Magufuli sasa kufuta ibara ya 46 (3) ya katiba

Magufuli sasa kufuta ibara ya 46 (3) ya katiba

Shondola

Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
95
Reaction score
58
Chanzo cha ndani Ikulu kimetoa habari kwamba mpaka sasa kazi zinazofanywa na Magufuli si mageni hata kidogo.

Kws mujibu wa chanzo hiki ni kwamba mafile yaliyoko mezani yalipelekwa siku nyingi sana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dr. Hoseah ila Serikali iliyokuwa ilipuuzia na kuyaweka kando.

Hivyo kwa mujibu wa chanzo hiki Dr. Hoseah anasemekana kufanya kazi zake nyingi kwa ustadi mkubwa ila amekuwa akipuuzwa.

Kwa mujibu wa chanzo hiki Dr. John Joseph Magufuli ameamua sasa muda si mrefu kukutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano hasa akitaka Bunge lake lijalo lishughulike mapema sana kurekebisha Ibara ya 46(3) ambayo imeweka kinga dhidi ya kutoshtakiwa Rais aliyemaliza muda wake kwa kosa lolote.

Chanzo hicho kinasema Magufuli anataka Ibara hiyo ifutwe na kimsingi yeye anataka mtu aliwahi kuwa Rais na kulisababishia Taifa hasara aburuzwe Mahakamani........
 
duh km itakuwa kweli!! atakuwa amefanya jambo moja zuri sana. Mungu amsimamie katika hili. Mungu ibariki tanganyika
 
That will be better, there wont be any more figisufigisu
 
Mimi ningependa aanze na Ibara ya kuundwa kwa baraza la mawaziri. Angeondoa tu hii Ibara ya kuunda baraza la mawaziri badala yake makatibu wakuu ndio hao hao wafanye vikao vya baraza la mawaziri.
 
Naomba iwe kweli na hicho kifungu kitolewe.

Ila kwa ufahamu wangu, mtu aliyetenda kosa jana hawez hukumiwa kwa sheria iliyoundwa leo..
Ila ni good move itawanyoosha wanafuata baada yake
 
Hahahaha!
My friend SHONDOLA, you are a great joker.
Please, don't make us happy.
Awaambie basi SMZ watoe matokeo ya uchaguzi pia kama kweli anachokifua hicho.
Shondala wacha kututania asubuhi hii ya Saturday!
Anyway, weekend njema ndugu yangu Shondola!
 
Nadhani ni njozi njema ulyoota. He will never do that. Angeamuru tu kuwa bunge hili likae na kuchagua wabunge wa BMK wasio zidi 29 tu watutengenezee katiba mpya. Asiwepo Makondakta tuu. Tuwe na katiba mpya ilotokana na hadidhu zile za Warioba.
Ataonekana kuwa katumwa na Mungu na atajiandikia historia Tz. Asijifunge mwenyewe
 
Hiyo sheria ingewekwa kabla Mkwere hajamaliza muda wake ingesaidia sana.
 
Back
Top Bottom