Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Magufuli hafai kuwa rais yy ni mtendaji mana hana vision ya kusaidia nchi.zaidi anahubiri nitadili na watumsh wabovu.ovy
 
mkuu naona wameanza kujihofia walimwonea mzee wa msata sasa amewajia ngosha wanahaha hawajui wakimbilie wapi.
Hata mabubu sasa hivi naona wanaongea magufuli anatisha

Magufuli hawezi kuwa Magufuli latika nafasi ya Urais. Kutokuwa kwake na uzoefu waambo ya siasa kutamfanya kutojiamini. Kuongoza nchi sio sawa na kujenga barabara au kusimamia wizara. Ni kipaji ambacho Magufuli hana.
 
Magufuli hafai kuwa rais yy ni mtendaji mana hana vision ya kusaidia nchi.zaidi anahubiri nitadili na watumsh wabovu.ovy
Kabisa Mkuu. Urais unaweza kuuita ni superstructure na mawaziri ndio structure. Magufuli does not have leadership skills.
 
Makala yako ni nzuri lakini umeiandika kana kwamba Magufuli anasubiri kuapishwa tu
Yani kama vile hakuna mchakato mwingine mbele yake ambao haiyumkini ndio ukawa mwisho wake na chama chake kuliongoza taifa hili
Msijisahau rais wa nchi hii hachaguliwi na NEC ya ccm anachaguliwa na watanzania wote.
Na hapa kuna watu wanajifariji eti 'system' ndiyo inamweka rais madarakani, ukiwauliza hiyo system ni nani watakwambia sijui tiss, sijui polisi, sijui jeshi na mengine mengi. Lakini ukiwauliza kama members wa hizi organs hawakuwemo kwenye 'safari ya matumaini' wanaishia tu kulazimisha hoja zao. Tunachosahau sana ni kuwa hawa nao ni binadamu na wana hisia, furaha, matumaini na kikubwa kabisa kuishi na kufa kama sisi!
Na mfano ni IGP anapowaomba wananchi kusaidia kuwapata wavamizi wa kituo na kuua polisi. Hivi mabadiliko tunayoongelea ni mapana zaidi na yanaenda mpaka kwenye hizo taasisi, sidhani kama wananchi watapiga kura zao zikafika 90% alafu wewe ukajitia ujanja wa goli la mkono na kuichakachua 40% yote kumsaidia mtu fulani na hii nchi ikabaki kama tulivyoizoea!
"Hizi .....iyena ....iyena hiziwezi kuleta ushindi na enzi za mteule wa ccm ni rais zimekwisha, ushindi unakuja kwa kujiandikisha na kupiga kura" - JK
 
Kabisa Mkuu. Urais unaweza kuuita ni superstructure na mawaziri ndio structure. Magufuli does not have leadership skills.

jaman msitafisir watu kwa kukariri nyerere alikwa na elim ya siasa?
Alikuwa na uzoefu wa kimataifa?
Tambuen uongoz bora sio elim wa utaalamu wala uzoefu bali n kipawa ambacho mtu hupewa na Mungu...
 
Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli atakuwa rais lakini watakaokuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwet na Mkapa.

Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

TINGATINGA LAZIMA LIENDESHWE. LISIPOENDESHWA LITALETA MAAFA!
Umenena vyema kuhusu tingatinga, hapo kwenye rangi nyekundu ni kwamba usipoliendesha tingatinga linabaki tu limetulia halifanyi chochote. Ila ukishaanza kuliendesha linakuwa katika hali uliyolielekeza wewe mpaka ulipe maelekezo mengine ndio litabadili kile lilichokuwa linafanya. Dah! hili jina halifai kupewa kiongozi mkuu wa nchi, bora wafikirie lingine. Kama hawatfanya hivyo maana yake wamekubaliana na tafsiri yako.
 
jaman msitafisir watu kwa kukariri nyerere alikwa na elim ya siasa?
Alikuwa na uzoefu wa kimataifa?
Tambuen uongoz bora sio elim wa utaalamu wala uzoefu bali n kipawa ambacho mtu hupewa na Mungu...
Sasa wewe ndio umekariri. Unamlinganisha Magufuli na Nyerere? Nyerere alukuwa geniuos na alokuwa na kipawa cha kuongoza cha kuzaliwa. Sasa hebu tuambie Magufuli ktk mda wote aliokaa serkalini ameonesha sifa za kiobgozi? Ana kipawa unachosema cha uongozi? Nimesema Magufuli is very mechanical. Nafasi akizofanyia kazi hazisadifu
Kabisa nature ya urais. Waziri wa barabara waziri wa uvuvi waziri wa nyumba na ardhi. Hizi sio post zinazomtengeneza mtu kuwa rais. Km akichaguliwa Tanzania tutaendelea kuwa na marais mediocre. Kwa mfano ungeniambia kuwalinganisha huko CCM heri Makamba Junior mara 10 kuliko Magufuli.
 
