Magufuli: Watanikoma!

Magufuli: Watanikoma!

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
Mgombea wa urais kupitia CCM, John Pombe Magufuli amesema akichaguli kuwa rais, mafisadi watamkoma.

Source: Tanzania Daima.

================================
magufuli.jpg

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli (55), amewaahidi Watanzania kuwa atawatumikia pasipo kujali itikadi zao za kisiasa na kwamba endapo atakuwa Rais, serikali yake haitavumilia wazembe, wala rushwa na wabadhirifu.

Akizungumza katika nyakati tofauti baada ya kuchaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM kuwa mgombea wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Magufuli alisema amepokea kitendo hicho kwa unyenyekevu mkubwa na kwamba hatawaangusha waliomwamini."Wakati Rais mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi alipopewa nafasi hii mwaka 1985, alisema neno moja na naomba kumnukuu; ‘Nimehemewa'.

Wakati ule sikumwelewa sana lakini leo baada ya uchaguzi huu, nimemuelewa na nasema nimehemewa sana."Naahidi kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuunda serikali imara. Katika hili, nataka niwathibitishie kuwa katika serikali yangu wazembe na wabadhirifu hawatapata nafasi… Wazembe na wezi nitawashughulikia kwa upole sana," alisema Magufuli huku akishangiliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Uchaguzi wa kumchagua Magufuli ulifanyika juzi katika ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM uliopo Dodoma ingawa matokeo yake yalitangazwa jana.Kwa ruhusa ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, matokeo hayo ya uchaguzi huo yalitangazwa na Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Anne Makinda, aliyetangaza kuwa Magufuli alishinda kwa kupata kura 2,104 kati ya kura 2,416 zilizopigwa.Idadi hiyo ya kura ilikuwa sawa na asilimia 87 ya kura zote zilizopigwa; huku washindani wake wa karibu, Dk. Asha Rose Migiro na Amina Salum Ali wakipata kura 59 (asilimia tatu) na kura 253 (asilimia 10).

Dalili za Magufuli kupitishwa na chama hicho zilianza kuonekana mapema juzi usiku mara baada ya kubainika kwamba atashindana na Migiro na Amina ambao hawakuonekana kuwa wapinzani wagumu kwake.Wanasiasa wawili waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kumrithi Kikwete; Edward Lowassa na Bernard Membe, hawakufika katika hatua ya tatu bora kwa sababu tofauti; Lowassa, Mbunge wa Monduli, aliondolewa kwa sababu za kimaadili huku Waziri wa Mambo ya Nje, Membe, akishindwa katika ngazi ya Halmashauri Kuu (NEC).Mkutano wa NEC ulikuwa mgumu kwa sababu unaundwa na asilimia kubwa ya wafuasi wa Lowassa ambao walikuwa wamedhamiria kuzuia majina kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu pasipo jina la mtu waliyemtaka kuwemo.Ni busara za viongozi wakuu wastaafu wa chama na serikali, akiwamo Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume na Benjamin Mkapa, ndizo zilizookoa jahazi katika mkutano huo na kuwafanya wajumbe hao wakubali kura zipigwe.

Raia Tanzania linafahamu kwamba wajumbe wa NEC waliokuwa wakitaka Lowassa aingizwe kwenye tano bora walikubali kubaki ukumbini na kupiga kura baada ya kuambiwa kuwa wakiacha majina hayo matano yatapelekwa kwenye Mkutano Mkuu kulikokuwa na uwezekano wa mshindani wake mkuu, Membe, kupitishwa.Dk. Migiro kivutioWagombea wote walioshindwa na Magufuli walikubali matokeo hayo, ingawa hotuba ya Migiro ilikuwa kivutio zaidi kutokana na kujaa maneno ya busara na ya kusisimua.

Wajumbe waliokuwepo, akiwamo Kikwete, walimshangilia zaidi Migiro wakati alipotumia nukuu kutoka kwa mwanasiasa wa Marekani, Hillary Clinton, aliyoitoa baada ya kukosa urais kwa Barack Obama mwaka 2008.Katika hotuba yake, ambayo Migiro aliinukuu kwa wajumbe jana, mke huyo wa Rais Bill Clinton alisema;

"Although we were not able to shatter that highest and hardest glass ceiling this time, thanks to you it has 18 million cracks in it, and the light is shining through like never before, filling us all with the hope and the sure knowledge that the path will be a little easier next time."

