Bobumikwara
Member
- Jul 17, 2014
- 43
- 13
Umenena mkuu,always God is able.
Ahahah kiukweli hazitofautiani.. Daahhhhh baya zaidi hao washikaji uliosoma.nao wakala shavu.. Ukiwa na matatzo hawapo tayari kukusaidia ingawa wakati mpo chuo ulikuwa mtu muhimu kwao hasa ktk masuala ya taaluma
haya yamenikuta sana mkuu upo sawa ila wakisikia unashavu wanaanza mbona kimya hatutafutani pindi unasota ukiomba msaada nikalenda rah
Japo bado sijapata kazi rasmi, nina ushuhuda wa kuwapa enyi watafutaji wa kazi kama mimi mja wa MUNGU. Kuna waajili wengine hapa nchini wanachangia kutufanya tuonekane kuwa tuna maisha magumu na ionekane kuwa tuna shida sana ya kupata kazi japo sio kwa wote, nakumbuka tar 1/8/2014 +255652198676 company X ilinihitaji kufika dar kwa ajili ya usaili wa Fertilizer Sales Person kwa bahati nzuri nikawaambia nipo nje ya dar kwa maana kwamba npo mkoani, nikasisitizwa kuwa nijitahidi nifike siku hiyo nikajipanga nikaamua kufunga kabiashara kangu hapa mjini ili nielekee huko dar kwa interview. Kitu Cha ajabu ni kwamba nilipoanza safari njiani walikuwa wakinipigia simu kuwa nmefika wapi, ile npo kimara tu, nikatumiwa sms kuwa wamearisha usaili wangu mpaka wiki inayofuata (nitapigiwa simu). Sikuwajibu nikasubiri mpaka niliposhuka kwenye basi ubungo, nikajaribu kuwasiliana nao lakini hawakunielewa kabisa na nikadiriki kuwaomba wanichangie japo nauli ya kurudia POLE SANA MKUU
Asanteeeee!!!!!!!!!!!!!
haya yamenikuta sana mkuu upo sawa ila wakisikia unashavu wanaanza mbona kimya hatutafutani pindi unasota ukiomba msaada nikalenda rah
Umeona ehhhh dahhh nakumbuka kuna mshikaji nilimsaidia sana chuo... Maana alielemewa na alikiri kuwa bila mimi sijui ingekuaje
haya tumekuja mtaani jamaa kapata shavu haraka... Basi kanisahau mpk nimtafute mimi kwa simu
tena smtmz anaweza kuniuliza nani mwenzangu?? aahhh daahhh
haya nikapata dharura kwenda kufanya usaili bahati mbya ukanikuta nikiwa patupu na inabidi nisafiri
nikasema ngoja nimcheki mshikaj.. Daahh akaniahidi kuwa atanisave kiasi flan cha fedha
basi imefika tarehe kumpigia simu hapokei na meseji hajibu...
Ahahahahahahah kiukweli tumwachie Mungu ulipo siku kazi zitapatikana tu... Tenda wema nenda zako
Haya mambo ya Ajira ni kumwachia Mungu pekee yake.
Siku zote ukitaka mafanikio mwachie Mungu awe ndio muamuzi wa mambo yako yote.
Mimi binafsi nilihangaika sana kutafuta ajira bila mafanikio.
Ndipo nilipomrudia Mwenyezi Mungu na kumlilia huku nikifunga na kuomba.
Kwa wakati huu wote nilianza kujiwekea akiba ya tshs 2000 killa siku. Baada ya miezi sita tu nilipata mtaji. Nikafungua kagrocery kangu. Kwa kweli mpaka sasa inanilipa vizuri sana.
Lango moja linapofunguka na mengine yanafunguka, hatimae nilipata kazi.
Ushauri kwa vijana, JIFUNZENI KUWEKA AKIBA NA NI MARUFUKU KUCHAGUA KAZI.
NAWATAKIA KILA LA HERI.
haya yamenikuta sana mkuu upo sawa ila wakisikia unashavu wanaanza mbona kimya hatutafutani pindi unasota ukiomba msaada nikalenda rah