Umezalishwa, ukatelekezwa. Sasa unaitwa single mother. Fanya haya:

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
25,752
61,867
UMEZALISHWA, UKATELEKEZWA. SASA UNAITWA SINGLE MOTHER. FANYA HAYA:

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kwèñye Maisha mambo meñgi usiyoyatarajia Wala kuyajua huweza kukutokea. Hata usiamini kwamba kweli yamekutokea. Wala usijali. Hayo ndîo Maisha.

Ikiwa ikatokea umezalishwa kibahati mbaya, au kimakusudi ukaamua kubeba Mimba, au uliolewa ukazaa m/Watoto lakini ikatokea mkaachana na huyo Mwanaume akakuacha au ukamuacha au mkaachana.

Íwe Kwa uzembe na Makosa yako au íwe Kwa uzembe na Makosa Yake. Sasa unaitwa Single mother. Mwanamke mwenye m/Watoto na Kwa Bahati mbaya zaidi Mwanaume akawa hawajibiki kuangalia m/Watoto wake mliozaa pàmoja. Íwe haangalii Kwa sababu yoyote Ile íwe ni Kwa sababu umemuudhi Kwa ukorofi na tàbia zako mbaya au ukorofi au tàbia Zake Mbaya.

Yaani Kwa lugha nyepesi umekuwa single mother aliyetelekezwa.
Basi Mimi Baba yako, ndiye Mtibeli nakuambia haya na unisikilize Binti yàngu;

Fanya haya ukiwa katika Hali hiyo:

1. Kubali ukweli;
kuwa wewe siô kama Wanawake Wengine àmbao Hawana Watoto Kabisa.
Hivyo ni ngumu Kwa Wanaume wengi kukubali kuwa na wéwe, kukuoa.
Huo ni ukweli na ni Haki Yao kukuona hivyo. Hivyo usijisikie vibaya.
Ukweli utakusaidia kutokujidanganya na kudanganywa na Wanaume Wengine hasa waovu àmbao watatumia Hali yako kukufanya ujione upo Sawa na Wanawake Wengine Wakati huo ni Uongo. Lengo Lao ni Kukutumia

2. Usimlaumu yeyote Wala kujilaumu.
Íwe ulikosea au ulikosewa. Huna haja ya kujilaumu Wala kulaumu Wengine.
Jisamehe Kisha jikubali vile ulivyo. Msamehe aliyekutelekeza au kaombe Msamaha kwa aliyekutelekeza.

3. Jitegemee. Beba Majukumu yako mwenyewe.
Tafuta Kazi kama ulikuwa hauna. Punguza mahitaji na matumizi yasiyo ya lazima yaendane na Hali yako.
Usimpe yeyote mzigo wako. Beba Msalaba wako mwenyewe. Jitunze na tunza Watoto wako.

Jinsi ya kujitegemea ukiwa Kama single mother;
a) Fanya Kazi Kwa bidii.
Kazi yoyote halali inayokufanya uishi.
b) Kula Vizuri.
Ukifanya Kazi utapata pesa, hiyo Pesa hata íwe ndogo vipi hakikisha unakula unashiba wewe na Watoto wako.
Kula Vizuri siô gharama Sana. Kula ni Sanaa na uwezo wa kubajeti Pesa utakayopata.
Kula Vizuri itakusaidia kuwa na Afya Njema na mvuto. MVUTO utalinda utukufu wako kama Mwanamke. Usikubali kuchoka.
Usitumie Pesa nyingi Saluni. Bora hizo pesa za Saluni uziingize kwèñye bajeti ya msosi weñye lishe Bora. Lishw bora itakusaidia kuwa na Mwili mzuri na urembo utazidi kuchomoza.

c) Toa zaka na sadaka
Saidia Watu waliochini yako. Kama huamini katika Dini. Tenga fungu la Kumi kwaajili ya wahitaji kama wajane wasiojiweza, mayatima, chokoraa na mtaani, au wafungwa.

d) ongeza ujuzi na maarifa.
Hakikisha unaongeza maarifa na kukuza Fikra zako, uwezo wako WA Kazi unaoifanya, ujuzi Mwingine kama kusuka, Kushona, Kupika, Kwa namna ya biashara.

e) jiunge na jumuiya Zenye maadili hapo mtaani.
Jiunge na vikundi vya Wanawake vyenye maadili. Kama ni Mkristo jiunge na vikundi vya Wanawake vya Kanisani vyenye maadili.
Kama ni muislam halikadhalika.

Usikubali ukatumika nguvu zako, Akili zako, Pesa yako sehemu àmbayo haina tija. Usikubali Mtu yeyote akakutumia Kwa maslahi yake Bila wewe kunufaika. Kwèñye hizô jumuiya íwe NI mtaani, Kanisani, msikitini au vyovyote.
Ndîo maana nikakuambia ongeza MAARIFA na hakikisha Akili yako inachaji.

Ujuzi usiouhitaji usiulipie. Jambo lolote ambalo halikufurahishi usilitolee Pesa yako hata Kama ni Kanisani au msikitini.
Usikubali kuambiwa wewe toa tuu Pesa utabarikiwa. Nop!
Toa Pesa pale unapoguswa Moyoni.
Sadaka ya kulazimishwa hainaga Baraka, sadaka ya kushawishiwa hainaga Baraka.
Toa sadaka Ikiwa Moyoni unaguswa kufanya hivyo.

