Magufuli: Subirini ushindi wa Tsunami

Magufuli: Subirini ushindi wa Tsunami

Naiomba serikali ianze kuangalia watafanyaje siku ya kumwapisha Magufuli sababu uwanja wa Taifa hautatosha kwa watu kujaa.Nashauri magari yashushe tu watu na kuondoka yakapaki mwembe yanga sababu umati utafurika ndani na nje kwenye maviwanja yote ya ndani na nje ya eneo la uwanja wa taifa hadi chuo cha ualimu mpaka shule ya Wayemeni.
Nashauri tv za nje zianze kuandaliwa ili watakao kuwa wamefurika hadi kule mataa ya DSA WAONE
 
Naiomba serikali ianze kuangalia watafanyaje siku ya kumwapisha Magufuli sababu uwanja wa Taifa hautatosha kwa watu kujaa.Nashauri magari yashushe tu watu na kuondoka yakapaki mwembe yanga sababu umati utafurika ndani na nje kwenye maviwanja yote ya ndani na nje ya eneo la uwanja wa taifa hadi chuo cha ualimu mpaka shule ya Wayemeni.
Nashauri tv za nje zianze kuandaliwa ili watakao kuwa wamefurika hadi kule mataa ya DSA WAONE

Dreams are valid.Keep dreaming.
 
mgombea urais kwa tiketi ya ccm, dk john magufuli, amewahakikishia wana-ccm na watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.

Dk magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani mtwara juzi alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa ccm ni lazima na upo pale pale.

Alisema ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama na kwamba watu hao wameiacha ccm ikiwa safi na salama zaidi. Alisema watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa ccm ambapo chama kiliwakata na kukimbilia vyama vingine vya upinzani.

Aliwataka wana-ccm wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya kampeni za kisayansi. Aidha, mbunge wa iramba magharibi, mwigulu nchemba alisema ni kazi rahisi kumnadi dk magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.

Mwigulu, ambaye pia ni naibu waziri wa fedha, alisema walioshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi, lakini wataumbuka mapema.

Akizungumza na mamia ya wana-ccm waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mgombea na kumdhamini, dk magufuli aliwataka makada hao na wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa watanzania walio wengi bado wanakipenda chama.

“ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa tsunami, watapiga kelele sana, watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa ccm ni lazima. Ni lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani,” alisema. Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, ccm ina kundi moja tu la ushindi.

“hako ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao safi. “lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama ccm.

Hata ukiangalia tangu enzi za baba wa taifa mwalimu julius nyerere wapo waliotoka wako akina kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao,” alisema.

Alisema iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu, asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atomize matarajio yao. Dk magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.

Aliwataka wana-ccm wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda chama. Dk magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya ccm, alisema alikuwa mbunge katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.

Alisema anaifahamu vizuri mtwara, tanzania, ccm na kero za watanzania anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya utendaji kwa maendeleo ya taifa. “nilichaguliwa na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale walionichagua waliwakishia watanzania wote.

Niwahakikishie kuwa mwaka huu, tutashinda zaidi,” alisema. Aliwataka wana-ccm katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si maneno matamu bila vitendo.

“chama nakifahamu, shida za wana-ccm nazifahamu, matarajio yao nayafahamu, shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo,” alisema.

chanzo:habari leo


huyu ndio rais wetu tunaemuhitaji kwa mabadiliko bora ya tanzania na sio bora mabadiliko
mchapakazi, muadilifu ,mfuatiliaji
 
Najiuliza ye Magufuli amejuaje kama atapata ushindi wa tsunami. Au goli la mkono limeshaanza implementation?
Au kashapewa uhakika tayari kuwa miundo mbinu inawekwa in place ili tsunami itokee?
Bado najiuliza mazee. Mkipata majibu na nyie naomba mnipe
 
Uchaguzi wa mwaka huu unaonesha kuwa CCM itashinda kwa kishindo. Hii ni kutokana na uadilifu wa mgombea wao John Pombe Magufuli na kukubalika kwa 100% nje na ndani ya Nchi.
Ushindi huu wa Kishindo utapelekea Chadema kudhani kuwa CCM imeiba kura ambako kutaweza kuleta vurugu Nchini.
Hivyo Naomba kwa vyama vyote kuwa wapole na kupokea Matokeo kwa hali yoyote ile.
Kwani dalili zinaonyesha Baada ya mgombea wa Chadema (UKAWA) kusema siku ya Uchaguzi wanaume woote walinde kura zao katika vituo vya kupigia kura na wanawake warudi Nyumbani. Hii inadhihirisha kuwa wafuasi wa Chadema watajikusanya kwa Makundi kwenye vituo vya kupiga Kura ili walinde kura zao. Hii inawezekana ikaatarisha maisha yao.
Mimi nawaomba watanzania msidanganywe na Wanasiasa kwani unaweza ukapoteza maisha kwa kudanganyana. Wao watakuwa wametulia kimya Nje ya Nchi/hapahapa Tz wanasikilizia kwenye vyombo vya Habari jinsi mauwaji ya vijana wanaodanganywa kuna Madiliko wakat yanatokea.
Ndugu zangu Boda boda nawaomba kwa upendo wangu woote kwenu, mara baada ya kupiga kura yako Ondoka uende Nyumbani maana wanaoweza kuleta vurugu hasa ni Nyie vijana wa Mtaani (bodaboda)

Tusidanganyane kwa kigezo cha Siasa, na tukapoteza maisha yetu... ni hayo tu.
 
huyo John Walker baada ya october 25 ataamia kwenye Viroba
 
Magufuli vijana tunakutegemea sana,bodaboda nao wamesema kule kwa mzee wanapiga dili tu,wewe ndiye haswa chaguo la wote.
 
Back
Top Bottom