Tanzania tunahitaji mtendaji si mtu type unsyodai ya maono,hata asiyena maono hapa kwetu anajifanya mwenye maono ili asikose hiyo nafasi ya urais,watanzania ni wavivu hamuwezi kujiongoza mpaka mkimbizwe mchakamchaka kama enzi za mrema,magufuri anafeet hapo,mliozoea kwenda lunch time 2-3hrs na kuinfia kazini saa 9am,na kuendekeza rushwa kwa kweli mbabidi mkimbie kihama kinakuja na ukumbuke speed ya magufuri itagusa kila idara,kuanzia kijijini mpaka taifa,private companies,government corporations,na mpaka nyumbani kwako,tunaimani na magufuri na yatakuwa tu,hakuna mtu aliyezaliwa na taaluma ya uraisi isipikuwa kusimamia sheria zilizowekwa,na kujua matatizo ya wananchi,nashangaa sana watu wanaom criticize magufuri,jamani tunahitaji kusoma profile za watu si kukurupuka na kushawishi watu uongo kwa yale unayoamini wewe,
 
Tunahitaji raisi dikteta ambaye anauwezo wa kukemea jambo na watendaji wote wakafyata.

Alikuwepo kikwete milikuwa mnamtukana kuwa n mpole hafuatlii mambo.
Kumbuka upole wa kikwete ndio ulisababisha yakatokea haya richmound, escrow n.k.

Sasa hapa ilitushike adabu lazma magufuli ashike nchi awawajibishe wazembe.

Karibu magogon mzee magufuli.
Naona wala rushwa, wafanyabiashara haramu na mafisadi wanaanza kufarakana.
Mm nakuombea uingie ikulu ili watafutane vzr
Wala rushwa mafisadi na wenye biashara haramu si ndio wameishikilia system? Si ndio wamekishikilia chama? Hebu ajaribu kupambana nayo tuone km chama kitabaki salama. Magufuli atakuwa anageuzwageuzwa tu km tingatinga.
 
Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli atakuwa rais lakini watakaokuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwet na Mkapa.

Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

TINGATINGA LAZIMA LIENDESHWE. LISIPOENDESHWA LITALETA MAAFA!
Umenena vyema kuhusu tingatinga, hapo kwenye rangi nyekundu ni kwamba usipoliendesha tingatinga linabaki tu limetulia halifanyi chochote. Ila ukishaanza kuliendesha linakuwa katika hali uliyolielekeza wewe mpaka ulipe maelekezo mengine ndio litabadili kile lilichokuwa linafanya. Dah! hili jina halifai kupewa kiongozi mkuu wa nchi, bora wafikirie lingine. Kama hawatafanya hivyo maana yake wamekubaliana na tafsiri yako.

La kuongezea ni kwamba tingatinga linakodishwa na kutumiwa hasa pale ambapo hali ni ngumu na wale wanaolitumia wakishafunguliwa njia hata lenyewe wanalizuia kupitia njia liliofungua lenyewe. Wao wanatia lami wanaendelea kufurahia wao wenyewe na kulirudisha tingatinga kwa mwenye kulimiliki.
 
TINGATINGA LAZIMA LIENDESHWE. LISIPOENDESHWA LITALETA MAAFA!

Hii statement haina mantiki hata kiduchu.
Tingatinga lisipoendeshwa litaletaje maafa??????
kivipi??

Lisipoendeshwa halina hatari yeyote.
Mtu akiitwa Jembe je utamjadili vipi?

Mtasema mengi sana safari hii.

Mtoa hoja kaelezo hasara zinazoweza kuletwa na tingatina kumkosoa wewe ulitakiwa kutueleza faida tutakazo pata kwa hilo tingatinga au we umeona tu kuwa tingatinga likipaki halitaleta maafa je ulihitaji tingatinga la kupaki je huko kupaki tu sindio hasara yenyewe jadili hoja wacha porojo nivizuri kila mwananchi akawa huru kuwajadili hawa wote wanaomba nafasi za kuwa viongozi wetu maana mwisho wakiwa viongozo kama kuna mateso ni raia watakao kabiliana na mateso hayo na wala sio hao viongozi
 
