Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

mkuu utambue kuwa raisi akiwa dhaifu hata waziri mkuu atakuwa dhaifu na raisi akiwa imara hata mawaziri nao watakuwa imara,

tunahitaji raisi ambaye akisimama kuhimiza jambo watendaji wake lazma waende mbio kulitekeleza.

Mbona mnajihofia sana kwann?
Hata kama itakuja ya kulala saa moja na kuamka saa 10 poa tu.
Tumezidi kufanya kaz kwa mazoea nakuona hata ww hapo unaongelea au unatetea mazoea.

Umeongea point tupu, Raisi akishakua legelege hata waziri mkuu atakua legelege tu.
 
Hivi ccm watakuwa wameishiwa kabisa? Magufuli ana sifa gani za kuwa rais wa nchi. Maana na umuhimu wa urais imepotea kabisa. Magufuli ni mchapakazi lakini hana sifa nyingine muhimu zinazofaa kuwa rais. Ni wa kawaida mno. Ccm walizingatia tu kigezo cha kufahamika kwa uchapakazi wakasahau vingine! Vyama vya upinzani jipangeni vizuri mchukue nchi. Magufuli sio presidential material.

Sifa nyingine ni zipi hizo mkuu?
 
Isipokuwa hajasema Tanzania inahitaji nani kazi ya kiongozi na mtendaji. Kuna mmoja ambaye nchi inamhitaji kwa sasa.

Ni nani huyo tutajie kama upo huru kutaja?

Kaka wenzetu japan wamefanikiwa kwa kuchapa kazi,ukiajiriwa japan kwenye kampuni ya tajiri hutamjua mpaka uambiwe maana kama kazi mnapiga ngoma draw hakuna cha boss wala tajiri mnaingia saa mbili kamili wote asubuhi,mnatoka kumi na moja na mbakuwa sawa katika kufanya kazi isipokuwa mshahara,sasa mtu mwajiriwa tajiri anapiga mzigo wewe kwa nini utegee,huo mfano magufuri akiingia front hata wale mawaziri walioteuliwa kama waba vi element vya uvivu watakaa kwenye mstari tu wakiona boss naye anawajibika,na ndito tanzania anatakiwa kiongozi kama huyo,tuache kulewa sifa za kujiita boss unakaa ofisini unaacha kukagua shughuli za serikali,kumbuka waziri mkuu anaweza kuwa strong ila kama raisi ni mpole,waziri mkuu utakosa confidence ya utendaji,chukulia mfano waziri magufuri alivyokuwa anasimamia sheria za barabara,lakini kwa sababu ya upile wa mheshimiwa rausi na mheshimiwa waziri mkuu,magufuri akajikuta anakutana na barrier,lakini yeye akiwa final na akawa ana base kwenye sheria ya nchi hiyo ndiyo njia pekee ya kumfanya mtendaji asimamie sheria si kuoneana aibu,tufike wakati tuwe wakweli na kuelimishana,raisi akiwa strong automaticaly watu wa chini watanyoka tu iwe kwa kujikosha au kweli ili mradi mafanikio na maendeleo yapatikane,kumbuka enzi za marehemu sokoine,na nyerere,kwa sababu marehemu nyerere hakutaka mchezo katika uongozi,sokoine akaonekana mtendaji mzuri sababu boss wake alikuwa naye ni mchapakazi,hata hiyo wizara ya ujenzi sasa hivi huwezi kuta ujinga ujinga,maana waziri wake magufuri ni mchapakazi,akamteua mr mfugale kama ceo wa tanroads,naye ni mchapakazi na wanakuwa kama team ndiyo maana unaona wakandarasi wa barabara hawaleti ujinga,jamani hebu tuwe wakweli na tusifie kitu kinapistahili,magufuri surely ataleta mabadiliko makubwa,na mfano uliotolewa wa bulldozer kuendeshwa na mtu mwingine nafikiri haufai ktk hilo
 
Umeongea point tupu, Raisi akishakua legelege hata waziri mkuu atakua legelege tu.

Shida kubwa ya Tanzania ni ufisadi na wala sio watu kutofanya kazi. ufisadi na rushwa ndio tatizo linalosumbua wananchi. Kumbe Kikwete alikuwa legelege? hahaha. na ufisadi ndio roho ya CCM. Ukipambna na ufisadi utakuwa unapambana na CCM. Magufuli anakuja kupambna na watu kwenda kufanya kazi au na ufisadi uliokokomaa ndani ya sysyem?
 
