Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Kaka wenzetu japan wamefanikiwa kwa kuchapa kazi,ukiajiriwa japan kwenye kampuni ya tajiri hutamjua mpaka uambiwe maana kama kazi mnapiga ngoma draw hakuna cha boss wala tajiri mnaingia saa mbili kamili wote asubuhi,mnatoka kumi na moja na mbakuwa sawa katika kufanya kazi isipokuwa mshahara,sasa mtu mwajiriwa tajiri anapiga mzigo wewe kwa nini utegee,huo mfano magufuri akiingia front hata wale mawaziri walioteuliwa kama waba vi element vya uvivu watakaa kwenye mstari tu wakiona boss naye anawajibika,na ndito tanzania anatakiwa kiongozi kama huyo,tuache kulewa sifa za kujiita boss unakaa ofisini unaacha kukagua shughuli za serikali,kumbuka waziri mkuu anaweza kuwa strong ila kama raisi ni mpole,waziri mkuu utakosa confidence ya utendaji,chukulia mfano waziri magufuri alivyokuwa anasimamia sheria za barabara,lakini kwa sababu ya upile wa mheshimiwa rausi na mheshimiwa waziri mkuu,magufuri akajikuta anakutana na barrier,lakini yeye akiwa final na akawa ana base kwenye sheria ya nchi hiyo ndiyo njia pekee ya kumfanya mtendaji asimamie sheria si kuoneana aibu,tufike wakati tuwe wakweli na kuelimishana,raisi akiwa strong automaticaly watu wa chini watanyoka tu iwe kwa kujikosha au kweli ili mradi mafanikio na maendeleo yapatikane,kumbuka enzi za marehemu sokoine,na nyerere,kwa sababu marehemu nyerere hakutaka mchezo katika uongozi,sokoine akaonekana mtendaji mzuri sababu boss wake alikuwa naye ni mchapakazi,hata hiyo wizara ya ujenzi sasa hivi huwezi kuta ujinga ujinga,maana waziri wake magufuri ni mchapakazi,akamteua mr mfugale kama ceo wa tanroads,naye ni mchapakazi na wanakuwa kama team ndiyo maana unaona wakandarasi wa barabara hawaleti ujinga,jamani hebu tuwe wakweli na tusifie kitu kinapistahili,magufuri surely ataleta mabadiliko makubwa,na mfano uliotolewa wa bulldozer kuendeshwa na mtu mwingine nafikiri haufai ktk hilo
 
aaah kuruka ruka kwa maharage ndo kuiva kwake bwana,,, na by the way mbona huyu jamaa mnamgwaya sana??
Hatumgwai kaka tunachambua tu udhaifu na ubora wake. Kumchambua mgombea sio kumwogopa ni kusaidoa jamii pana imwelewe zaidi. Ulitka tusimjadili kabisa? Tutakuwa watu wa aina gani. Tutamjadili sana na tutaendelea kuanika mabaya yake na mazuri yake. Si anaitaka ofisi kuu ya nchi bwana. Lazima aanikwe.
 
Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli atakuwa rais lakini watakaokuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwet na Mkapa.

Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

TINGATINGA LAZIMA LIONGOZWE LISIPOONGOZWA VIZURI LITALETA MAAFA!

Ni Ukweli mtupu CCM iondoke ila nataka kujua mbona Kikwete alikuwa mchumi ila mambo yameyumba na Mkapa alikuwa mwanahabari ila kwa kiasi kidogo alijitahidi.
 
Isipokuwa hajasema Tanzania inahitaji nani kazi ya kiongozi na mtendaji. Kuna mmoja ambaye nchi inamhitaji kwa sasa.

Tunahitaji ambaye yuko balanced. Awe na sifa za kiuongozi na kiutendaji. Magufi ni pure mtendaji hana sifa za kiuongozi.
 
Nimemkumbuka ndugu Charles Keenja akiwa mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam alifanya kazi kubwa sana ya kuliweka jiji likawa safi na kiukweli alichapa kazi. Akanogewa akagombea ubunge wa Ubungo akapata na kupewa uwaziri wa kilimo na chakula. Alishindwa wizara ile kabisa. So kuna watu wanaweza micromanagement ukimpeleka kwingine kudeal na macromanagement wanachemsha. Na watu hawa ni wale wenye sifa ya jazba na maamuzi bila tafakari ya kina. Wanashindwa kwa sababu si wavumilivu na wanapenda results ndani ya muda mfupi. Kusubiri muda mrefu kwao ni kama wanashindwa hence wanakata tamaa.
 
Tunahitaji ambaye yuko balanced. Awe na sifa za kiuongozi na kiutendaji. Magufi ni pure mtendaji hana sifa za kiuongozi.

mkuu ww utakuwa una hisa na rushwa,ufisadi au uvivu kazn ndio maana humpendi magufuli...
Yaan mpaka unakuja uwataja akina january makamba ambao hawajui na hawana lolote ndan ya utendaji wala uongozi.

Kweli magufuli ni mti wenye matunda.
 
Nimemkumbuka ndugu Charles Keenja akiwa mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam alifanya kazi kubwa sana ya kuliweka jiji likawa safi na kiukweli alichapa kazi. Akanogewa akagombea ubunuge wa Ubungo akapata na kupewa uwaziri wa kilimo na chakula. Alishindwa wizara ile kabisa. So kuna watu wanaweza micromanagement ukimpeleka kwingine kudeal na macromanagement wanachemsha. Na watu hawa ni wale wenye sifa ya jazba na maamuzi bila tafakari ya kina. Wanashindwa kwa sababu si wavumilivu na wanapenda results ndani ya muda mfupi. Kusubiri muda mrefu kwao ni kama wanashindwa hence wanakata tamaa.

Sawa kabisa mkuu kufanikiwa kuongoza wizara ni tofauti na kupewa linchi. Kuongoza nchi kunataka busara kubwa na utulivu. Magufuli juzi katukamatia lile limeli la uvuvi tukamsifu kweli kumbe alikurupukaka. Leo tunatakiwa kulipa fidia ya 13 bilioni.
 
mkuu ww utakuwa una hisa na rushwa,ufisadi au uvivu kazn ndio maana humpendi magufuli...
Yaan mpaka unakuja uwataja akina january makamba ambao hawajui na hawana lolote ndan ya utendaji wala uongozi.



Kweli magufuli ni mti wenye matunda.

Kaka nikuhakikishie Magufuli nampenda sana ni mchapa kazi. Lakini nafasi ya urais ni too much kwake. Angekuwa waziri mkuu angetukamata vizuri zaidi sisi wazembe, wala rushwa na wavivu. Infact kumweka pale juu ni kumnyima fursa hii. Magufuli hana sifa za kuwa rais inaonekana ccm wameishiwa kabisa. Hivi zile sifa 13 alizotaja Mangula Magufuli anazo ngapi vile?
 
by the way mkitisha watu wapinzani wanaweza kuitumia hoja yako kwa watu maskini kwamba Magufuli hana huruma kwa wanyinge amekuwa anabomoa nyumba za watu bila kufuata taratibu na wakakubaliana nalo. Si mnasema ni mtu wa kufuata sgeria km zilivyo? Imagine nwendesha bodaboda mamantilie na machinga ambao wengi wanaishi kwa kutafuta rizki ktk maeneo yasiyokubalika kisheria? Mnachokiona ni strenght ya Magufuli wengine wanaweza wakaidanya ionekane ni weakness kwa wapiga kura maskini km niliowataja hapo juu.

mkuu waliotunga hizo sheria mnazotaka jamaa asizisimamie walikua smart sana zaid yako we na mimi na mwisho wa siku ukiitafakari hii kwa mapana yake utaja gundua kuwa hizi sheria ni muhimu mara mia zaid ya hawa mama ntilie na mabodaboda,,, usiposimamia sheria kesho kuna watanzania watajenga nyumba za kupangisha katikati ya barabara ama round about na wanapogongwa hawa waliojenga barabarani ni hasara zaidi kuliko kuwaondoa mapema! kama unatoa tu kasoro for that sake basi sina tatizo na wewe
 
Mkuu ukumbuke hata lowasa alikuwa mtendaji mzuri lakn udhaifu wa raisi ndio ukamponza mpaka yanamfika haya...
Mtu kama magufuli akiwa raisi halafu wazir mkuu akawa mwakyembe hapo mafisadi na waivu watajuta kuzaliwa tanzania


Kaka nikuhakikishie Magufuli nampenda sana ni mchapa kazi. Lakini nafasi ya urais ni too much kwake. Angekuwa waziri mkuu angetukamata vizuri zaidi sisi wazembe, wala rushwa na wavivu. Infact kumweka pale juu ni kumnyima fursa hii. Magufuli hana sifa za kuwa rais inaonekana ccm wameishiwa kabisa. Hivi zile sifa 13 alizotaja Mangula Magufuli anazo ngapi vile?
 
Mkuu nchi haiendeshwi kwa kuangalia mafisadi na wavivu tu. Ukiwa mkuu wa nchi unatakiwa uwe na vision ya wapi unataka nchi ielekee kiuchumi, kisiasa, kijamii, kielimu, kiutamaduni nk. Utendaji wa kukurupuka mara nyingi unaweza kukiuka haki za binadamu so twahitaji raisi mwenye utulivu wa akili, mwenye hekima na maamuzi yenye tija, na mtu mwenye kuboresha mahusiano na jirani zake, mwenye uzoefu wa kimataifa na kujua mabadiliko katika dunia.
 
Mkuu ukumbuke hata lowasa alikuwa mtendaji mzuri lakn udhaifu wa raisi ndio ukamponza mpaka yanamfika haya...
Mtu kama magufuli akiwa raisi halafu wazir mkuu akawa mwakyembe hapo mafisadi na waivu watajuta kuzaliwa tanzania

Aliyemuangusha JK ni Pinda kwa kukosa maamuzi kila Jambo kwake mpaka apewe maelekezo.
 
Mara 50 JK kuliko Magufuli!!! mark my words siku moja utaniambia!!!

Hana mvuto wakuwa alama ya umoja wa Taifa.

Kikwete mpaka sasa hakuna mfano wake kwa waliopita na huyu ataekuja inawezekana kabisa kuwa Kikwete ni juu yake kwa sana tu.

Hilo nnakubaliana na wewe.
 
Si mpaka uingie kwenye uongozi ndiyo utajulikana uwezo wako,nani alijua ben anaweza kuitoa nchi ilipokuwa toka kwa mzee mwinyi na kuifikisha pale ilipofika,jamani suluhisho watanzania tuache uvivu,hata magufuri akiingia kama bulldozer wananchi mkawa mnapiga story za kina lowasa na simba na yanga hamtafika popote zaidi ya kulaumu na kusingizia mambo
 
Back
Top Bottom