Kwenye nukuu hiyo, Migiro na Hillary wanazungumzia ugumu uliopo kwa akinamama kupata nafasi za juu za uongozi katika mfumo dume uliopo, lakini akasema kwa mafanikio ambayo yeye na Amina wameyapata mwaka huu, fursa zaidi zitajitokeza kwa wengine.

Wakati akihutubia, Migiro alikuwa amesimama sambamba na mumewe, Profesa Cleophas Migiro, ambaye aliwahi kuwa mwalimu wa Magufuli Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).Samia mgombea mwenzaMkutano Mkuu huo wa CCM jana ulipitisha jina la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mwenza wa Magufuli katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.Jina la Samia lilipatikana kutoka katika Kamati Kuu ya CCM iliyokutana kwa dharura kujadili suala hilo mara baada ya Magufuli kutangazwa kuwa mgombea urais.

Ni Magufuli ndiye aliyetaja jina hilo la Samia –akianza kwa kueleza kwa kirefu namna akinamama walivyomsaidia kisiasa, akitaja jina la mwanasiasa mkongwe, Anna Abdallah, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi wakati mgombea alipoingia kwenye Baraza la Mawaziri la Rais Mkapa kwa mara ya kwanza mwaka 1995. Wakati huo, Magufuli alikuwa na umri wa miaka 35."Baada ya kutafakari sana.

Na kwa kuzingatia jinsi waasisi wetu kuanzia Baba wa Taifa, Mzee Mwinyi, Mzee Karume, Mzee Mkapa na Rais Kikwete wanavyothamini mchango wa akinamama na kwa kuzingatia CCM pia kuthamini mchango wa kinamama, nimeamua kumtangaza Samia kuwa mgombea mwenza," alisema Magufuli katika kauli iliyopokewa kwa shangwe na vifijo ukumbini.

First Lady kutoka Mbuyuni?Mke wa Magufuli, Janet, ni mwalimu kitaaluma akiwa anafundisha katika Shule ya Msingi Mbuyuni iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Kikwete, Salma, alikuwa pia mwalimu katika shule hiyo wakati mumewe alipopata madaraka ya urais.

Chanzo: Tanzania Daima
 
mkwara tu huo, jk yalimshinda

Usimfananishe JK na JPM, Angalia Hata Utendaji Wao Wakiwa Mawaziri Utaona Tofauti!!! JPM Anachukuaga Maamuzi Magumu Sana Kuliko JK, Makandarasi Wanamjua, Wezi Wa Samaki Bahari Kuu Pia Wanamjua, Matapeli Wa Viwanja Pia!!!Aliekuwa Mtendaji Mkuu Wa Tanroad (Mrema)Muulize Habari Ya Huyu Jamaa
 
TAFAKURI YA LEO:

Kunamaana mbaya sana ya CCM kuvunja makundi. Hii inamaana na mafisadi wote wanaingia kwenye mchakato na wameishahakikishiwa maslahi yao.

Kwa macho ya haraka haraka na uzembe wa kuchunguza watanzania wengi wamefikiri wamepata mkombozi wa matatizo sugu yanayoikabili serikali yao kama ufisadi rushwa na huduma mbovu za uma kwa kuwa magufuli atagombea kupita CCM.

Wamesahau CCM ni system. System iliyojaa wizi na hakuna aliye ndani mwenye uwezo wa kuibadili au kuigusa. Wamuulize Mwakyembe.

Labda tukumbushane.
Kikwete ameingia madarakani akiwa mzalendo kupindukia. watu wakiwa na matumaini ya kutosha. Yani wakati huo alikuwa waziri kwa miaka mingi tu. Mkewe alikuwa mwalimu wa shule ya msingi tu anapokea laki mbili kwa mwezi mpaka jk anaingia madarakani. Riziwani alikuwa kaajiliwa na kampuni ya Masha aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani. kiujumla alikuwa mtu mwenye maisha ya kawaida, asiye na tamaa lakini ilimchukua miezi minne tu kuwekewa kucha kali na meno makali na kufundishwa kurarua. wakaivuta familia yake kwenye dili zao wakamziba mdomo. baada ya hapo wakaanza kupiga mara Richmond mara Escrow na madini. Wakakwamisha mipango yake mizuri kama katiba mpya na kukuza democrasia. Ila JK ni mwanaume kasubutu kuwanyima kuwapa nchi moja kwa moja watesi wake.