Sifa nyingine ni zipi hizo mkuu?

Waliorodhesha sifa nying tu mfno awe na uzoefu wa kutosha kimataifa. Asiwe dikteta. Awe msikivu na anayesikiliza ushauri. Asiwe na papara. Haya ni aliyatja mangula. By the way hata system uslama ya nchi magufuli haijui Wenzake wengi walifik vyeo vikbwa va jeshi, wengne usalama wa Taifa. Huyu mmmhh. Wengine walikuwa wanasema awe anakifahamu chama vizuri, yaani amekulia kwenye chama. magufuli ni wa kuja. Ni rahisi kuja kupigwa chini na wanaccm akijifany analeta za kuleta!
 
Safiii sana Mkuu..! Obrigado kwa uchambuzi wa kina juu ya mr presida to may be come..! Tuna kazi kama dereza atakayeendesha hili tingatinga atakuwa wale wale
 
Unajipa moyo.

Hebu na wee changia hoja acha mipasho, Huoni aibu wenzio wanvyochangia hoja wewe unakuja na taarabu zenu za pwani? najua hata wewe hujafuraishwa na magufuli. lakini ndio hivyo wa dini yenu hayupo mara hii!
 
Neno hili tingatinga nililisikia kwanza kwa Malecela. Ilisemekana pia kuwa tjngatinga linatumika kutengeneza barabara, lakini barabara ikishakamilika tingatinga aliruhusiwi kupita. Na hii ndivyo ilivyokuwa kwa Malecela alitengeneza barabara hakuruhusiwa kupita ila wengine walipita kwa raha! Sijui kwa nini Rais Kikwete alimbatiza jina hili Mh. Magufuli?
 
Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli atakuwa rais lakini watakaokuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwet na Mkapa.

Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

TINGATINGA LAZIMA LIONGOZWE LISIPOONGOZWA VIZURI LITALETA MAAFA!
Wabongo mbona hamueleweki? Mara Rais anawabeba marafiki zake, mara hana maamuzi, mara hafai! Leo Kachaguliwa Magulfuli..... mmeanza oogh... Rais ni taasisi, Rais sio mtendaji, mara Magufuli hana personal vision wakati huo huo unasema Rais ni taasisi... ulisha una wapi Taasisi inaogozwa kwa personal vision?
 
Shida kubwa ya Tanzania ni ufisadi na wala sio watu kutofanya kazi. ufisadi na rushwa ndio tatizo linalosumbua wananchi. Kumbe Kikwete alikuwa legelege? hahaha. na ufisadi ndio roho ya CCM. Ukipambna na ufisadi utakuwa unapambana na CCM. Magufuli anakuja kupambna na watu kwenda kufanya kazi au na ufisadi uliokokomaa ndani ya sysyem?

nakushangaa sana mkuu unajifanya hufaham wakat unafahamu...

Kipind cha nyerere hakukuwa na ufisadi kama ulivyo miaka hii yote hayo ni kwamba nyerere alikuwa na uwezo wa kuvamia watendaji wake na kuwakemea pale mambo yanapoteteleka kuna mawaziri wamewahi kula cha moto kipind cha nyerere.

Ukija kipind cha kikwete watendaji wengi walilala sababu kiranja mwenyewe alikuwa sio mkali wala sio mvamizi
 
Wabongo mbona hamueleweki? Mara Rais anawabeba marafiki zake, mara hana maamuzi, mara hafai! Leo Kachaguliwa Magulfuli..... mmeanza oogh... Rais ni taasisi, Rais sio mtendaji, mara Magufuli hana personal vision wakati huo huo unasema Rais ni taasisi... ulisha una wapi Taasisi inaogozwa kwa personal vision?

Wewe wa wapi? personal vision na conviction ya CEO ndiyo inayodtermine ufanisi wake. Km CCM wakimpa magufuli sera ambazo haziamini unadhani atazitekeleza kwa moyo wake wote? Unataka kusema Magufuli ndio ana sifa tulizozitaka? Magufuli hana sifa za kuwa rais wa nchi. sansana angefaa uwaziri mkuu.
 
bora umeliona hilo mkuu.
Watanzania wajinga sana hawana msimamo kazi yao kulalamika tu
 
bora umeliona hilo mkuu.
Watanzania wajinga sana hawana msimamo kazi yao kulalamika tu

