Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Kaka wenzetu japan wamefanikiwa kwa kuchapa kazi,ukiajiriwa japan kwenye kampuni ya tajiri hutamjua mpaka uambiwe maana kama kazi mnapiga ngoma draw hakuna cha boss wala tajiri mnaingia saa mbili kamili wote asubuhi,mnatoka kumi na moja na mbakuwa sawa katika kufanya kazi isipokuwa mshahara,sasa mtu mwajiriwa tajiri anapiga mzigo wewe kwa nini utegee,huo mfano magufuri akiingia front hata wale mawaziri walioteuliwa kama waba vi element vya uvivu watakaa kwenye mstari tu wakiona boss naye anawajibika,na ndito tanzania anatakiwa kiongozi kama huyo,tuache kulewa sifa za kujiita boss unakaa ofisini unaacha kukagua shughuli za serikali,kumbuka waziri mkuu anaweza kuwa strong ila kama raisi ni mpole,waziri mkuu utakosa confidence ya utendaji,chukulia mfano waziri magufuri alivyokuwa anasimamia sheria za barabara,lakini kwa sababu ya upile wa mheshimiwa rausi na mheshimiwa waziri mkuu,magufuri akajikuta anakutana na barrier,lakini yeye akiwa final na akawa ana base kwenye sheria ya nchi hiyo ndiyo njia pekee ya kumfanya mtendaji asimamie sheria si kuoneana aibu,tufike wakati tuwe wakweli na kuelimishana,raisi akiwa strong automaticaly watu wa chini watanyoka tu iwe kwa kujikosha au kweli ili mradi mafanikio na maendeleo yapatikane,kumbuka enzi za marehemu sokoine,na nyerere,kwa sababu marehemu nyerere hakutaka mchezo katika uongozi,sokoine akaonekana mtendaji mzuri sababu boss wake alikuwa naye ni mchapakazi,hata hiyo wizara ya ujenzi sasa hivi huwezi kuta ujinga ujinga,maana waziri wake magufuri ni mchapakazi,akamteua mr mfugale kama ceo wa tanroads,naye ni mchapakazi na wanakuwa kama team ndiyo maana unaona wakandarasi wa barabara hawaleti ujinga,jamani hebu tuwe wakweli na tusifie kitu kinapistahili,magufuri surely ataleta mabadiliko makubwa,na mfano uliotolewa wa bulldozer kuendeshwa na mtu mwingine nafikiri haufai ktk hilo
 
aaah kuruka ruka kwa maharage ndo kuiva kwake bwana,,, na by the way mbona huyu jamaa mnamgwaya sana??
Hatumgwai kaka tunachambua tu udhaifu na ubora wake. Kumchambua mgombea sio kumwogopa ni kusaidoa jamii pana imwelewe zaidi. Ulitka tusimjadili kabisa? Tutakuwa watu wa aina gani. Tutamjadili sana na tutaendelea kuanika mabaya yake na mazuri yake. Si anaitaka ofisi kuu ya nchi bwana. Lazima aanikwe.
 

Ni Ukweli mtupu CCM iondoke ila nataka kujua mbona Kikwete alikuwa mchumi ila mambo yameyumba na Mkapa alikuwa mwanahabari ila kwa kiasi kidogo alijitahidi.
 
Isipokuwa hajasema Tanzania inahitaji nani kazi ya kiongozi na mtendaji. Kuna mmoja ambaye nchi inamhitaji kwa sasa.

Tunahitaji ambaye yuko balanced. Awe na sifa za kiuongozi na kiutendaji. Magufi ni pure mtendaji hana sifa za kiuongozi.
 
Nimemkumbuka ndugu Charles Keenja akiwa mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam alifanya kazi kubwa sana ya kuliweka jiji likawa safi na kiukweli alichapa kazi. Akanogewa akagombea ubunge wa Ubungo akapata na kupewa uwaziri wa kilimo na chakula. Alishindwa wizara ile kabisa. So kuna watu wanaweza micromanagement ukimpeleka kwingine kudeal na macromanagement wanachemsha. Na watu hawa ni wale wenye sifa ya jazba na maamuzi bila tafakari ya kina. Wanashindwa kwa sababu si wavumilivu na wanapenda results ndani ya muda mfupi. Kusubiri muda mrefu kwao ni kama wanashindwa hence wanakata tamaa.
 