4. Usigombane na Mzazi mwenzako Kwa maslahi ya Watoto wako.
Mmeshaachana, Haitakusaidia kitu kugombana naye.
Mtoto au Watoto wako kûna kitu kikubwa watakihitaji Kwa Baba Yao. Na mwenye uwezo wa kukifanya kitu hicho Watoto wako wakipate ni wewe mwenyewe.

Watoto watahitaji Baraka za Baba Yao àmbaye wewe ulikuwa mwenza wake au ulizaa naye kibahatibahati.
Tumia Akili.
Huenda ni kweli haupendezwi na tàbia ya Mzazi mwenzako au huenda wewe mwenyewe ndîo unamatatizo lakini vyovyote iwavyo hakikisha watoto wako Wapate Baraka za Baba Yao.

Namaanisha, Baba yao asiwe na kinyongo na Watoto uliowazaa wewe. Wala Mtoto asiwe na kinyongo na Baba yake. Hapo Maisha ya Mtoto yatakuwa salama. Hata kama Baba asimpomtamkia Baraka Mtoto.
Mwambie Mzazi mwenzako Watoto wake wanampenda na wanatamani sana kumwona.

Mwambie, unaamini kuwa Hata yeye anawapenda Watoto wake semà mambo yake hayajakaa Sawa. Mwambie asijali kwani Mungu ndiye anayejua.

5. Usiwaabudu WATOTO.
Binti yàngu, Kwanza usimuabudu yeyote isipokuwa Mungu. Ninaposema usiabudu namaanisha usimtegemee yeyote. Wala usimtumainiye yeyote kuwa ndiye tegemeo Lako.

Usiwakuze Watoto wako ili waje wakusaidie baadaye. Unawapa Laana Bila ya wewe Kujua.
Wewe ni Mama. Jukumu Lako ni kuzaa na kulea Watoto àmbao tayari umetelekezewa.

Kulea Watoto ukiwa unawategemea kuwa watakuwa msaada kwako baadaye ni kupanda Mche wa maumivu àmbao Miaka mingi ijayo utakuja kuyala matunda Yake wewe na haohao Watoto.

Mtegemee Mungu, Kisha Fanya wajibu wako. Mungu yeye ndiye anayejua na ndiye anayeandaa msaada wako pindi utakapopatwa na shida. Kumuandaa mtoto kama sehemu ya KUKUSAIDIA Huko baadaye ni kuongeza tatizo zaidi.

6. Ongeza na Linda Thamani na heshima yako
Kuwa Mtu pekee haitoshi kuwa na heshima na thamani. Kûna wajibu unatakiwa ufanye ili uzidi kuheshimiwa na kuongeza thamani yako.

Usilale lale hovyo na kîla Mwanaume kama Mbwa.
Epuka Kulala na Vijana wadogo uliowazidi umri zaidi miaka 10 unajitia aibu na kudhalilisha Watoto wako.

Epuka kuombaomba Pesa na kupewa misaada.
Epuka kujihusisha na Watu wa hovyo yàani kuwaweka Karibu ila haimaanishi uwatenge.

Epuka kufanya Kazi za aibu na kudhalilisha Ûtu wako.
Epuka kuongea ongea maneno ya kishakunapu na matusi.
Epuka kuvaa nguo za kukudhalilisha.

Epuka kudhurura hovyo mitaani pasipo mpàngo maalumu.
Epuka kushinda Bar au kwèñye masaluni Kúpiga umbea.

Epuka kuzozana zozana na Watu mtaani.
Epuka matani na Watu hovyohovyo. Wewe siô Mwanaume. Sisi Baba zako ndîo tunataniana na kuwa na jokes hata za hovyohovyo.

7. Ikiwa utapata Mume mwambie wazi Hana wajibu wa kuwafikiria Watoto aliowakuta. Ila humzuii kukusaidia kama vile wewe utakavyosaidia Watoto wake.

8. Epuka Kúpigania Mali za Mwanaume atakayekuoa Ambazo ulizikuta. Hiyo ni dhulma. Labda upewe Kwa Upendo tuu.

9. Andaa Watoto wako kuwa wake na waume Wazuri.
Kamwe usihamasishe kuishi bila Ndoa.
Watoto wajifunze tàbia Njema kupitia wanavyokuona.
Hawatakuwa na sababu ya kukuuliza Kwa nini wewe NI single mother alafu unawataka waô wawe kwèñye Ndoa kwani tàbia zako zitakuwa Majibu tosha.

10. Waandalie Watoto Urithi.
Akili yako Ikiwa na wazo la kuwaachia Watoto wako Urithi itakuchochea kuzidisha juhudi za kufanya Kazi na kuweka Akiba. Kisha kuandaa Urithi Kwa Watoto wako.

Hivyo ndîvyo Binti za Tibeli hufanya pale àmbapo Bahati mbaya ya kutelekezwa na kuwa single mother inapowatokea.
Huna haja ya kuwa Feminists.

Kutetea haki zako binti yàngu ni kufanya wajibu wako na kujitegemea.
Huwezi pigania Haki zako alafu unamtegemea mtu Mwingine.

Acha nipumzike sasa
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom