Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa! | Page 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mcfm40, Jul 18, 2015.

 1. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

  Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

  Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

  Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli akibahatika kuwa rais watakao kuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwete na Mkapa.

  Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

  Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA kama akibahatika KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

  Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

  TINGATINGA LAZIMA LIONGOZWE LISIPOONGOZWA VIZURI LITALETA MAAFA!
  Watanzania tuchague mtu atakayekuwa na maamuzi ya kwake asiyehitaji kuwa na hofu na alifanyalo. na mtuhuyo ni LOWASA pekee! Magufuli hatoshi kabisa kwenye nafasi ya urais!
   
 2. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #141
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Na dalili zinajionesh kabisa kwamba Magufuli hajiamini. Ukifuatiliwa kampeni zake alizoanza kabla ya muda you feel it kuna kitu hakliko sawa. CCM wanamkaririsha maneno matamu ya kuwaambia watu, eti mfano, nitawatetea wanyonge, hii si nature ya Magufuli. Magufuli yeye anafuata sharia km roboti tu. Hivi mmachinga na mwendesha bodaboda anaweza kuamini maneno ya Magufuli kweli eti atawatetea! Atawatetea dhidi ya nani? Dhidi ya serikali yake mwenyewe?
   
 3. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #142
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Uzoefu wa kimataifa, mtu aliyemtulivu, na naye fanya maamuzi bila papara. mtu asiye na kashfa (Magufili ana kashfa ya upotevu wa mabilioni wizarani kwake na kuuza nyumba za serikali kwa hawara zake) baadhi tu ya sifa. Usisahau CCM wametupa sifa za mgombea wao wanayemtaka. magufuli alipatikana kwa bahati mbaya!
   
 4. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #143
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Mwanangu! FF tuseme ukweli ishu ya Magufuli unaionaje? Hapa tuna rais kweli? Bora JK hakya nani! Tuacheni ushabiki wa kijinga. Hivi kina Mkapa walikaa kabisa wakaona magufuli ndio bora kuliko wote? Seriosuly? Bora wangempa hata yule muhuni Makamba mzee wa upara!i Tukipe heshima kiti cha urais jamani!
   
 5. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #144
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Nani anategemea Magufuli aje atende kinyume na mazoea na utaratibu wa CCM? Kikwete alijaribu wakati ule wa akitaka kuleta katiba mpya kwa nia njema kabisa lakini, wanccm wakamwambia waziwazi kwamba kwa vile yeye anaondoka sasa anataka kuleta mambo yatakayokiangusha chama? Kikwete akaufyata akawaruhusu CCM wabadili ile rasimu walivyotaka wao. Eti Magufuli ndio ataweza kupambna kubadili hiki chama ambacho kinaogopa mabadiliko kwa kigezo kwamba yatakiumiza? Magufuli hataruhusiwa kufanya jambo lolote linloweza kuhatarisha uhai wa CCM. Ni kwa msingi huu tunasema tusitegemee mapya. Tulimsifia sana kikwtet wakati ule kwa kusema ni Nyerer mpya lakini hakuna mabadiliko ya maana aliyofanya leo kila mtu analalamika. Kilichomfanya kikwet kushindwa leo magufli aweze nini? wakati mifumo ni ile ile iliyomkwamisha kikwete?
   
 6. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #145
  Jul 19, 2015
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,398
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  Anhaa!
  Hapo sawa mkuu, nilichokifikiria mimi ni sawa na ulichokifikiria wewe...ni kweli kabisa tunahitaji kiongozi ambaye ni mtendaji kwa Tanzania ya leo, nchi hii kwa mtazamo wangu katika kila nyanja kama vile kisiasa, kijamii, kielimu, kiuchumi na mengineyo naweza nikasema zimeharibika kwa baadhi ya mambo tena mengi tu, hapa dawa ni kumweka mtendaji tu wa kuweka mambo yote sawa, jamani Watanzania wenzangu tuwe na nia mmoja, Magufuli kwa vile ni mtendaji hasa hasa kwa nature yake, itapendeza saaana nchi kuwa ya kiutendaji kuanzia ngazi za juu hadi chini kiuongozi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
  Tanzania ya leo dawa yake ni kufanya kazi kwa bidii kuliko siasa, Magufuli ndo dawa ya Tanzania ya leo.
   
 7. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #146
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  ila hakuna kitu kinaitwa rais mtendai kaka. Rais ni rais, watendaji ni walio chini yake. Ndani ya mifumo ileile inayoruhusu watendaji kuharibu unategemea nini kipya? Unamweka mtu mzuri kwenye mfumo mbovu unategemea atadeliver? Tatizo la hii nchi sio watu ni mifumo iliyoasisiwa na chama cha mapinduzi. Unadhani magufuli anaweza kuibomoa? kuibomoa hiyo mifumo ya ulaji ni sawa na kuibomoa ccm ukumbuke> Na alishawaahidi kwamba hatawaangusha!
   
 8. KATASAN'KAZA

  KATASAN'KAZA JF-Expert Member

  #147
  Jul 19, 2015
  Joined: Jul 24, 2013
  Messages: 2,844
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Akafie mbali alipokea ilani ya akakubali wamtume na kukiri kuwatumikia leo awe kiboko wao utakuwa unamwa wewe c bure!
   
 9. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #148
  Jul 19, 2015
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,398
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  Sawa umenena vizuri, lakini pamoja kwamba Rais siyo Mtendaji, ni afadhali zaidi kwa huyo maana atakuwa anabuni njia mbalimbali za kutatua matatizo, Nyerere alikuwa mtendaji zaidi, hata ukiangalia Uhuru Kenyatta ambaye ni Rais wa Kenya ni mtendaji, Kagame mwenyewe huko Rwanda ni mtendaji, unaona hali ilivyo??
   
 10. A

  Ambiente Guru JF-Expert Member

  #149
  Jul 19, 2015
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 2,314
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Unge -Google kupata tasfiri ya kiingereza ungeshaangaa zaidi maana ya kiongozi kuitwa Bulldozer.

  Nashauri Mgombeamwenza naviongozi wengine waache mara moja jinahilo
   
 11. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #150
  Jul 19, 2015
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,565
  Likes Received: 367
  Trophy Points: 180
  Tingatinga ebu tumalizie kipande cha barabara ya lami kutoka Nyakanazi hadi Kigoma kabla haujachukuwa nchi. Kigoma imesahauliwa kwa barabara za lami zinazounganisha mikoa toka enzi Mv. Liemba!
   
 12. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #151
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Pokea like mkuu. Eti wao ccm wamtyme halafu awe kiboko ya kiwakomesha ccm haohao waliomtuma. Thubutu?
   
 13. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #152
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Kuna jambo najiuliza. Magufuli amekuwa waziri wa ujenzi vipindi tofauti kwa muda mrefu, imekuwaje kashindwa kushughulikia tatizo la foleni Dar. Mpaka leo ni hadithi za kaflyover kamoja eti tazara upembuzi yakinifu unaendelea!
   
 14. Usher-smith

  Usher-smith JF-Expert Member

  #153
  Jul 19, 2015
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 6,505
  Likes Received: 5,390
  Trophy Points: 280
  Lol makubwa
   
 15. M

  MTK JF-Expert Member

  #154
  Jul 19, 2015
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 7,262
  Likes Received: 3,105
  Trophy Points: 280
  Well stated man, I Can not agree more with You! John Magufuli ni Nyapara sio meneja! Too mechanical and whimsical to be a good président, He has to be managed by someone else while He does his Unyapara antics! Bad choice for the country, a terror régime Is rearing to enter, God forbid.
   
 16. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #155
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  kabisa mkuu. Magufuli hata sijaona kabisa. Ni mtiifu sana kwa wakubwa zake. Sioni akiweza kuovercome nguvu yw hawa marais wWili waliomtangulia kwa sababu lwa sifa za jumla za kiuongozi anapwaya sana.
   
 17. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #156
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Nimependa hilo neno ulilotumia 'Nyapara' linamdefine vizuri sana Magufuli.
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #157
  Jul 19, 2015
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,140
  Likes Received: 22,410
  Trophy Points: 280
  Magufuli ni msimamizi mzuri wa kazi anazopewa, hilo kisha lionesha. Kumbuka kuwa na sera atazosimamia atapewa na chama cha mapinduzi, usifikiri Magufuli kuwa atathubutu kuja na jipya kama aliyokuja nayo Kikwete. Huko hapawezi yeye ataendelea kuwa ni msimamizi wa sera za chama katika Serikali atayoiendesha.

  Sasa hivi CCM imeamuwa kuwa Rais yeyote ni lazima afate maelekezo ya Chama, hiyo ni baada ya Kinana kutembelea nchi nzima, mikoa yote, na wilaya na kata karibu zote. Kazi kubwa sana ameifanya Kinana na hata uchambuzi wa mgombea Urais ndani ya CCM umetokana na kazi hiyo ya Kinana.

  Cha muhimu tusitathmini kitabu kwa jalada lake.
   
 19. J

  Jang Bo Go JF-Expert Member

  #158
  Jul 19, 2015
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 852
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Dah Kikwete hana mfano kumbe.
   
 20. J

  Jang Bo Go JF-Expert Member

  #159
  Jul 19, 2015
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 852
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Endelea kujiuliza.
   
 21. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #160
  Jul 19, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  Faiza Fox leo umeamua kuwa mkweli! Nimependa hapo uliposema Magufuli hataweza kuja na jipya. Ataitegemea Ccm. Kwa hiyo mwanaCcm umekubali bila Magufuli kuongozwa hii nchi hataiweza! Sasa ndugu, tuiamini CCM hii hii iliyoshindwa kuleta mabadiliko kwa miaka hamsini? Tutaaminije CCM itamwongoza Magufuli kwa faida ya wananchi na si chama chenyewe? Kwa nin nini tumwamini mtu ambaye hana personal vision? Tuongozwe ma rais ambaye atasubir maelekezo ya kinana?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...