Mnamkumbuka na Mkapa. Aliingia kama kiongozi masikini kabisa na mfuasi wa sera za mwalimu. Nae aligeuzwa kutoka kumiliki Land lover wakamshirikisha mkewe kwenye dili kubwa kubwa na kumpa hisa kwenye taasisi za kifedha. mkapa kushtuka wakampa hadi mgodi wa makaa ya mawe. Baadae Jamaa wakafanya yao. Mara Rada Epa na Bot.

Walimzidi akili na mwinyi pia. Mzalendo aliyependwa na mwalimu. Wakamuundia zengwe mkewe Mama siti. Wakamfanya ashindwe kabisa kuendelea namikakati ya kusafisha utendaji mbovu wa secta za uma na sera zake za Fagio la chuma. Watu wakafanya yao.

Tusitegemee miujiza kwa magufuli. Labda akae na familia yake sasa. Awe tayari kufunga mkewe na watoto wake wakiingizwa kwenye dili. Kama alivyofanya raisi wa korea kaskazini aliyemnyonga mjomba wake na kumtupa kwenye shimo la simba.

Kwa CCM ilivyo hakuna wakuendesha nchi kwa weredi ata kama anaweredi kiasi gani.

CCM sasa imetutangulizia kondoo mbele huku akifatwa na kundi la mbwa mwitu wenye njaa hatari. Tuchukue tahadhari!!!!
Tulishasahau kilasiku tunasema tatizo ni mfumo. Tunatakiwa tuufumue mfumo tu basi ambao ni CCM.

Kumgeuza magufuli wataanza kumchangia pesa za kampeni watamwekea na za escrow humohumo. baadae wanafanya yao kwa uhuru. Watawazungukia watoto wake na ukoo wake. kama walivyomuuzia nyumba ya uma mdogo wake ili kumkata kauli alipokuwa wizara ya ardhi.
Ikumbukwe CCM imeishavunja makundi na Mafisadi wote watakuwa wamehakikishiwa usalama namaslahi yao na sasa wanaingia kwenye kampeni kwa miguu miwili. TUMEKWISHA.
 
Msimamo wake kwenye katiba mpya ulikuwaje?

Mbona wakati Watetezi wa wananchi wakipigana na mafisadi bungeni yeye hakudiriki kuonyesha kukerwa na ufisadi, leo hii ndipo kaona ufisadi ni tabu au ni gear? Kama alinywea na kuwa mdogo kama pilitoni, leo ujasiri huo anaupata wapi ikiwa hao mafisadi wamegombana wakaamua kumtupia yeye taulo ili kukomoana. Kambi ya fisadi lowasa ndiyo imemteua, leo anasema atashughulika na mafisadi, wakati UKAWA wakipigana na ufisadi yeye alikuwa ccm kimya. Huu si unafiki na hadaa kwa Watanzania?

Miswada gandamizi imepitshwa, yeye akiwa bungeni, kama mbunge, kwa nini hakutoa angalizo kwa wana ccm wenzake ili kama walikuwa hawajui kwa kuwa wengi yalikuwa majuha, ili kuwafanya wasifanye maamuzi ya kuua nchi?

Huo uzalendo umetoka wapi leo?

Huu ni utani!
 
Usimfananishe JK na JPM, Angalia Hata Utendaji Wao Wakiwa Mawaziri Utaona Tofauti!!! JPM Anachukuaga Maamuzi Magumu Sana Kuliko JK, Makandarasi Wanamjua, Wezi Wa Samaki Bahari Kuu Pia Wanamjua, Matapeli Wa Viwanja Pia!!!Aliekuwa Mtendaji Mkuu Wa Tanroad (Mrema)Muulize Habari Ya Huyu Jamaa

Unataka kusema atakamata mafisadi wote au?
Anaweza kudeal na kina makengeza and Co.?
 
Kwangu Mm Hakuna Kiongozi Mkamilifu Duniani, So Far Ni Binadamu, Kama Kina Blatter Wamepiga Iweje Hawa Wetu, Tunachoangalia Unaafuu Wa Hali Iliyopo Na Tujitahidi Kumpa Wabunge Wa Upinzani Wengi Ili Mhimili Huu Uwe Na Nguvu Pia!!
 
Ukawa mpaka muda huu mgombea ni kitendawili lakini akili yote kwa magufuli
 
TAFAKURI YA LEO:

Kunamaana mbaya sana ya CCM kuvunja makundi. Hii inamaana na mafisadi wote wanaingia kwenye mchakato na wameishahakikishiwa maslahi yao.

Kwa macho ya haraka haraka na uzembe wa kuchunguza watanzania wengi wamefikiri wamepata mkombozi wa matatizo sugu yanayoikabili serikali yao kama ufisadi rushwa na huduma mbovu za uma kwa kuwa magufuli atagombea kupita CCM.

