifa nilizopata kutoka kwa viongozi wa CHASO na BAVICHA Dodoma ni kwamba yale mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Dodoma ambayo yalishindwa kufanyika baada ya kuzuiliwa na polisi, sasa yatafanyika tarehe 23 july.

Mahafali hayo yanafanyika baada ya Polisi kutoa ufafanuzi ya kwamba hawajazuia matukio ya ndani ya kisiasa.

Tulipotaka ufafanuzi juu ya kwanini waliamua kufanya mahafali hayo siku ambayo CCM watakuwa wanafanya mkutano mkuu wao, walidai ya kwamba ni siku ambayo wanachuo wote watakuwa huru baada ya mitihani yao, pia hawaoni tatizo sababu mahafali yao yanafanyika katika ukumbi tofauti na ule wa CCM. Pia walidai ya kwamba tayari wameshapata kibali cha kufanya tukio hilo na wamehakikishiwa ulinzi wa kutosha, hivyo wanawaomba watu wanaopenda kuhudhuria tukio hilo kuwa na amani.

Mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa mjumbe wa kamati kuu na aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa.
Hayataruhusiwa...! Hivi wana graduate nini? Uana harakati kama alivyo sema mwana hisa mkuu Lowasa?
 
Ni kweli sisi wengine tutahakikisha masikio yetu hayazidi kichwa, ila kama baadhi yenu mtakakuwa mnayavuta masikio yenu ili yazidi kichwa hapo ndipo itakuwa shughuli pevu....
atakayeyavuta masikio yazid kichwa atakuwa nsyuka au jini binadamu wa kawaida hawez masikio yako yatabak kuwa ya kwako huwez kupata maumivu wewe kwa kuvutwa masikio mwingine.
 
Kwani kuna shida gani hapo?? Acheni kutokwa mapovu. Chaso watakua na mkutano wao na nyie mtakua na mkutano wenu. Au siku mnayofanya mkutano hamtaki wengine wafanye mikutano yao??
Nyie machadema acheni kujilinganisha na chama chenye dola, ndio maana mnaishia kuwa wanaharakati tu. Ovyo kabisa, kwani wakifanya tarehe 24 kuna tatizo gani?
 
Jana umeona RPC Dodoma katoa magari yote, Polisi wote, pikipiki zote mpaka mbwa wao na kuwazungusha mchana kutwa mitaani eti tuko tayari kwa lolote. Huko ndio kuchanganyikiwa kutokana na kauli ya vijana wa Bavicha. Utadhani wameambiwa majeshi ya Kenya yanakuja kuvmia Dodoma kumbe ni kauli ya kuja kusaidiwa kazi yao ya kuzuia mikutano?

Kwa hiyo BAVICHA lengo lenu ni kuwakosesha usingizi polisi wasipate muda wa kulala na wake zao na waume zao au kulala majumbani mwao kisa nyie mnawakosesha usingizi?

Unajua polisi kitu ambacho hukifanya kwa yule ambaye anawakosesha usingizi ili wapate muda wa kulala fofofo hata kwenye lindo bila shida? Unakijua?

Kama hukijui labda unataka kukijua endeleeni na hizo kampeni zenu za kuhakikisha polisi hawalali mtakigundua ni kitu gani mbele kwa mbele.Ila najua hawawezi kuendelea kukesheshwa macho na BAVICHA forever awe ni mtu mmoja au genge la watu ndani ya BAVICHA.

Nadhani BAVICHA hamuwajui polisi wa Tanzania!!
 
mbona 23 july tu?

Ili inteligensia ya polisi iweze kuona mbali ikiwa hapo hapo Dom hiyo tarehe 22 Julai kwa kuwatumia chadema barua ya sitisho la mahafali yao ya tarehe 23/7/16 kwani yasingemalizika kwa amani.Hio ni moja.Pili baada ya inteligensia yetu kutuonyesha kujipenyeza vijana wa bavicha wenye nia ovu ya kuja kutupa msaada tusiouomba wala kuuhitaji tumeshawaagiza hata wenye nyumba za kulaza wageni wasiwape vyumba.Hivyo kila mwenye nia nzuri na amani ya nchi hii atakubaliana na sababu hizo nzito.Tutatoa nafasi ya mahafali hayo kufanyika kuanzia mwezi wa nane kuendelea.
 
Ni ngumu kuwaelewa nyie ndugu kwa maana hiyo CCM wakiahirisha na nyinyi mtaahirisha kusikilizia wanafanya lini? ni shiidah
 
CHASO ni chuo gani?Alafu tangu lini mahafali yakafananishwa na mkutano wa ndani wa chama unaohusu mambo ya utendaji na utawala?Hapo mm naona huo uchokozi tu kwakua hicho mnacho dai kua mahafali ya CHASO kilishakatazwa
 
nadhani ni stori tu, hamna mkutano wa CHASSO hiyo siku.
kwa sababu wale wa upande wa pili hawatakubali..
in sukuma tone , somebody said 'sitaki hao mavijana wafanye mkutano julai 23,, mkutano tunafanya sisi, pigeni hao niwapandishe macheo sawaa?.'
 
Back
Top Bottom