Uchaguzi wa mwaka huu unaonesha kuwa CCM itashinda kwa kishindo. Hii ni kutokana na uadilifu wa mgombea wao John Pombe Magufuli na kukubalika kwa 100% nje na ndani ya Nchi.
Ushindi huu wa Kishindo utapelekea Chadema kudhani kuwa CCM imeiba kura ambako kutaweza kuleta vurugu Nchini.
Hivyo Naomba kwa vyama vyote kuwa wapole na kupokea Matokeo kwa hali yoyote ile.
Kwani dalili zinaonyesha Baada ya mgombea wa Chadema (UKAWA) kusema siku ya Uchaguzi wanaume woote walinde kura zao katika vituo vya kupigia kura na wanawake warudi Nyumbani. Hii inadhihirisha kuwa wafuasi wa Chadema watajikusanya kwa Makundi kwenye vituo vya kupiga Kura ili walinde kura zao. Hii inawezekana ikaatarisha maisha yao.
Mimi nawaomba watanzania msidanganywe na Wanasiasa kwani unaweza ukapoteza maisha kwa kudanganyana. Wao watakuwa wametulia kimya Nje ya Nchi/hapahapa Tz wanasikilizia kwenye vyombo vya Habari jinsi mauwaji ya vijana wanaodanganywa kuna Madiliko wakat yanatokea.
Ndugu zangu Boda boda nawaomba kwa upendo wangu woote kwenu, mara baada ya kupiga kura yako Ondoka uende Nyumbani maana wanaoweza kuleta vurugu hasa ni Nyie vijana wa Mtaani (bodaboda)
Tusidanganyane kwa kigezo cha Siasa, na tukapoteza maisha yetu... ni hayo tu.