Magumu gani umeyapitia/unayapitia katika kutafuta kazi?

Japo bado sijapata kazi rasmi, nina ushuhuda wa kuwapa enyi watafutaji wa kazi kama mimi mja wa MUNGU. Kuna waajili wengine hapa nchini wanachangia kutufanya tuonekane kuwa tuna maisha magumu na ionekane kuwa tuna shida sana ya kupata kazi japo sio kwa wote, nakumbuka tar 1/8/2014 +255652198676 company X ilinihitaji kufika dar kwa ajili ya usaili wa Fertilizer Sales Person kwa bahati nzuri nikawaambia nipo nje ya dar kwa maana kwamba npo mkoani, nikasisitizwa kuwa nijitahidi nifike siku hiyo nikajipanga nikaamua kufunga kabiashara kangu hapa mjini ili nielekee huko dar kwa interview. Kitu Cha ajabu ni kwamba nilipoanza safari njiani walikuwa wakinipigia simu kuwa nmefika wapi, ile npo kimara tu, nikatumiwa sms kuwa wamearisha usaili wangu mpaka wiki inayofuata (nitapigiwa simu). Sikuwajibu nikasubiri mpaka niliposhuka kwenye basi ubungo, nikajaribu kuwasiliana nao lakini hawakunielewa kabisa na nikadiriki kuwaomba wanichangie japo nauli ya kurudia POLE SANA MKUU
 
Unavyoongea kuhusu hiyo laki tano utafikiri sh 100 vile. Acha nadharia wewe ,nadhani kuna watu hawajaishi ulimwengu wa kutoka chuo na kupigika vibaya mno! Ushawahi lima wewe? Unaongelea vitunguu na matikiti unajua gharama zake? Usikurupuke shirikisha ubongo toa experience ya vitu ulivyopitia sio vya kufikirika.
Mkuu kweli huyu bwana kakurupuka nisikufiche ndgu yangu mwaka huu vitunguu cjui matikiti hakuna kitu kabisa mm mwenyewe nililima vitunguu maji nimepata GREAT LOSS YA AJABU,cdhani kama mtu anishaur nitajishuhulisha na kilimo,kilimo ni hasara sana huu mwaka wa 2 nalima lakn napata hasara tuu daaa,bora niendelee kusaka ajira!
 
Habari wan JF, ni matumaini yangu wote mko poa na mnaendelea na kupigana na maisha. Kwangu bado mambo sio mazuri na naendelea kutafuta kazi, ila kuna situation hua zinanipa shida sana and nafikiri na ww mtafutaji mwenzangu hua zinakukuta, ni pale unapoamka siku kam ya J3 huna pakwenda, interview ulizokua unasikilizia umefanya but umeishia mchujo, makampuni unayoyajua yote na recruitment agencies ushapeleka CV zaidi ya mara moja, nafasi ulizoziomba utumishi hujui wataita lini, washkaji zako uliokua unachati nao kupeana moyo wakati mnatafuta now wako busy walishakula mashavu, ukimtumia mtu sms anajibu baada ya 1hr. Basi siku inakua ndeeeefu na ngumuuu
 
Ahahah kiukweli hazitofautiani.. Daahhhhh baya zaidi hao washikaji uliosoma.nao wakala shavu.. Ukiwa na matatzo hawapo tayari kukusaidia ingawa wakati mpo chuo ulikuwa mtu muhimu kwao hasa ktk masuala ya taaluma
 
Ndugu KUNA MAGUMU MENGI SANA KWENYE KUTAFUTAKAZI. TENA NI MBAYA SANA KAMA UNAFAMILIA MIMI NILIKUWA SINA KAZI FOR A YEAR MKEWANGU ALIKUWA ANAKAZI BAHATI NILIYO NAYO NI KWAMBA MY WIFE TUNAELEWANA NA KUHESHIMIANA SANA SIKUWAHI KUJISIKIA KUNYANYAPALIWA. ILA IS A VERY BAD EXPERIANCE IN LIFE, NI A AFADHALI BABA AWE NA KAZI.

ILA NILIKUJA GUNDUA KITU KIMOJA. SIO HALI YA KAWAIDA MTU KUKOSA KAZI FOR MORE THAN A YEAR SOMETIMES HUWA NI KAZI YA IBILISI SHETANI NA WANACHAMA WAKE. MIMI NIMEYASHUHUDIA HAYA NINAYO YASEMA KWANGU MWENYEWE NA KWA RAFIKI ZANGU ZAIDI YA WATATU.