Tunahitaji ambaye yuko balanced. Awe na sifa za kiuongozi na kiutendaji. Magufi ni pure mtendaji hana sifa za kiuongozi.

mkuu ww utakuwa una hisa na rushwa,ufisadi au uvivu kazn ndio maana humpendi magufuli...
Yaan mpaka unakuja uwataja akina january makamba ambao hawajui na hawana lolote ndan ya utendaji wala uongozi.

Kweli magufuli ni mti wenye matunda.
 

Sawa kabisa mkuu kufanikiwa kuongoza wizara ni tofauti na kupewa linchi. Kuongoza nchi kunataka busara kubwa na utulivu. Magufuli juzi katukamatia lile limeli la uvuvi tukamsifu kweli kumbe alikurupukaka. Leo tunatakiwa kulipa fidia ya 13 bilioni.
 
mkuu ww utakuwa una hisa na rushwa,ufisadi au uvivu kazn ndio maana humpendi magufuli...
Yaan mpaka unakuja uwataja akina january makamba ambao hawajui na hawana lolote ndan ya utendaji wala uongozi.



Kweli magufuli ni mti wenye matunda.

Kaka nikuhakikishie Magufuli nampenda sana ni mchapa kazi. Lakini nafasi ya urais ni too much kwake. Angekuwa waziri mkuu angetukamata vizuri zaidi sisi wazembe, wala rushwa na wavivu. Infact kumweka pale juu ni kumnyima fursa hii. Magufuli hana sifa za kuwa rais inaonekana ccm wameishiwa kabisa. Hivi zile sifa 13 alizotaja Mangula Magufuli anazo ngapi vile?
 

mkuu waliotunga hizo sheria mnazotaka jamaa asizisimamie walikua smart sana zaid yako we na mimi na mwisho wa siku ukiitafakari hii kwa mapana yake utaja gundua kuwa hizi sheria ni muhimu mara mia zaid ya hawa mama ntilie na mabodaboda,,, usiposimamia sheria kesho kuna watanzania watajenga nyumba za kupangisha katikati ya barabara ama round about na wanapogongwa hawa waliojenga barabarani ni hasara zaidi kuliko kuwaondoa mapema! kama unatoa tu kasoro for that sake basi sina tatizo na wewe
 
Mkuu ukumbuke hata lowasa alikuwa mtendaji mzuri lakn udhaifu wa raisi ndio ukamponza mpaka yanamfika haya...
Mtu kama magufuli akiwa raisi halafu wazir mkuu akawa mwakyembe hapo mafisadi na waivu watajuta kuzaliwa tanzania


 
Mkuu nchi haiendeshwi kwa kuangalia mafisadi na wavivu tu. Ukiwa mkuu wa nchi unatakiwa uwe na vision ya wapi unataka nchi ielekee kiuchumi, kisiasa, kijamii, kielimu, kiutamaduni nk. Utendaji wa kukurupuka mara nyingi unaweza kukiuka haki za binadamu so twahitaji raisi mwenye utulivu wa akili, mwenye hekima na maamuzi yenye tija, na mtu mwenye kuboresha mahusiano na jirani zake, mwenye uzoefu wa kimataifa na kujua mabadiliko katika dunia.
 
Mkuu ukumbuke hata lowasa alikuwa mtendaji mzuri lakn udhaifu wa raisi ndio ukamponza mpaka yanamfika haya...
Mtu kama magufuli akiwa raisi halafu wazir mkuu akawa mwakyembe hapo mafisadi na waivu watajuta kuzaliwa tanzania

Aliyemuangusha JK ni Pinda kwa kukosa maamuzi kila Jambo kwake mpaka apewe maelekezo.
 
Mara 50 JK kuliko Magufuli!!! mark my words siku moja utaniambia!!!

Hana mvuto wakuwa alama ya umoja wa Taifa.

Kikwete mpaka sasa hakuna mfano wake kwa waliopita na huyu ataekuja inawezekana kabisa kuwa Kikwete ni juu yake kwa sana tu.

Hilo nnakubaliana na wewe.
 
Si mpaka uingie kwenye uongozi ndiyo utajulikana uwezo wako,nani alijua ben anaweza kuitoa nchi ilipokuwa toka kwa mzee mwinyi na kuifikisha pale ilipofika,jamani suluhisho watanzania tuache uvivu,hata magufuri akiingia kama bulldozer wananchi mkawa mnapiga story za kina lowasa na simba na yanga hamtafika popote zaidi ya kulaumu na kusingizia mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…