Magumu gani umeyapitia/unayapitia katika kutafuta kazi?

Vipajilink hao mkuu....kama sijakosea.

Sijawataja, najua hata humu jukwaani wapo sana tu na wameiona hiyo post yangu. Naomba waache kabisa huo mchezo maana najua "ustaarab wa mtu sio kuvaa nguo nzuri na tai tu!". Proffessional ya mtu ni pamoja na mambo anayotafanya. Sijajua km watakuwa ndio hao jamaa uliowataja au lah! japo hujakosea saaaana!111111
 
USHAURI WANGU JITAIDI SANA KUOMBA KWA MUNGU AKUFUNGULIE MILANGO YA KAZI, PIA HUDHURIA SANA MAOMBI NA MAOMBEZI MUNGU NIMWAMINIFU SIKU ZOTE. HAKIKA UTAPATA KAZI BILA WASIWASI. MIMI BAADA YA KUSOTA FOR A YEAR AND HALF HUKU NINA DEGREE YA BBA NA MASTERS YA FINANCE PAMOJA NA WORKING EXPERIANCE YA 3YRS HAPA BONGO NA ABROAD, NILIKUWA KARIBU SANA NA MUNGU NILIKUJA PATA KAZI BILA HATA KUTUMA CV NILIKUTA NAPIGIWA TU SIM KWAMBA NIENDE KWA INTERVIEW NAKUPATA KAZI 3 WEEKS AFTER THAT. SO DONT BE DISCOURAGED TRUST AND HAVE FAITH IN GOD. WACHAWI WATU WABAYA SANA, NA HAWANA MAANA KABISA.

aisee! mkuu mbona hapo kama umezidisha chumvi!" ...........

Grand PA
 
mwaka juzi kuna siku niliitwa kwa interview dar nikakopa adi nauli.The interview was okay waliuliza simple questions wakasema majibu watatoa after 2 weeks.Kesho yake nkaanza safar ya kurud mkoan hata kabla hatujafika chalinze nikatumiwa msg'tunapenda kukutaarifu kuwa haukuchaguliwa kweny usaili....etc'...just imagine hio safar ilivokua..ni shiidaa!
 
poleni sana wahanga mimi nilikaa miezi mitatu baada ya kutoka chuo hicho kipindi sisahau yaaani unajikuta huna hata mia mfukoni,maisha yalikuwa magumu sana na mawazo mengi sana kwa kweli nilikonda sana
nashukuru Mungu kwa kazi niliyopata,ila msikate tamaa ndugu zangu mtafanuikiwa kwa wakati ukifikaa

Hongera yaani wewe miezi mitatu tu.mie miaka 4 ,then nikaja kupata sehemu fulani tena niliingia kwa gia ya kijitolea kwanza, siwezi sema ni kazi ila angalau pesa za matumizi ya kawaida sikosi.loh dunia ina majaribu hii...
 
Hata ukifika kwenye usaili unakutana na vikwazo

unaulizwa maswali ya ajabuajabu ya kukomolewa ili mradi tu ushindwe kujibu

hii ni aina nyingine ya udhalilishaji

Nilihudhuriaga oral intetview ya post ya Network Specialist. Cha ajabu niliulizwa maswali ya Programming. Mpaka nikawauliza mbona mnaniuliza maswali ya Programming na wkt post ni networking. Wakajibu,ww si IT utashindwaje kujua programming bwana. Nilichoka kwa kweli..
 
Unasailiwa na mtu ambaye sio hata wa profession yako, ndio hayo maswali ya kukomoa na yasiyoeleweka, kuna vituko sana huko basi tu...,mtu anakufanyia usaili huku anasoma maswali kwenye karatasi, as if hawezi kuformulate maswali kwa kichwa, sasa anapimaje uelewa wa anayemsaili? Kama anasoma maswali means ana marking scheme na anaexpect ujibu majibu aliyonayo kwenye karatasi...Ujinga sana.

Hiyo ya mtu wa interview panel kusoma maswali ktk karatasi ipo sana kwa oral interview za secretariat ya ajira. Inaboa kweli,mana huyo anakuwa na jibu lake/marking. Ukiende tofauti na yy inambulia marks chache.
Nilipenda ule usahili wa PCCB kwa upande wa IT. Panel ilikuwa na watu 9,ila hauhulizwi maswali na watu wote km ilivyo kwa secretariat. Na anayekuliza maswali ya technical,alikuwa anayatoa kichwani kutokana na experience yake. Kweli jamaa walijipanga vzr sana.
NB: Ingawa nadhani walikuja kuchakachua majina ya kuitwa kazini.
 
Mimi naomba niweke jina kapuni

Taasisi moja ya afya iliyoko nwanza... Inafanya kazi na serikali na kanisa katoliki

waliita watu kwenye oral interview ktk fani mbalimbali za kiutawala na usimamizi

cha kushangaza maswali yalikuwa ya aina moja kwa wasailiwa wote

just imagine unaulizwa

1. Taja wakurugenzi 5 wa miaka iliyopita wa taasisi yetu
2. Taja mawaziri 5 waliopita wa wizara ya afya
3. Jieleze kwa maneno 5

yani utadhani hyo namba 5 wameichukua freemason tehhhhhhhh

next tym kama wana watu tayari wasisumbue graduate kusafiri kwa ajili ya interview jamani... Nauli zenyewe za kusaidiwa

Duh..!! Ilimradi tu ushindwe kujibu.
 
vijana wengi tunakua na mawazo ya kujiajri suala linakuja mitaji tutapata wapi? pia kuna baadhi ya NG'OS hapa nchini ambazo zinasema zipo kwa lengo la kusaidia vijana wajikwamue na umaskini na zinapata misaada kutoka mashirika ya nje lakini kinyume chake hiyo misaada haiwafikii walengwa,mfano mzuri mimi pamoja na rafiki zangu tuliitwa na hiyo NG'O tukahudhuria semina ya wiki moja ambayo walitufundisha masuala ya customercare na jinsi ya kuandaa business plan then wakasema tuandike business plan ili tuweze kupata mkopo, kweli tuliandika business plan tukawapelekea wakaikubali kua ni nzuri na watatupa mkopo lakini cha ajabu kila tukifuatilia mara njooni kesho mara mkurugenzi kasafiri mara hatuwezi kumpa kijana fedha nyingi atazitumia vibaya!!! yaan ni usumbufu kiasi kwamba hata member wengine washaanza kukata tamaa ya kupata huo mkopo,swali tukajiuliza kama waliona hawawezi kumpa kijana kiasi kikubwa cha pesa kwanini walituita na kusema tuandike bussiness plan
 
Walidhani hamtaweza kuandaa plan... Hao hela washatafuna
 
Ndugu KUNA MAGUMU MENGI SANA KWENYE KUTAFUTAKAZI. TENA NI MBAYA SANA KAMA UNAFAMILIA MIMI NILIKUWA SINA KAZI FOR A YEAR MKEWANGU ALIKUWA ANAKAZI BAHATI NILIYO NAYO NI KWAMBA MY WIFE TUNAELEWANA NA KUHESHIMIANA SANA SIKUWAHI KUJISIKIA KUNYANYAPALIWA. ILA IS A VERY BAD EXPERIANCE IN LIFE, NI A AFADHALI BABA AWE NA KAZI.

ILA NILIKUJA GUNDUA KITU KIMOJA. SIO HALI YA KAWAIDA MTU KUKOSA KAZI FOR MORE THAN A YEAR SOMETIMES HUWA NI KAZI YA IBILISI SHETANI NA WANACHAMA WAKE. MIMI NIMEYASHUHUDIA HAYA NINAYO YASEMA KWANGU MWENYEWE NA KWA RAFIKI ZANGU ZAIDI YA WATATU.

USHAURI WANGU JITAIDI SANA KUOMBA KWA MUNGU AKUFUNGULIE MILANGO YA KAZI, PIA HUDHURIA SANA MAOMBI NA MAOMBEZI MUNGU NIMWAMINIFU SIKU ZOTE. HAKIKA UTAPATA KAZI BILA WASIWASI. MIMI BAADA YA KUSOTA FOR A YEAR AND HALF HUKU NINA DEGREE YA BBA NA MASTERS YA FINANCE PAMOJA NA WORKING EXPERIANCE YA 3YRS HAPA BONGO NA ABROAD, NILIKUWA KARIBU SANA NA MUNGU NILIKUJA PATA KAZI BILA HATA KUTUMA CV NILIKUTA NAPIGIWA TU SIM KWAMBA NIENDE KWA INTERVIEW NAKUPATA KAZI 3 WEEKS AFTER THAT. SO DONT BE DISCOURAGED TRUST AND HAVE FAITH IN GOD. WACHAWI WATU WABAYA SANA, NA HAWANA MAANA KABISA.

Kwel kabisaaa!
 
nadhani tuanzishe chama cha wasio na ajira tanzania(ccwt) kupitia hicho chama tuchague uongozi na kupitia michango midogo midogo tutaweza kufungua hata fixed account bank yoyote baadaye tukajiajiri tuko wengi jaman na ajira ngumu sana,ntasikitika sana waliosababisha haya wakirudi madarakani mwaka 2015,wameshindwa kupanga sera za kumkomboa kijana kwa miaka mingi,wanadai tujiajiri wao waajiriwa wa serikali,tunazunguka na vyeti barabarani wao wanazungusha viuno bungeni it real pain.....
 
Mwansile
Wazo zuri
Je? sis wenyewe tuna umoja?
 
Sitakuja kusahau usaili wa bugando medical centre. ..

Yan wale jamaa live walikuwa na Watu wa kuwaweka ktk administrative posts..

Eh eti mtu anakuuliza

1. taja madirector 5 wa bugando wa miaka iliyopita
2. taja mawaziri 5 wa afya wa miaka iliyopta
3. jieleze kwa maneno 5. , yan from nowhere.......
 
Lol! Bora wewe mkuu! Mimi niliomba kazi kwenye kampuni moja ya wahindi. Nkapata kama materials manager, cha ajabu kazini unaingia saa 1 Asubuhi unatoka sa 3 usiku, nkajifanya mbishi nkatoka sa 12 kesho yake manager ananipa adhabu eti nichukue fyekeo nifyeke nyasi eneo la ofisi! Kha! Nkamtukana matusi ya nguoni nkalala mbele! Juzi napata taarifa kuna dogo kampiga vichwa! Ki ukweli inauma sana, kazi ngumu mshahara kiduchuuu! Afu bado dharau kibao! Kwa macho yangu nlishuhudia mzee wa miaka 47 na ni holder wa certificate ya electrical akidekishwa ofisi na muhindi wa miaka 30! Manyanyaso makubwa, kisa amedondosha kikombe cha chai ofisin, nilijisikia kulia!

Kweli hapo mkuu bora niache,yaani nakuwa kama shule ya msingi daaa!
 
Back
Top Bottom