Magufuli sasa kufuta ibara ya 46 (3) ya katiba

Magufuli sasa kufuta ibara ya 46 (3) ya katiba

Kimsingi kama ikifuatwa itaanza kufanya kazi tarehe itakayokuwa imesainiwa. Haitaweza kutumika dhidi ya rais/marais wastaafu sana itambana yeye.
 
Hii ni njozi ya mchana TENA kweupeee na kwa tz yetu haitawezekana labda vizazi vyetu.
Sisi tuwaandalie MAZINGIRA!
 
Mimi ningependa aanze na Ibara ya kuundwa kwa baraza la mawaziri. Angeondoa tu hii Ibara ya kuunda baraza la mawaziri badala yake makatibu wakuu ndio hao hao wafanye vikao vya baraza la mawaziri.

Siku akiondoa tu kipengele hicho njoo uchukue kadi yangu ya CUF tafadhali
 
Naisubiri kwa hamu hiyo,akiongeza na tume huru ya uchaguzi pamoja na kuweza kupinga matokeo ya urais nitamuunga mkono rasmi.
 
Haya yakiwa ya kweli nitamshukuru Mungu kwa namna ya pekee sana. Hata hivyo, chini ya CCM, hili linaweza kubakia kuwa ndoto (hasa kwa sababu ya wingi).

Natamani maraisi wasiwe na kinga; wawe wanaehitakiwa na wakikutwa na hatia wafilisiwe na kuachwa na vile walivyokuwa navyo walipoingia madarakani.

Hapo ndipo nitakaposema JPJM hoyee!
 
Kamwe Hilo haliwezi kutokea, na likitokea nahamia aliko Magufuli
 
Wamweke wao afu awageuke?? Thubutu yake, anze na mkapa na jk
 
Na ibara hiyo hiyo iboreshwe itamke kwamba ni marufuku kwa 'mswahili' kugombea urais
 
Can't work out.....won't work anymore. No one can get the job well done.waiting .....to no avail.
 
Of course najua kuwa JPJM ni jasiri sana lakini hilo haliwezi kabisa. Akitaka tuamini kuwa analiweza ashughulikie Tegeta Escrow Account hasa zile hela zilizotolewa kwenye benki ya Stanbic. Better still, arejeshe rasimu ya warioba kwenye BMK jipya na dogo sana (watu 70 wanatosha) na lisichukue zaidi ya mwezi mmoja kutuletea katiba ya wananchi.

Ndipo nitakaposema: JPJM hoyee; na Mungu ashukuriwe.
 
Kwakweli Dr. JPM hatabiriki lakini kwa swala la kuondoa hicho kifungu hana ubavuhuo na akifanya hivyo nitajua anajiamini 100%.
 
Hilo hatafanya, ila anaweza revise katiba pendekezwa na kuiadopt ya warioba kwa Kiasi Kubwa sana
 
Back
Top Bottom