Wamesahau CCM ni system. System iliyojaa wizi na hakuna aliye ndani mwenye uwezo wa kuibadili au kuigusa. Wamuulize Mwakyembe.

Labda tukumbushane.
Kikwete ameingia madarakani akiwa mzalendo kupindukia. watu wakiwa na matumaini ya kutosha. Yani wakati huo alikuwa waziri kwa miaka mingi tu. Mkewe alikuwa mwalimu wa shule ya msingi tu anapokea laki mbili kwa mwezi mpaka jk anaingia madarakani. Riziwani alikuwa kaajiliwa na kampuni ya Masha aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani. kiujumla alikuwa mtu mwenye maisha ya kawaida, asiye na tamaa lakini ilimchukua miezi minne tu kuwekewa kucha kali na meno makali na kufundishwa kurarua. wakaivuta familia yake kwenye dili zao wakamziba mdomo. baada ya hapo wakaanza kupiga mara Richmond mara Escrow na madini. Wakakwamisha mipango yake mizuri kama katiba mpya na kukuza democrasia. Ila JK ni mwanaume kasubutu kuwanyima kuwapa nchi moja kwa moja watesi wake.

Mnamkumbuka na Mkapa. Aliingia kama kiongozi masikini kabisa na mfuasi wa sera za mwalimu. Nae aligeuzwa kutoka kumiliki Land lover wakamshirikisha mkewe kwenye dili kubwa kubwa na kumpa hisa kwenye taasisi za kifedha. mkapa kushtuka wakampa hadi mgodi wa makaa ya mawe. Baadae Jamaa wakafanya yao. Mara Rada Epa na Bot.

Walimzidi akili na mwinyi pia. Mzalendo aliyependwa na mwalimu. Wakamuundia zengwe mkewe Mama siti. Wakamfanya ashindwe kabisa kuendelea namikakati ya kusafisha utendaji mbovu wa secta za uma na sera zake za Fagio la chuma. Watu wakafanya yao.

Tusitegemee miujiza kwa magufuli. Labda akae na familia yake sasa. Awe tayari kufunga mkewe na watoto wake wakiingizwa kwenye dili. Kama alivyofanya raisi wa korea kaskazini aliyemnyonga mjomba wake na kumtupa kwenye shimo la simba.

Kwa CCM ilivyo hakuna wakuendesha nchi kwa weredi ata kama anaweredi kiasi gani.

CCM sasa imetutangulizia kondoo mbele huku akifatwa na kundi la mbwa mwitu wenye njaa hatari. Tuchukue tahadhari!!!!
Tulishasahau kilasiku tunasema tatizo ni mfumo. Tunatakiwa tuufumue mfumo tu basi ambao ni CCM.

Kumgeuza magufuli wataanza kumchangia pesa za kampeni watamwekea na za escrow humohumo. baadae wanafanya yao kwa uhuru. Watawazungukia watoto wake na ukoo wake. kama walivyomuuzia nyumba ya uma mdogo wake ili kumkata kauli alipokuwa wizara ya ardhi.
Ikumbukwe CCM imeishavunja makundi na Mafisadi wote watakuwa wamehakikishiwa usalama namaslahi yao na sasa wanaingia kwenye kampeni kwa miguu miwili. TUMEKWISHA.

Kaka Napenda Sana Hoja Zenye Vielelezo Kama Za Kwako, Na Ninakubali Hata Yy Anaweza Akamezwa Na System, Lakini Nimeshauri Pia Tujitahidi Kuweka Wapinzani Wengi Kwenye Bunge Lijalo, Ikiwezekana Hata Spika Atokane Na UKAWA Halafu Tuweke Hoja Mezani!! Yeye Mwenyewe Ataogopa Kuhatibiwa Serikali Yake Na Kumbuka Huyu Jamaa Ni Mpenda Sifa, Asingependa Yatokee Kama Ya Kina JK Na Kashfa Kila Kukicha
 
labda mwarubaini wako wew na familia yako. Huyo ni kondoo tu iliyotangulizwa mbele kinafiki kwani mafisadi wanakuja nyuma. Hayo ayasemayo kila mwana ccm husema.
haujui unachosema wewe nakuona kama mmoja wa watu wasio kuwa na matumini na Maisha ushauri wangu jenga maisha yako kwa kufanya kazi na si vinginevyo kwa kutegemea watawala.
 
Back
Top Bottom