Magufuli usikubali kupiga ngoma tena

Magufuli usikubali kupiga ngoma tena

siyo kila muda ni kuwaza kazi tu. Muda mwingine unafanya vitu laini muda mwingine unafanya vitu vigumu.
 
Yuko na gwiji la usanii JK lazima apige ngoma kufumisha usanii
 
Hivi kuna tofauti kati ya ngoma, tumba na drums, hebu tusaidiane kufahamishana. Maana mara zote nimemuona Makufuli akipiga tumba, zile zinapigwa na viganja vya mikono, na sio zile zipigwazo na vijiti au mdundo.
 
Chee...eti afanye nn kwenye ujenzi..wakati yeye ndo waliouziana nyumba za serikali kwa bei chee kabisa.....!!!!
 
Magufuli na Jakaya ni wale wale. Tena Magufuli atakuwa dhaifu mara mbili kwa sababu haujui System na hakijui chama...
 
Sikubaliani kabisa na maoni hayo. Mtu kama ana vipawa vingi, kwa nini asivitumie tu. Mtu kama ana starehe mbalimbali anazozipenda, kwa nini asizifanya wakati ambapo haiingilii shughuli zake nyingine. Kwa nini ni lazima awe mtu wa upande mmoja tu. Ni vizuri kama akiwa well rounded person. Hiyo itamfanya aelewe zaidi shughuli mbalimbali za wananchi wake. Kutokutilia maanani mambo hayo ndiko kulikopelekea waziri fulani kufuta michezo mashuleni.
Lazima Watanzania tuangalia nyanja mbalimbali za maisha ya mtu na siyo kuwaweka watu katika maboksi madogo. Je, unafahamu kwamba viongozi wengi duniani huwa wanajishughulisha na sanaa fulani fulani kila mara.

Kipawa kinaonekana baada ya kupachikwa kwenye uwania urais?..? acha aambiwe..!
 
mwisho wa ngoma ni 25october!!

wakiweza kukupigisha ngoma leo hawatashindwa kukuingiza kwenye chaka la ufisadi kesho, sio wema hao. JK alikuwa mpenda dansi, hata alivyokuwa waziri alikuwa akionekana Msondo na Sikinde kama sehemu ya hobby yake. Magufuli akiwa mbunge na waziri hakuwahi kuonekana kwenye ukumbi wowote wa musiki wala kununua CDs za wasanii, iweje leo ghafla aibuke anapiga ngoma baada ya tukio la uteuzi. Hii sio tabia njema kwa mtu anayetaka kuwa rais wa nchi, rais wa nchi anapaswa awe anatabirika na awe na hobby zinazofahamika kwa wananchi. Matatizo ya wa wananchi sio kupiga ngoma wala sanaa, bali maji, umaskini, rushwa, barabara, foleni ndefu, kupanda kwa gharama za maisha, hospitali duni na elimu yenye mashaka. Magufuli kwa sasa anapaswa kutumia kila sekunde moja aliyonayo kuwaelezea wananchi chimbuko la kero hizi na namna atakavyotofautiana na Kikwete katika kuzitatua kero hizi za wananchi na sio kupiga ngoma mbele yao.
 
JK ndiyo kampeleka huko. Nasikia weeke end hii amepanga kumpeleka saloon kupiga scrub. Then duka la nguo.
 
Exactly. Napenda watu wanaoonesha kujishughulisha na sanaa mbalimbali licha ya ya vipawa vingine walivyo navyo. Niseme tu kwamba muziki hasa unahusishwa sana na creativity. Katika nchi nyingine hapa duniani, stadi za muziki za kiongozi zinachukuliwa kama ni asset. Hebu angalia hapa: Obama, Clinton, nk.
5 Most Musical Presidents: From Barack Obama to Thomas Jefferson | Billboard

Mkuu umesahau ktk ule uzinduzi wa barabara za jimbo la Ubungo,mdee na mnyika walikuwa wanacheza gitaa au??? Wenyewe ndio wa kwanza kuimba jembe...jembe...jembee.
 
Aisee nape nnauye nae kama diblo dibala na gitaa halafu dancer mkuu wa kaya na vanessa
 
Back
Top Bottom