Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa! | Page 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mcfm40, Jul 18, 2015.

 1. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

  Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

  Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

  Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli akibahatika kuwa rais watakao kuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwete na Mkapa.

  Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

  Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA kama akibahatika KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

  Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

  TINGATINGA LAZIMA LIONGOZWE LISIPOONGOZWA VIZURI LITALETA MAAFA!
  Watanzania tuchague mtu atakayekuwa na maamuzi ya kwake asiyehitaji kuwa na hofu na alifanyalo. na mtuhuyo ni LOWASA pekee! Magufuli hatoshi kabisa kwenye nafasi ya urais!
   
 2. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #121
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Kipi cha kusubiri kitokee kaka. Magufuli si tupo maye siku zote. Angekuwa na sifa za urais tungexiona. Hakuna udhahania hapa
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #122
  Jul 19, 2015
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,139
  Likes Received: 22,410
  Trophy Points: 280
  Nimekipenda hicho kibinti kwenye avatar yako.

  Ma sha Allah.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #123
  Jul 19, 2015
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Magufuli leo kashindwa kuamini alichokiona Mwanza kapokelea ma makumi ya watu..Magufuli utamu utausikia kampeni zikianza
   
 5. k

  kerubi afunikaye JF-Expert Member

  #124
  Jul 19, 2015
  Joined: May 20, 2013
  Messages: 842
  Likes Received: 323
  Trophy Points: 80
  Ukweli mtupu huu ila watanzania hawajiulizi hayo.Wao wanataka JINA KUBWA basi.Hawajiulizi jina kubwa limekuwa kubwa kwa sifa zipi.
  Huyu bwana wamempeleka chaka.Sio kwake huko.
   
 6. Charles Ignatio

  Charles Ignatio Member

  #125
  Jul 19, 2015
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Nikukubali mkuu kula gwara
   
 7. Neutral Figure

  Neutral Figure JF-Expert Member

  #126
  Jul 19, 2015
  Joined: Mar 8, 2015
  Messages: 537
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Bado upo kwenye chungu au ushatoka?
   
 8. G

  Gabhiteka Manji Senior Member

  #127
  Jul 19, 2015
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu sana kupata majibu ya nini Magufuli atafanya na nn kikichomsukuma kuchukua fomu,hadi pale yeye mwenyewe atakapoelezea kiundani labda kupitia midahalo na wagombea wenzake au atakavoichambua ilani ya uchaguzi ya CCM wakati anaomba kura.
  Watanzania tumejawa na uzembe aa kiutendaji,hilo kalizungumzia kwa kina kuwa atapambana nalo.Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa unatokana na viongozi au watu wenye mamlaka kutowajibika.Sijui kwa nn mleta mada hakuliona hilo km ni tatizo.Sheria mbovu zilizopo zenyewe hazisimamiwi ipasavyo,maendeleo yepi tutayapata katika hali hii?Tusimamie sheria na atafanya kazi nzuri zaidi kama mapendekezo ya katiba ya Warioba itarudishwa bungeni na kuidhinishwa kutumika.
  Magufuli anaijua sheria,tatizo ni viongozi wetu walio wengi kutopenda kutekeleza sheria,huyu jamaa ni mtu wa kipekee na taifa linamhitaji kiongozi km huyu asiyegubikwa na makundi ya rushwa yanayowanyima haki wananchi wa kawaida.
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #128
  Jul 19, 2015
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Mkubwa, ni kuangalia hali ya nchi kwa sasa,naona tunahaitaji mtendaji. Tatizo ni kuwa uongozi umewekwa kwenye makaratasi kwenye mipango, sera na miongozo. Tatizo ni kuwa ni nani hasa wa kuhakikisha hayo yanafanyika au yanatekelezwa? In my view tunahitaji Rais Mtendaji, waziri mkuu mtendaji, wakuu wa mikoa watendaji na wakuu wa wilaya watendaji. Tatizo letu ni kuwa watu hawafanyi kazi.
   
 10. STDVII

  STDVII JF-Expert Member

  #129
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 24, 2014
  Messages: 1,500
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Nachukia watu wanaolinganisha udhaifu/ujinga/matatizo yao binafsi na Watanzania kwa ujumla wao.
  Tafadhali usituweke kundi moja fijiri tofauti....
   
