Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa! | Page 9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mcfm40, Jul 18, 2015.

 1. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

  Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

  Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

  Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli akibahatika kuwa rais watakao kuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwete na Mkapa.

  Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

  Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA kama akibahatika KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

  Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

  TINGATINGA LAZIMA LIONGOZWE LISIPOONGOZWA VIZURI LITALETA MAAFA!
  Watanzania tuchague mtu atakayekuwa na maamuzi ya kwake asiyehitaji kuwa na hofu na alifanyalo. na mtuhuyo ni LOWASA pekee! Magufuli hatoshi kabisa kwenye nafasi ya urais!
   
 2. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #161
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Nijiulize mpaka lini kaka?
   
 3. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #162
  Jul 20, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Unaonae? Kwa vile mwenyeketi kasema ni bulldozzer basi kila mtu kaona ni sawa. Ingawa wanaccm wenyewe km kina Faiza Fox wanakubali kuwa lazima magufuli aongozwe na chama km atachaguliwa la sivyo ataharibu vibaya. sasa hapa tuna rais?
   
 4. e

  eddy JF-Expert Member

  #163
  Jul 20, 2015
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 10,661
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Matingatinga ya kisasa ni programmable na linaweza setiwa kwa auto control, au likawa computer guided, hivyo usiwe na wasiwasi.
   
 5. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #164
  Sep 18, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Na kweli hili Tinga tinga limesetiwa na autocontrol. Linaropoka hovyohovyo hata vitu vingine halijui linasema nini!
   
 6. f

  food test JF-Expert Member

  #165
  Sep 18, 2015
  Joined: Jul 15, 2015
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sadam alikua rais wa libya
  sadam alikua rais wa kuwait.
   
 7. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #166
  May 8, 2016
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,148
  Trophy Points: 280
  Qejsjakk
   
 8. Cjtranter

  Cjtranter JF-Expert Member

  #167
  May 8, 2016
  Joined: Aug 23, 2013
  Messages: 206
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Wewe utakuwa umeficha sukari sio bure, sasa sisi hii habari inatusaidia nini?
   
 9. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #168
  Oct 12, 2017
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Vipi Paskali, umeikumbuka storry ya Tingatinga ya 2015. Vipi huu unabii unauonaje? Sehemu kubwa nilipatia!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...