Magufuli Vs. Lowassa, nani zaidi katika Utekelezaji?

hawa ndio viongozi wakuu wa kisiasa nchini.

hivi sasa ni miezi saba tangu magufuli achukue kiti, lakini baada ya miezi saba Lowasa kajitokeza, wengi waliamini labda alikuwa ameisha kabisa.

sasa kwa utendaji wa magufuli kwa miezi saba unazani Lowasa ni tishio zaidi ya 2015?

je unaonaje?
Tishio na kutokuwa tishio inategemea na utendaji wa Rais kwa kutimiza Ahadi alizotoa
 
Tatizo la Tanzania ni kwamba....
Huongozwa na MTU ambaye hakuitajika.

Amino nakwambia Lowassa ni levo ingine katika mambo ya kiuongozi na huwezi mlinganisha na Magu japo Magu ni presdaa.

Aliyoyapitia Lowasa angepitia Magu asingekumbukwa wala kufahamika na yeyote Leo hii.
 
Lowasa anamtisha nani? Wanaomtegemea wasubiri mahakama ya mafisadi ianze kazi.

Unayasema haya uku umejificha nyuma ya katiba ya ccm. Nyuma ya tume ya uchaguzi inayoongozwa na kada wa ccm. Nyuma ya polisi inayoongozwa na remot ya ccm. Nyuma ya bunge linaloilinda serikali N.k. yatafakari haya otherwise unajitekenya ili uangue kicheke
 
JK inawezekana alikuwa ana wivu kuona besti yake naye akiingia kwenye listi ya mapresdaa. Ili kwenye group lao EL asimfunike. Maana kiukweli walikuwa marafiki. Lakini urafiki wa JK ulikuwa wa kinafiki zaidi.

JK akaleta siasa za "kuvua gamba", akiwa target walio kuwa wakipigiwa kelele za ufisadi. JK alijuwa EL si fisadi lakini alinyamaza na kuendeleza politics za kiswalihina. Ufisadi wote wa kuuza nchi EL hajatokea.

JK yuko responsible kwasababu hata mimi nilimpigia kura Maghufuli badala ya Lowassa kwa kuamini ni fisadi ambaye JK anaogopa kumtimua waziwazi ili chama kisimegeke. But I was wrong.

JK pia alitaka wananchi wamkumbuke uongozi wake ndo maana akaona JPM anafaa zaidi kwasababu anamfahamu vyema(alishawahi kupindua maamuzi yake mengi tu JPM alipokuwa waziri na JK rais), JK alijuwa kuna namna mambo yatakuwa ndivyo sivyo na wananchi kulalamika zaidi, hence kumkumbuka.

However nimekaa nikafikiria, sababu kubwa ya kumpigia kura JPM badala ya Lowassa ni ufisadi. Nikasubiri ccm wamshitaki EL, wapi. Subiri wataje kashfa ambaye kiukweli amehusika yeye, hakuna.

Yani ina maana kashfa ya kuuza nyumba za serikali kwa ndugu zake, inaonyesha wazi uncle Magu ni fisadi na wala siyo EL.

Kwahiyo hapa kusema JPM ni msafi kuliko EL ni upotoshaji mkubwa kabisa.

Hivyo basi hapo ndo tofauti kubwa ya kwanza kabisa kati ya hao viongozi wawili. Pia kingine ni busara. Mzee EL ana busara sana, na pia huchaguwa maneno ya kuzungumza nk.

Watu hao lakini pia wana similarities. Yani kuna mambo wanafanana. Na hilo ni ufuatiliaji, utekelezaji na uwajibikaji.

Hizo ndo nguzo kuu za sifa za Lowassa. Sasa wale ambao hatukuwa na uhakika kuhusu EL, tukaona kuwa Maghufuli pia anaweza kufanya tu kama yeye.

Lakini tofauti ni ukosefu wa busara kwenye maamuzi hayo. Busara ikikosekana kwenye jambo lolote la msingi, basi matokeo yake ni sawa "kujipiga risasi ya mguuni" ukiwa kwenye safari inayoitegemea miguu hiyo.

EL pia ni msikilizaji. Hiyo sifa rais wetu wa sasa hana. Nina imani kuna anaowasikiliza wachache, ambao hao kwake hawana makosa.

Pamoja na sifa ya ujasiri na uchukuaji wa maamuzi magumu alizonazo EL, bado ni mtu mwenye UPENDO na HURUMA.

Rais anaonekana ana ujasiri. Wengi wanapiga wanasema ni uoga. Mimi ninaamini ana ujasiri, lakini hana upendo wala huruma hata chembe.

Binafsi ninaamini rais lazima awe na empathy, yani uwezo wa kujiweka kwenye nafasi ya mtu mwingine na kuona anayopitia. Mtu wa namna hawezi kukosa huruma na upendo, ingredients ambazo ni muhimu sana kwenye jamii ya kitanzania. Aliposhindwa kujiweka kwenye nafasi ya wafiwa, aliamuru rambi rambi zisikabidhiwe kwa wafiwa/waathirika. Hapo ndipo utaona umuhimu wa empathy kwa kiongozi mkuu wa nchi.

Pia EL siyo mtu wa visasi wala vinyongo. Kwa kuwa nilikuwa nimeshamchukia sana kwasababu za uongo kuwa ni fisadi namba moja nchini, nilishindwa kuamini kama hana hizo characteristics.

Nikawa nadhani anajifanyisha tu pale ambapo akitukanwa wala hajibu. Na wanaomuita fisadi hawamyimi usingizi. Yani wala hakutumia nguvu kubwa kupingana na hao wanaomuita fisadi na matusi mengine.

Binafsi ninaamini kuwa JPM amepiga marufuku siasa kwasababu ya Lowassa. Kiukweli, wengi wangeona makosa makubwa tuliyofanya.

Hapo mwanzoni nilikubaliana na JPM kuwa serikali inatakiwa ipewe muda wa kufanya kazi na kutekeleza ahadi zake badala ya kuendeleza siasa. However sasa nimegunduwa kuwa sababu kubwa ni yeye binafsi. Wasiwasi kuwa wananchi watagunduwa mapema makosa waliyoyafanya.

Kama Mungu akimpa uzima, na afya ikawa inaruhusu, nina imani kuwa Lowassa bado ana nafasi ya kuongoza Taifa letu. Pengine akayafanya yale mazuri yaliyoko kwenye uongozi huu wa sasa, na kuachana na negativity zote za utawala huu.

La mwisho kabisa, ni uzalendo wa kweli.
 
Back
Top Bottom