 11. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #130
  Jul 19, 2015
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,961
  Likes Received: 1,420
  Trophy Points: 280
  mkuu maneno murua kabisa. lakini jee ni wangapi watakuelewa?
   
 12. CONSTRUCTIVE THOUGHT

  CONSTRUCTIVE THOUGHT JF-Expert Member

  #131
  Jul 19, 2015
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 1,167
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Sifa za Rais ni zipi kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania?
   
 13. S

  SADIT Member

  #132
  Jul 19, 2015
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Aliyeacha kufikiri ni yule aliyekufa tu. Narejea, jina hubeba sifa, tabia na mwenendo wa mtu, kitu au sehemu. Aliyetoa jina la Tingatinga kwa mtu hakukosea alifanya akijua hasa anamaanisha nini kwa aliyemkusudia, Wote tunajua sifa za Tingatinga lakini kifaa hiki bila dereva makini si chochote, Kwa kuwa wamechagua Tingatinga ninaamini watakuwa wameandaa na dereva. Keep watching the movie
   
 14. CONSTRUCTIVE THOUGHT

  CONSTRUCTIVE THOUGHT JF-Expert Member

  #133
  Jul 19, 2015
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 1,167
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Magufuli wamemuonea kivipi? Niambie neno nilielewe neno usiniambie neno nilikalili neno. Sawa kumbe unaandika neno litakalokuijia haraka kichwani bila kujali ujumbe unaokusudiwa, muktadha wa maengezi, uelewa wa wazungumzaji kuhusiana na lugha yenyewe.
   
 15. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #134
  Jul 19, 2015
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,963
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  Dereva nasikia anaitwa/jiita KITENGO.
   
 16. P

  Pilitoni JF-Expert Member

  #135
  Jul 19, 2015
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 1,002
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Kuna watu wanatikisa kiberiti ile wajue kuwa kimejaa au la,watu wanatishia kuhama mf.james lembeli,mnatakiwa mjue kuwa huyu jamaa alikuwa na hali tete jimboni kwake kahama na sasa jimbo hilo limegawanywa ie kahama mjini na ushetu.Kama anataka ajifie kisiasa ahame,sawa upinzani ulikuwepo ukanda huu wa kahama ila kwa sasa mmh,mbunge wa bukombe prof kahigi-chadema anapumulia mashine,harudi bungeni 100% na jimbo hilo litarudi ccm.Kusimamishwa kwa tingatinga ni pigo kwa upinzani aisee.WATU WANASEMA HUKU KUWA WAPINZANI+LOWASSA WATACHIMBA MASHIMO TINGATINGA LITAFUKIA,CHEZA NA TINGATINGA WEWE,nawaonea huruma sana wapinzani maana ruzuku ndio hiyo inapotea
   
 17. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #136
  Jul 19, 2015
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,947
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Huyo tinga nani ampe kura,huyo ni jk part 2,jk kamchomoa mfukoni kwake,jk akistaafu atakuwa anaendesha nchi akiwa msoga
   
 18. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #137
  Jul 19, 2015
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,827
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hizi ni ndoto za mchana za kujifariji. Huwezi kusema eti wanaohama chama wanamuhofia Mh. Magufuli. Tafuteni sababu ya msingi na muifanyie kazi kuliko kutunga hizi porojo.
   
 19. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #138
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Magufuli amebaki kusema tu sitawaangusha. Nitatekeleza ilani ya CCM. yeye km yeye ana maono gani kuhusu hii nchi? Anaonekana km ameshtukizwa. Watz tumeingizwa choo cha kike!
   
 20. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #139
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Ongelea habari za magufuli wewe. Achana na ngonjera. Ungekuwa hujaelewa usingeweza kujibu! Hebu nitajie sifa tatu za magufuli zitakazomfanya rais bora kuliko wengine Tanzania!
   
 21. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #140
  Jul 19, 2015
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,819
  Likes Received: 3,621
  Trophy Points: 280
  Tingatinga atamaliza kazi ..vijana wa Jf wako hapa kama kawaida yao wanashinda kwenye mitandao wwkidhani siasa hiko mitandaoni, tuliona vijana wa Lowassa walivyokuwa wakikesha hapa Jf na baadae kilichomtokea Mungu wao ..mwaka huu mtaisoma namba
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...