USHAURI WANGU JITAIDI SANA KUOMBA KWA MUNGU AKUFUNGULIE MILANGO YA KAZI, PIA HUDHURIA SANA MAOMBI NA MAOMBEZI MUNGU NIMWAMINIFU SIKU ZOTE. HAKIKA UTAPATA KAZI BILA WASIWASI. MIMI BAADA YA KUSOTA FOR A YEAR AND HALF HUKU NINA DEGREE YA BBA NA MASTERS YA FINANCE PAMOJA NA WORKING EXPERIANCE YA 3YRS HAPA BONGO NA ABROAD, NILIKUWA KARIBU SANA NA MUNGU NILIKUJA PATA KAZI BILA HATA KUTUMA CV NILIKUTA NAPIGIWA TU SIM KWAMBA NIENDE KWA INTERVIEW NAKUPATA KAZI 3 WEEKS AFTER THAT. SO DONT BE DISCOURAGED TRUST AND HAVE FAITH IN GOD. WACHAWI WATU WABAYA SANA, NA HAWANA MAANA KABISA.

Una experience inayolingana na ya kwangu. Mimi mwenyewe Ibilisi shetani na mawakala wake walinifanya vibaya. Nimesota sana kupata kazi japokua nina masters ya masuala ya afya. Nilionana na mtumishi wa Mungu na akanifanyia maombi. Huwez amini kesho yake nikapata ajira. Nasema ile siku nimeombewa kesho yake nikapata ajira. Mtumishi aliniambia njia yangu imefungwa sana na pia nikitaka kubadili kazi ni lazma niombe vingnevyo itakua ngumu.
 
Mkuu kweli huyu bwana kakurupuka nisikufiche ndgu yangu mwaka huu vitunguu cjui matikiti hakuna kitu kabisa mm mwenyewe nililima vitunguu maji nimepata GREAT LOSS YA AJABU,cdhani kama mtu anishaur nitajishuhulisha na kilimo,kilimo ni hasara sana huu mwaka wa 2 nalima lakn napata hasara tuu daaa,bora niendelee kusaka ajira!

Sio siri mkuu majitu yanakurupuka tu na nadharia na michanganuo za karne ya 15 waliyokariri huko vyuoni. Eti tukalime (wakati lenyewe lipo ofisini lilipigiwa pande na mjomba wake). Sidhani kama wote tunayajua mazingira ya mashambani na kilimo kwa ujumla. Mboga na matunda yanaozea shambani. Hayo mahindi ndio yamerundikana kibao mabohari hata serikali inashindwa kununua. Hizo cash crops (kahawa, korosho) bei hazieleweki leo elfu moja kesho mia hamsini. Ni tabu tu aisee.
 
Ndugu yangu kazi ni ngumu cku hizi, hata mi nilisota kdg, mwombe sana Mungu kwa imani yako. Ikibidi funga, mtaani kugumu ati. Mimi niliattend interview 3 ktk ofisi nyeti nchini lakini sikuitwa ila nilijaribu sehemu ya 'kawaida' nikapata. usikate tamaa.

Nimependa signature yako mkuu.
 
Sio siri mkuu majitu yanakurupuka tu na nadharia na michanganuo za karne ya 15 waliyokariri huko vyuoni. Eti tukalime (wakati lenyewe lipo ofisini lilipigiwa pande na mjomba wake). Sidhani kama wote tunayajua mazingira ya mashambani na kilimo kwa ujumla. Mboga na matunda yanaozea shambani. Hayo mahindi ndio yamerundikana kibao mabohari hata serikali inashindwa kununua. Hizo cash crops (kahawa, korosho) bei hazieleweki leo elfu moja kesho mia hamsini. Ni tabu tu aisee.

Ila kweli asehhhh
 
Una experience inayolingana na ya kwangu. Mimi mwenyewe Ibilisi shetani na mawakala wake walinifanya vibaya. Nimesota sana kupata kazi japokua nina masters ya masuala ya afya. Nilionana na mtumishi wa Mungu na akanifanyia maombi. Huwez amini kesho yake nikapata ajira. Nasema ile siku nimeombewa kesho yake nikapata ajira. Mtumishi aliniambia njia yangu imefungwa sana na pia nikitaka kubadili kazi ni lazma niombe vingnevyo itakua ngumu.

Hahahahah kweli kabisa
 
Mkuu nina mashaka na hiyo ajira! did you apply for it before? hata interview hukufanya kabisa?

si kwamba napingana na maombi, hapana! jambo linaloniwazisha hapa ni kuhusu process za kupata kazi kwa maana lazima kuwe na interview, both oral and written, maamuzi yafanyike na management kisha upewe information za kuajiriwa na muda wa kujiandaa kabisa kuja kuingia kazini....

Sasa je? hiyo kazi uliipataje je?
 