Its not time for show off ni uwajibikaji tu,wazori mkuu anawekwa kwenye uwaziri mkuu na nani?,usifuate kauri zote,si lazima akushughulikie yeye,anamaanisha waziri mkuu atakayemuweka na baraza la mawaziri kwa ujumla litakuwa mwiba kwa wazembe hivyo hao watendaji unaozungumzia wewe,yeye ndiye anayewateua,hivyo usitegemee ateue baraza la mawaziri legelege,hilo hilo ndilo litakuwa tingatinga kwako mind
 
Sasa wewe ndio umekariri. Unamlinganisha Magufuli na Nyerere? Nyerere alukuwa geniuos na alokuwa na kipawa cha kuongoza cha kuzaliwa. Sasa hebu tuambie Magufuli ktk mda wote aliokaa serkalini ameonesha sifa za kiobgozi? Ana kipawa unachosema cha uongozi? Nimesema Magufuli is very mechanical. Nafasi akizofanyia kazi hazisadifu
Kabisa nature ya urais. Waziri wa barabara waziri wa uvuvi waziri wa nyumba na ardhi. Hizi sio post zinazomtengeneza mtu kuwa rais. Km akichaguliwa Tanzania tutaendelea kuwa na marais mediocre. Kwa mfano ungeniambia kuwalinganisha huko CCM heri Makamba Junior mara 10 kuliko Magufuli.

sawa mkuu sasa hebu tuambie nani anafaa kuwa raisi?
 
Tanzania tunahitaji mtendaji si mtu type unsyodai ya maono,hata asiyena maono hapa kwetu anajifanya mwenye maono ili asikose hiyo nafasi ya urais,watanzania ni wavivu hamuwezi kujiongoza mpaka mkimbizwe mchakamchaka kama enzi za mrema,magufuri anafeet hapo,mliozoea kwenda lunch time 2-3hrs na kuinfia kazini saa 9am,na kuendekeza rushwa kwa kweli mbabidi mkimbie kihama kinakuja na ukumbuke speed ya magufuri itagusa kila idara,kuanzia kijijini mpaka taifa,private companies,government corporations,na mpaka nyumbani kwako,tunaimani na magufuri na yatakuwa tu,hakuna mtu aliyezaliwa na taaluma ya uraisi isipikuwa kusimamia sheria zilizowekwa,na kujua matatizo ya wananchi,nashangaa sana watu wanaom criticize magufuri,jamani tunahitaji kusoma profile za watu si kukurupuka na kushawishi watu uongo kwa yale unayoamini wewe,
Kaka sikatai kwamba tunahitaji kukimbizwa mchakamchaka. Lakini rais hawezi kufanta hiyo kazi. Hiyo ni lazi ya waziri mkuu. Km kina Sokoine na Lowasa walivyofanya. Haya uliyoyaandika hapa sio makukumu ya rais. Magufuli angekuwa waziri mkuu angeiweza sana kazi hiyo. Urais una miiko yake. Uhuru anaokuwa nao waziri mkuu kufanya mambo ni tofauti kabisa na uhuru anaokuwa nao rais.
 
Magufuli hawezi kuwa Magufuli latika nafasi ya Urais. Kutokuwa kwake na uzoefu waambo ya siasa kutamfanya kutojiamini. Kuongoza nchi sio sawa na kujenga barabara au kusimamia wizara. Ni kipaji ambacho Magufuli hana.

Tusubiri UKAWA/Vyama vingine vipitishe wagombea wao ndiyo tuwalinganishe kwa sasa muda bado, pia kumponda wakati wewe hujashika kitu mkononi ni makosa.
 
sawa mkuu sasa hebu tuambie nani anafaa kuwa raisi?
Nadhani kwa upinzani kuna mtu mwenye sifa walau balanced kidogo. Dr Slaa. Huko CCm labda Makamba. Magufuli km akichaguliwa atapata shida sana kufanya kazi km alivyozoea kwa sababu system haitamruhusu. Kumbuka kila anachosema na kufanya rais lazima kihakikiwe. Tofauti na waziri.
 
Wala rushwa mafisadi na wenye biashara haramu si ndio wameishikilia system? Si ndio wamekishikilia chama? Hebu ajaribu kupambana nayo tuone km chama kitabaki salama. Magufuli atakuwa anageuzwageuzwa tu km tingatinga.

mkuu utambue kuwa raisi akiwa dhaifu hata waziri mkuu atakuwa dhaifu na raisi akiwa imara hata mawaziri nao watakuwa imara,

tunahitaji raisi ambaye akisimama kuhimiza jambo watendaji wake lazma waende mbio kulitekeleza.

Mbona mnajihofia sana kwann?
Hata kama itakuja ya kulala saa moja na kuamka saa 10 poa tu.
Tumezidi kufanya kaz kwa mazoea nakuona hata ww hapo unaongelea au unatetea mazoea.
 
Back
Top Bottom