Magufuli: Nitaendelea kutumbua majizi 2020

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
1577949620089.png
Aidha, alitaja miradi hiyo kuwa ni ununuzi wa ndege, kujenga reli na elimu bure, huku akitaka Watanzania kudumisha amani na upendo ili uwe mwaka wa maendeleo na ustawi kwa taifa.

Kwa mujibu wa salamu za Mwaka Mpya kwa Watanzania zilizopo kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Magufuli alisema, serikali itaendelea kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma ili iendelee kutekeleza miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.

Alitoa salamu hizo jana, wakati akiagana na maofisa na askari wa wanyamapori na Hifadhi ya Misitu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ambako alitembelea na kujionea vivutio vya utalii pamoja na wananchi wa Nyabugera na Muganza aliowasalimu wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake Chato.

“Nchi hii ilikuwa inaliwa sana na majizi na mpaka sasa bado wapo, namwomba Mwenyezi Mungu aendelee kunipa uhai ili katika mwaka 2020 niendelee kuwatumbua majizi wote na fedha tutakazopata tuzipeleke kwenye miradi ya maendeleo kama ambavyo tumenunua ndege 11, tunajenga reli (standard gauge), tunatoa elimu bure na mengine mengi,” alisema.

Aidha, Rais amemwonya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke, kwa matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na halmashauri hiyo na ametaka dosari hizo zirekebishwe mara moja.

“Nataka ujirekebishe, wananchi hawa wanateseka sana,” alisisitiza.
Baada ya kuvuka Ziwa Victoria kwa kivuko cha MV Chato, Rais Magufuli alikutana na wananchi wa Kasenda na kuelezea kutoridhishwa kwake na ukusanyaji wa mapato ya soko la dagaa na samaki la Kasenda baada ya kuelezwa kuwa makusanyo ya mapato ya soko hilo ni Sh. 500,000 kwa siku licha kuwa soko kubwa la pili kwa kuuza dagaa katika ukanda wa Ziwa Victoria.

Rais alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato, kufuatilia ukusanyaji wa mapato katika soko hilo na kuchukua hatua za kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato itakayobainika ili Halmashauri ya Wilaya ya Chato ipate fedha zitakazosaidia kutatua kero za wananchi ikiwamo kuboresha mazingira ya soko hilo na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyabugera ambayo alichangia Sh. milioni 5.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais amemwagiza Mkurugenzi wa Chato Mwaiteleke kutangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya Kasenda hadi Muganza yenye urefu wa kilometa 2.2, ili ijengwe kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi, na kwamba serikali itatoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo.

Aidha, Rais aliwasalimu wananchi wa Muganza, ambapo amewapongeza kwa maendeleo yaliyopatikana katika eneo hilo na amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ili iendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli alipokea salamu za heri ya Mwaka Mpya wa 2020 kutoka kwa wananchi, viongozi mbalimbali wakiwamo marais wastaafu, maaskofu na masheikh ambao wamempongeza kwa kazi nzuri ya kuongoza nchi kwa mafanikio makubwa na wamemwelezea matarajio yao ya kufanikiwa zaidi katika mwaka ujao.

“Rais wangu, Dk. Magufuli, Bwana Yesu Asifiwe. Ninakupa hongera sana kwa wajibu mzito ulionao. Kwa neema ya Mungu tumejaaliwa kufikia siku ya mwisho kwa mwaka huu wa 2019. Mimi nakupongeza kwa jitihada zako nyingi za kuleta maendeleo kwa nchi yetu. Ninakuombea na kukutakia Mwaka Mpya 2020 wa heri na mafanikio makubwa. Uso wa Bwana uende nawe popote utakapokuwa, alisema Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo.

Kabla ya kuondoka katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Rais Magufuli alimshukuru Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk. Allan Kijazi, maofisa na askari wote wa hifadhi hiyo kwa mapokezi mazuri na juhudi kubwa zilizowezesha hifadhi hiyo kuvutia.
Aidha, aliwahakikishia kuwa pamoja na kutoa Sh. bilioni 2 za ujenzi wa kivuko cha kwenda hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo, serikali itatoa Sh. milioni 200 za kuboresha barabara za hifadhi hiyo.

Chanzo: Nipashe
 
Ha ha ha ha ha
Aidha, alitaja miradi hiyo kuwa ni ununuzi wa ndege, kujenga reli na elimu bure, huku akitaka Watanzania kudumisha amani na upendo ili uwe mwaka wa maendeleo na ustawi kwa taifa.
 
nitajieni wezi 100 tu ambao amewatumbua na kuwafunga.
bwana jonathan malosa ni DED wakati ni mwizi wa kutiliwa mfano tangu alipokuwa DT.
Balozi ame mpungwe anamiliki hoteli ya kifahari hapa ifakara wakati ni mtumishi wa umma pesa kapata wapi.
makonda/bashite kaja mjini na malapa leo ni tajiri mkubwa pesa kapata wapi
mifano michache tu
 
Asisahau kwamba yeye anahusika na ubadhirifu mkubwa wa kuchota mali za nchi na kupeleka kwao.
 
nitajieni wezi 100 tu ambao amewatumbua na kuwafunga.
bwana jonathan malosa ni DED wakati ni mwizi wa kutiliwa mfano tangu alipokuwa DT.
Balozi ame mpungwe anamiliki hoteli ya kifahari hapa ifakara wakati ni mtumishi wa umma pesa kapata wapi.
makonda/bashite kaja mjini na malapa leo ni tajiri mkubwa pesa kapata wapi
mifano michache tu
Makonda sasa hivi ni tajir wa kutupwa,hata huyo Eliud Mwaiteleke ni mwizi kufuru alikuwa Misungwi kabla hajahamishiwa Chattle!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom