Magufuli usikubali kupiga ngoma tena

Magufuli usikubali kupiga ngoma tena

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,255
Reaction score
16,185
WAtanzania tunakujua kwa uhodari wako kwenye ujenzi sio kwenye usanii, achana na kona hizo watu watakuona umeshaanza kuharibiwa. Baki kwenye ofeneo lako lililokufanya uwe maarufu mchini. Watu wanataka kusikia utafanya nini migogoro ya ardhi, maeneo ya wazi yaliyoporwa, barabarà zisizo na viwango, ujenzi holela mijini, foleni mijini, ujenzi wa barabara na mabwawa vijijini na reli, n.k. kupiga ngoma kunakupunguzia sifa, tunakuona kama ze comed usiye serious na unachokitafuta. Jaribu kuwa wewe kama tunavyokufahamu wananchi
 
Sikubaliani kabisa na maoni hayo. Mtu kama ana vipawa vingi, kwa nini asivitumie tu. Mtu kama ana starehe mbalimbali anazozipenda, kwa nini asizifanya wakati ambapo haiingilii shughuli zake nyingine. Kwa nini ni lazima awe mtu wa upande mmoja tu. Ni vizuri kama akiwa well rounded person. Hiyo itamfanya aelewe zaidi shughuli mbalimbali za wananchi wake. Kutokutilia maanani mambo hayo ndiko kulikopelekea waziri fulani kufuta michezo mashuleni.
Lazima Watanzania tuangalia nyanja mbalimbali za maisha ya mtu na siyo kuwaweka watu katika maboksi madogo. Je, unafahamu kwamba viongozi wengi duniani huwa wanajishughulisha na sanaa fulani fulani kila mara.
 
kwahiyo hicho kipawa cha kupiga ngoma kimezuka mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais? Kilikuwa wapi wakati wote akiwa mbunge na waziri maana wasanii walikuwepo lakini hakuwahi kujihusisha nao wala kuonekana akipiga ngoma katika maisha yake ya uwaziri ingawa wasanii walikuwepo na ngoma zilikuwepo pia.
 
Mchizi alikua anapiga ngoma kitambo tuu.. sema media zilikua hazimpi nafasi sana, by the way alikua waziri wa ujenzi na sio wa michezo.
 
Hata kama ni kweli anahicho kipawa ila c wakati muafaka wa kukionesha kwan kutokana na matatizo tuliyonayo tanzania tunahitaji kiongozi ambae ataonesha kipaji kimoja tu cha kutatua kero zilizoshindwa kutatuliwa na watawala walotangulia ili tuweze kukomboa kizaz chetu na vijavyo pia coz Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa gharama kubwa za umeme duniani ilihali nishat tunayo wenyewe.hatuna viwanda, mitaala mibovu, mahospitalini hakuna madawa, shughuli zipo lkn hakuna ajira.utulivu upo lkn hakuna amani.tunahitaji mtu ambae atleast ataonesha umahir kwenye kukabiriana na hayo
 
...itaanzishwa taasisi ya wapigangoma Lowassa akishaapishwa mwenyekiti magufuli kuenzi sanaa zake....
 
kwahiyo hicho kipawa cha kupiga ngoma kimezuka mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais? Kilikuwa wapi wakati wote akiwa mbunge na waziri maana wasanii walikuwepo lakini hakuwahi kujihusisha nao wala kuonekana akipiga ngoma katika maisha yake ya uwaziri ingawa wasanii walikuwepo na ngoma zilikuwepo pia.
Mkuu umesahau ktk ule uzinduzi wa barabara za jimbo la Ubungo,mdee na mnyika walikuwa wanacheza gitaa au??? Wenyewe ndio wa kwanza kuimba jembe...jembe...jembee.
 
Daah! Nimecheka Kweli...Eti "Nini Ngoma,ngoja Fisi Kwenye Mikutano..." Ccm Shida!
 
pombe jazzband ndiyo itatumbuiza lowassa akiapishwa mcheza show akiwa kinana na nape jitaa jk
 
kwahiyo hicho kipawa cha kupiga ngoma kimezuka mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais? Kilikuwa wapi wakati wote akiwa mbunge na waziri maana wasanii walikuwepo lakini hakuwahi kujihusisha nao wala kuonekana akipiga ngoma katika maisha yake ya uwaziri ingawa wasanii walikuwepo na ngoma zilikuwepo pia.

Una uhakika kaanza kupiga ngoma baada ya uteuzi? Ndugu fuatilia siasa siyo kuja huku na kupiga porojo zako
 
Mchizi alikua anapiga ngoma kitambo tuu.. sema media zilikua hazimpi nafasi sana, by the way alikua waziri wa ujenzi na sio wa michezo.

Sasa hivi ndio kawa waziri wa michezo ghafla!
 
Sioni tatizo hapa..apige tu ngoma...na marimba ikiwezekana
 
huyu jamaa hana kabisa sifa ya urais, bora hata Nape au DC wa Kinondoni.
 
Back
Top Bottom