Iko hv mkuu. Nilipomamiza shule nilihangaika kupata ajira. Nikawa nafanya mahali kama part time na sio ajira kamili. Kwa hyo sikua na security yeyote. Baada ya maombi kesho yake asbh nilipofika asbh bosi akaniambia niandike barua ili wanipatie ajira permanent. Na kweli niliandika barua na akaipitisha siku hyo hyo na nikapata ajira na kutambuliwa kama mwajiriwa rasmi mwenye haki ya kupata benefits zinazohusiana na ajira. Before nilikua napiga deiwaka tu mkuu.
 
Mkuu nina mashaka na hiyo ajira! did you apply for it before? hata interview hukufanya kabisa?

si kwamba napingana na maombi, hapana! jambo linaloniwazisha hapa ni kuhusu process za kupata kazi kwa maana lazima kuwe na interview, both oral and written, maamuzi yafanyike na management kisha upewe information za kuajiriwa na muda wa kujiandaa kabisa kuja kuingia kazini....

Sasa je? hiyo kazi uliipataje je?

Umekua muungwana umeniuliza kistaarabu sana. Wengne wangenipiga mawe
 
dah ka sio ajira ya serikalini cjui ningekuwa wapi?? Kuna mhindi mmoja aliniita kwenye interview akaniletea dharau na frustration zangu nikampiga kichwa nililala kituo cha usa siku mbili sitasahau
daaa! mkuu umenichekesha sana, kama nimekuna ulivyo mrukia ka baba ubaya.
 
Wakati wa kutafuta kazi utadharauliwa, kutukanwa, na pia utasemwa sana vibaya. Usichoke upo vitani na Mungu bado yupo upande wako. Chamsingi mtangulize Mungu kwenye kila aplication unayofanya na usichoke kutuma Maombi pindi nafas zikitoka hakika utapata kazi tu. Mimi nilipata kazi mwaka mmoja baada ya kumaliza chuo. Nilikua sitak kuajiriwa ila nilikua sina mtaji hivyo ikanisukuma kujituma kusaka ajira na hatimaye nikapata kazi na kila mwezi huwa nasave 33.3% ya mshahara wangu kwa ajil ya kuanzisha biashara yangu na kuachana na ajira na baada ya mwaka mmoja naresign kwani lengo langu litakuwa limetimia. Nawatia moyo msichoke kuaply na pia usikate tamaa. Mungu yupo
 
sanga tena we ni kamkinga kenzangu ... bro achana kabiasa na mawazo ya kichuo chuon huwezi toka chuo uanzishe NGO huo ni utindio kwanza zalisha fungua shamba ...hata kama huna mtaji sizdhani utakosa hata laki tano ukiichukua uende kijijini ndani mno kuna vilimo vya muda mfupi kama vitunguu swaumu matikiti ni miez 3 tuu una piga zaidi ya 10 m ....serious huwezi anzisha NGO una chini ya 100 m ni kupoteza muda

Mkuu unamaanisha huwezi anzisha NGO kama huna milioni 100?
 
Mimi nilikaa miezi sita bila kupata ajira, lakini ndani ya miezi hiyo sita nikawa nimebahatika kuitwa kwenye usaili kwenye taasisi ya umma, ni kazi ambayo nilikua naitaka kabisa, ila sitosahau hiyo siku, niliitwa kwenye usaili nimewahi asubuhi sana ili nisichelewe, wakati wa usaili unafika, nikatolewa nje eti sina cheti, kwamba hata nikifanya usaili sitachaguliwa, kwamba watu wa utumishi hawawezi kuajiri mtu bila cheti. Niliumia sana siku hiyo, nilikaa na stress takribani kwa wiki nzima. Ila niliendelea kumwamini Mungu.

Baada ya muda mfupi nikaitwa na NGO fulani na nikapewa kazi hata bila interview. Kama una mwamini Mungu hatakuacha uteseke.

Mnaotoka chouni sasa, msiwe na matarajio makubwa ya kupata ajira ndani ya muda mfupi, kuweni wavumilivu, na kuweni wabunifu katika kutafuta kazi. Usiwe mchaguzi sana wa kazi omba kazi yoyote ambayo unadhani unaweza kufanya. Utafanikiwa tu.
 
asante sana mkuu kwa ushauri mwanana!

hakuna mtu duniani anayetegemea mambo madogo, hata masikini huwaza kupata mali nyingi sana siu moja...

Nimejifunza kitu hapa kwako, naamini nami ujumbe wako utanisaidia mara 100 zaidi ulivyofanikiwa wewe!

Nazidi kuamini juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu... asante sana!
 
Back
Top Bottom