Labda raisi wa WANAOTETEMEKA
Raisi wenye Tezi Du....
Magufuli Vs. Lowassa, nani zaidi katika Utekelezaji?
Wote wawili ni watekelezaji wazuri na wafuatiliaji katika maeneo walimofanya kazi! Lakini nani zaidi kwa mujibu wa rekodi zilizo wazi na zinazofahamika na siyo Majungu?
LOWASSA:
*Alipokuwa Waziri wa Ardhi, alizuia uuzwaji wa Mnazi Mmoja, iliyokwishauzwa kwa kina Baghdad; alitekeleza kwa ustadi Maagizo ya Rais Mwinyi ya kuanzisha Ujenzi wa Maghorofa Jijini Dar es Salaam na Miji Mikubwa na yasitaifishwe; kuifufua NHC na kuiwezesha ianze kutoa gawio kwa Serikali; Viwanja Elfu-20 kupunguza ulanguzi wa Viwanja; alitengeneza Sera ya Ardhi, iliyozaa Sheria ya Ardhi.
* Ofisi ya Makamu wa Rais, alisimamia kidete Mazingira na kubuni Mipango ya kuwawezesha watu wa kipato cha chini;
* Maji na Mifugo, alisimamia kikamilifu Mradi wa kuleta Maji ya Ziwa Victoria Shinyanga; aliwafukuza matapeli wa City Waters; alianzisha mipango ya Kuwawezesha Wafugaji kwa
kuwajengea Malambo/Majosho, wasichunge ovyo na kurandaranda nchi nzima. Alipoondoka, sasa mipango yote imevurugika na Wakulima na Wafugaji wanapigana na kuuana ovyo, hakuna anayejali; alitekeleza kwa dhati Ujenzi wa Sekondari za Kata na zikajengwa zaidi ya Elfu-2 kwa Miaka Miwili tu, bila ya mpango wa gharama kubwa wa Rais Kikwete wa BRN (Matokeo Makubwa sasa), aliouazima kutoka Malaysia. Alipoondoka hata Maabara za shule hizo zimeshindikana kukamilishwa, Wanafunzi wanakalia mawe Shule za Msingi, hawana Vyoo, chini ya Waziri Mkuu "muadilifu", Pinda. Lowassa alibuni mpango wa Boda Boda na Bajaj ili vyombo hivyo viruhusiwe kufanya Biashara na kutoa Ajira. Alipoondoka Boda Boda na Bajaj wanabanwa na hawafanyi tena Biashara yao kwa Uhuru mijini! Aliwachemsha sana na kuwasimamia Watendaji wa Serikali Kuu Mikoani na Wilayani na Watendaji wa Halmashauri na kazi zikawa zinafanyika, kinyume na sasa Mabilioni yanapelekewa huko, yanaliwa tu na maendeleo duni...
MAGUFULI:
- Akiwa Waziri wa Mifugo/Uvuvi, alikamata Meli ya wavuvi haramu, lakini kutokana na Rushwa ya Watendaji wa Serikali, Meli hiyo imezamishwa kupoteza ushahidi na Serikali sasa inakabiliwa na kulipa Mabilioni ya Fidia; kachoma Nyavu za Wavuvi Wadogo Wadogo, bila ya fidia au kuwapa Nyavu mbadala, huko Ziwa Victoria na Pwani ya Lindi na Mtwara, mpaka Wavuvi hao sasa wamekuwa "Malofa", bila ya kujua nini cha kufanya!
* Akiwa Waziri wa Ujenzi, kajenga Barabara, kwa fedha za Mfuko wa Barabara zinazotokana na Ushuru mkubwa tunaokamuliwa kwenye Petroli, lakini kwenye maeneo Barabara za Lami zilikopita, watu wengi wamevunjiwa Majumba yao bila ya Fidia na wengine wanaishi nje sasa! Sijui akiwa Rais itakuwaje.
* Aliwaambia Wananchi wa Kigamboni, waliokuwa wanalalamikia Huduma za Magogoni Ferry kuwa Wapige "Mbizi" kama wanaona kivuko kina karaha na ghali.
* Ameuza Nyumba zote nzuri za Seikali kwenye maeneo muhimu ya Oysterbay, Jijini Dar es Salaam, kwa bei chee na majumba mengine yaliuzwa kwa watu wasiohusika, wakiwemo watumishi wa CCM...
Nani zaidi? Tafakari, chukua hatua!
Magufuli hana tezi..du mkuu,au unaota?
Msukuma hapa kazi tu! Huyo mwingine dondosha shilingi huone atavyohaha kuisaka unaweza shangaa ndo yule robot au mwingine