Watanzania tuna msimamo sana. Tuliposema tunataka rais dikteta, hatukumaanisha rais asiwe na busara na mediocre. Mfano wa rais dikteta ni kama mkapa. Intellectual na anaogopeka. lakini magufuli suio intellectual. We want an all round president sio mwenye sifa za upande mmoja tu. Nafasiya urais ni special jamani. sio ya kila mtu. agufuli natapwaya san km akkichaguliwa
 
Mtu ambaye hata akisimama kwenye majukwaa ya kimataifa akizungumza watu wakubali there is a president. Mkapa alikuwa na hizi sifa. Aliheshimika sana kimataifa na wenzake huko serikalini walimwogopa. Unajua ile uwezo wa kucomand respect kutoka kwa subordinates wako inatgemea na uwezo wako binafsi na upeo wako. Je wenzako wanaweza kukuangalia km dira yao? wakafuata misimamo na falsafa yako? I cant see this in magufuli.
 
Wewe wa wapi? personal vision na conviction ya CEO ndiyo inayodtermine ufanisi wake. Km CCM wakimpa magufuli sera ambazo haziamini unadhani atazitekeleza kwa moyo wake wote? Unataka kusema Magufuli ndio ana sifa tulizozitaka? Magufuli hana sifa za kuwa rais wa nchi. sansana angefaa uwaziri mkuu.
Atakubalije kuteuliwa kwake na wao alafu sera zao awe na wasiwasi nazo. Pia, wewe mwenyewe umenukuu kauli yake kuwa ataekeleza sera za chama!!!!!!!!!!! Magufuli hana sifa za kuwa Rais, tuambie kwa mujibu wa katiba ya Tanzania sifa za Rais ni zipi? Alafu tumia lugha moja kama Kiingereza au Kiswahili au Kichina.... usichanganye luga zaid ya moja kwenye sentensi moja.
 
Mtu ambaye hata akisimama kwenye majukwaa ya kimataifa akizungumza watu wakubali there is a president. Mkapa alikuwa na hizi sifa. Aliheshimika sana kimataifa na wenzake huko serikalini walimwogopa. Unajua ile uwezo wa kucomand respect kutoka kwa subordinates wako inatgemea na uwezo wako binafsi na upeo wako. Je wenzako wanaweza kukuangalia km dira yao? wakafuata misimamo na falsafa yako? I cant see this in magufuli.
Unataka kuona kitu kabla hakijatokea? mbaya zaidi unataka kuona vitu dhahania!!!!!!!!!!
 
Hapo hakuna ki2 tuctegemee magufuli kuleta mabadiliko kwani anasema atailinda ilan ya ccm inamaana ataendelea kuwalinda mafisadi yani watawala ote wa CCM nikama bakuli inabadilishwa mboga tu ila bakuli nililelile namakufuli imebadilishwa mboga ila bakuli ni lilelilea.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Magufuri kweli ni mchapakazi hapo hakuna ubishi, hilo tingatinga litaweza kubomoa mafisadi walioko ndani ya CCM maana hao ndio ni hatari zaidi ya watendaji wazembe walioko serikalini.
 
Magufuri kweli ni mchapakazi hapo hakuna ubishi, hilo tingatinga litaweza kubomoa mafisadi walioko ndani ya CCM maana hao ndio ni hatari zaidi ya watendaji wazembe walioko serikalini.

Kaka tatizo ni kwamba akijaribu kubomoa mafisadi maana anabomoa chama kwa sababu ccm na ufisadi ni uji na mgonjwa
 
Atakubalije kuteuliwa kwake na wao alafu sera zao awe na wasiwasi nazo. Pia, wewe mwenyewe umenukuu kauli yake kuwa ataekeleza sera za chama!!!!!!!!!!! Magufuli hana sifa za kuwa Rais, tuambie kwa mujibu wa katiba ya Tanzania sifa za Rais ni zipi? Alafu tumia lugha moja kama Kiingereza au Kiswahili au Kichina.... usichanganye luga zaid ya moja kwenye sentensi moja.
Kuhusu la lugha nitajimwaga kuendana na neno linalomijia haraka kichwani. Siandiki dussertation hapa! Kama lugha inakuudhi kale malimao. Sijui atakuwa tena mtu ambaye akizungumza kwenye mikutano ya kimataifa inabidi uinsmishe kichwa chini kwa sababu ya lugha. Kwa Magufuli hakuna rais hapo wamemwonea tu.
 
Back
Top Bottom