Magufuli nimekupa nyota 3, hadi sasa fanya haya nikupe nyota 5

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,555
3,535
1. Futa mwenge wa uhuru

2. Tumbua jipu la escrow, Richmond.

3. Hamia Dodoma

4. Fikisha kima cha chini mshahara 600,000

5. Waambie watz sera ya viwanda itachukua zaidi ya miaka, 20

6. Watangazie watz ya kwamba upo uwezekano wa dawa kupotea Kwenye vituo vya kutolea huduma, lakini tatizo la msingi ni serikali kutotenga bajeti ya kutosha kwa msd.

7. Hakikisha unafanya vizuri sana kwa idara 3,(elimu, maji na afya)
na hakikisha maeneo haya (elimu, maji na afya) yanaendeshwa kwa mapato ya ndani kwa 100%

8. Tuletee katiba mpya

9. Zuio la safari la nje zisizo na tija lipo sawa,, lakini hili la kuzuia ata wataalamu wetu wa vyuo vikuu kwenda kujiendeleza nje ya nchi(tena hapa karibu Zambia, Kenya, Rwanda, Uganda) halipo sawa.Fanya marejebisho apa

10. Safari yako ya Kwanza nje ya nchi iwe United States of America.
 
Si kila kinachoshauriwa ni lazima Rais akifuate. Ni bora akabaki na nyota hizo tatu kuliko kuwa na nyota tano halafu akaharibu kabisa nchi
 
Kwani hizo nyota 3 ulizompa, ulimpangia nini cha kufanya na akafanya?

Hoja yako haitofautiani na wale wanaohamisha magori ya kisiasa kila siku!

Wengine walitaka Rais aseme mshahara wake, Rais akasema. Kwa sasa wamehamisha tena nguzo za magori ya kisiasa wanataka aseme posho zake na ninaamini akisema, watakuja tena na madai kama aseme huwa ana chakula gani na gharama yake!

It's the political stupid!
 
Kima cha chini mshahara 600000, duh wakati jamaa anabana matumizi!!!
 
Kwani hizo nyota 3 ulizompa, ulimpangia nini cha kufanya na akafanya?

Hoja yako haitofautiani na wale wanaohamisha magori ya kisiasa kila siku!

Wengine walitaka Rais aseme mshahara wake, Rais akasema. Kwa sasa wamehamisha tena nguzo za magori ya kisiasa wanataka aseme posho zake na ninaamini akisema, watakuja tena na madai kama aseme huwa ana chakula gani na gharama yake!

It's the political stupid!

Viroba hivyo chapa Jogoo
 
nyongeza za kupata nyota
1.Afanye majadiliano na wahisani warudi tena kusaidia TZ.
2.Atutengeneze katiba nzuri kama ya South Africa
3.Atupie macho kodi kandamizi za uingizaji magari bandarini.Ni kodi kandamizi sana na kubwa kuliko.
4.Asimamie demokrasia zaidi.
5.Ampe rungu kubwa zaidi waziri wa ardhi katika kutatua migogoro ya ardhi.
 
Si kila kinachoshauriwa ni lazima Rais akifuate. Ni bora akabaki na nyota hizo tatu kuliko kuwa na nyota tano halafu akaharibu kabisa nchi
ni ushauri, na kwa bahati nzuri rais wetu, ana watu makini waliomzunguka.
 
Lumumba wanajitekenya wenyewe na kucheka wenyewe lhalafu wanakimbilia ukawa!

Yaani unampa mtu nyota 3 na unaanza kumpangia

chakufanya umuongezee 5.halafu isemi Hizo nyota za uganga au za angani ??
 
Lumumba wanajitekenya wenyewe na kucheka wenyewe lhalafu wanakimbilia ukawa!

Yaani unampa mtu nyota 3 na unaanza kumpangia

chakufanya umuongezee 5.halafu isemi Hizo nyota za uganga au za angani ??

ni mwenda wazimu tu ndiye ataamini hakuna kitu magufuri ameshafanya adi sasa, lakini ukweli utabaki pale pale ya kwamba safari bado ni ndefu, tena yenye vikwazo vingi kufikia malengo
 
Back
Top Bottom