Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,346
- 9,881
Hatuwezi chaguliwa rais na familia ya kikwete
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.
Dk Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa CCM ni lazima na upo pale pale.
Alisema ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi. Alisema watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na kukimbilia vyama vingine vya upinzani.
Aliwataka wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya kampeni za kisayansi. Aidha, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.
Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi, lakini wataumbuka mapema.
Akizungumza na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado wanakipenda Chama.
"Ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana, watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani," alisema. Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.
"Hako ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao safi. "Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.
Hata ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao," alisema.
Alisema iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu, asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atomize matarajio yao. Dk Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.
Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama. Dk Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.
Alisema anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya utendaji kwa maendeleo ya taifa. "Nilichaguliwa na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale walionichagua waliwakishia Watanzania wote.
Niwahakikishie kuwa mwaka huu, tutashinda zaidi," alisema. Aliwataka wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si maneno matamu bila vitendo.
"Chama nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu, shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo," alisema.
Chanzo:Habari Leo
Labda waende kukodi mapolisi wote kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Hizi tafiti za kupikwa ni za ajabu sana. CCM haiwezi kushinda Musoma na Mwanza, hiyo najua for a fact.
Usijiaminishe kiasi hicho.
Kichapo kikianza nadhani we utakuwa wa kwanza kununua Pijo!
Tusiombee balaa hapa Tz.
Wananchi ni Dhaifu mno.
Wengi wa wanaojifanya Wapigania Haki ni MAJIZI TU.
Ule Msafara wa Juzi wa Lowasa Wananchi wameibiwa Ovyo na Vibaka wa Ukawa.
I assume kwa sasa upo nje ya nchi hauishi TZ...ndugu huu mhemko uliopo hauelezeki coz people are tired of this madness of CCM.
Binafsi pia sipendi machafuko but kwa hali ninayoiona, sijui!
Hata katika waovu kuna afadhari
mi nahisi kuna kundi kubwa weng tumelisahau, ukawa itaweza kupata ushindi endapo itaweza kuhamasisha wanawake kuwapgia kura,tukumbuke wanawake ni wengi na wengi wamehamasika kupigia ccm kutokana na kuwa empowered kwa mwanamke mwenzao kupendekezwa kuwa makamu wa rais.ukiangalia umoja wa wanawake chadema na ukawa kwa ujumla haiko so powerfl kuliko ccm..hata ukiangalia chadema kiongozi wao halima mdee hana ushawish mkubwa tz zaid ya viongoz wa ccm ambao weng wao ni wakina mama watu wazima wenye ushawish mkubwa esp kwenye mashina...kwa hyo m bado naipa nafasi kubwa ccm....tho anythng can happen...
Mi natokea kanda ya ziwa, labda kama unasema kanda ya ziwa ya Marekani
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.
Dk Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa CCM ni lazima na upo pale pale.
Alisema ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi. Alisema watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na kukimbilia vyama vingine vya upinzani.
Aliwataka wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya kampeni za kisayansi. Aidha, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.
Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi, lakini wataumbuka mapema.
Akizungumza na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado wanakipenda Chama.
Ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana, watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani, alisema. Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.
Hako ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao safi. Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.
Hata ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao, alisema.
Alisema iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu, asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atomize matarajio yao. Dk Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.
Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama. Dk Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.
Alisema anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya utendaji kwa maendeleo ya taifa. Nilichaguliwa na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale walionichagua waliwakishia Watanzania wote.
Niwahakikishie kuwa mwaka huu, tutashinda zaidi, alisema. Aliwataka wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si maneno matamu bila vitendo.
Chama nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu, shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo, alisema.
Chanzo: Habari Leo
Kwa hio wewe binafsi uko tayari Kufa kutetea haki yako ya kidemokrasi?
Hilo ndio tunaloomba Takriban Watanzania Wote.
Lkn Ccm wana laana. Hawatokubali Kutoka ikulu kimya kimya.
Tusipochunga TZ hali itakuwa mbaya kuliko Rwanda na Syria.
Mm hapa Rais wangu magufuli
Siko tayari kufa...labda kuua!
Mi natokea kanda ya ziwa, labda kama unasema kanda ya ziwa ya Marekani
Nina mashaka makubwa kama Geita atapata hata watu hamsini elfu hasa baada ya mafuriko ya jana.Geita ukiizungunzia CCM unataka upigwe bure ingawaje kuna sintofahamu mgombea wa CHADEMA alieshinda kura za maoni hawamtaki wanasema ni pandikizi la CCM.Katika tafiti zote zilizopita ilionekana Lowassa anaongoza na Dr Slaa anamfuata kwa karibu. Maghufuli hata kwenye tano bora alikuwa haonekani, sasa imani ya kushinda inatoka wapi?
Baada ya Lowassa kuchukua fomu ya Ukawa Maghufuli akapotea hata kwenye media na mikutano yake huko Mtwara ilikuwa kama ya mgombea udiwani. Jeuri ya ushindi inatoka wapi?
Pamoja na kitengo kupenyeza lupia kwa Ukawa kwa lengo la kuvuruga bado Ukawa wamebaki wamoja na wanasonga mbele. Majigambo yanatoka wapi?
Sina hakika kama Maghufuri anaweza kupata kura laki moja mikoa ya Arusha na Manyara. Lakini je Lowassa hatakomba kura za kutosha Geita? Hilo linahitaji miwani kuliona?
Ccm inabomoka kila siku, wanachama wanakimbia kwa maelfu. Wanategemea goli la mkono! Goli la mkono wakati unachezwa nusu uwanja?