Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Makala yako ni nzuri lakini umeiandika kana kwamba Magufuli anasubiri kuapishwa tu
Yani kama vile hakuna mchakato mwingine mbele yake ambao haiyumkini ndio ukawa mwisho wake na chama chake kuliongoza taifa hili
Msijisahau rais wa nchi hii hachaguliwi na NEC ya ccm anachaguliwa na watanzania wote.
Sasa waweza kubaliana na mimi kuwa watz wengi kutokana na kujiaminisha kuwa wajinga ndio watakaopiga kura hivyo Rais lazima atatoka ccm!
 
Nadhani kwa upinzani kuna mtu mwenye sifa walau balanced kidogo. Dr Slaa. Huko CCm labda Makamba. Magufuli km akichaguliwa atapata shida sana kufanya kazi km alivyozoea kwa sababu system haitamruhusu. Kumbuka kila anachosema na kufanya rais lazima kihakikiwe. Tofauti na waziri.

unaweza kunipa mifano hai ya utendaji bora ya Dr slaa mpaka tumwamini kumpa nchi?

Makamba anauongozi gani ambao unakupa iman ya kushika wadhifa mkubwa kias hicho?
Wakat hata ndan ya siasa ana awamu moja tu?
 
Its not time for show off ni uwajibikaji tu,wazori mkuu anawekwa kwenye uwaziri mkuu na nani?,usifuate kauri zote,si lazima akushughulikie yeye,anamaanisha waziri mkuu atakayemuweka na baraza la mawaziri kwa ujumla litakuwa mwiba kwa wazembe hivyo hao watendaji unaozungumzia wewe,yeye ndiye anayewateua,hivyo usitegemee ateue baraza la mawaziri legelege,hilo hilo ndilo litakuwa tingatinga kwako mind
Dhubutu miaka mitano ya kwanza km akipita atakuwa anachaguliwa baraza na hawa wazee. Hawawezi kumwacha achague mwenyewe kwa sababu wanajua udhaifu wake. By the way hao mawaziri wa kuiendesha nchi mcjamchaka huko ccm ndio watapatikana leo? Magufuli anaenda kuwanunua wapi?
 
Makala yako ni nzuri lakini umeiandika kana kwamba Magufuli anasubiri kuapishwa tu
Yani kama vile hakuna mchakato mwingine mbele yake ambao haiyumkini ndio ukawa mwisho wake na chama chake kuliongoza taifa hili
Msijisahau rais wa nchi hii hachaguliwi na NEC ya ccm anachaguliwa na watanzania wote.

NDugu yangu umenena vema zaid ya 200%, tatizo ni wachache wanaolielewa hili, weng wetu tumekalili kwamba CCM wakiteua mgombea raisi,basi ndiye raisi moja kwa moja kana kwamba Uraisi kwa CCM ni mali yao wao tu.
 
Its not time for show off ni uwajibikaji tu,wazori mkuu anawekwa kwenye uwaziri mkuu na nani?,usifuate kauri zote,si lazima akushughulikie yeye,anamaanisha waziri mkuu atakayemuweka na baraza la mawaziri kwa ujumla litakuwa mwiba kwa wazembe hivyo hao watendaji unaozungumzia wewe,yeye ndiye anayewateua,hivyo usitegemee ateue baraza la mawaziri legelege,hilo hilo ndilo litakuwa tingatinga kwako mind

mkuu eid hii utapenda kutumia kinywaji gani?? watu wamekaa kupotosha eti rais hana uwezo wa kupambana na watendaji wabovu sasa mi najiuliza kama hana mamlaka hayo anakuepo ili iweje sasa? kwani team ikicheza ovyo kwanini afukuzwe kocha wakati hua haingii uwanjani kucheza?
 
Dhubutu miaka mitano ya kwanza km akipita atakuwa anachaguliwa baraza na hawa wazee. Hawawezi kumwacha achague mwenyewe kwa sababu wanajua udhaifu wake. By the way hao mawaziri wa kuiendesha nchi mcjamchaka huko ccm ndio watapatikana leo? Magufuli anaenda kuwanunua wapi?

ikilazimika baraza zima litapatikana kwa mtindo aliopatikana prof. Muhongo kama hiyo ndo shida yako
 
Mtoa hoja kaelezo hasara zinazoweza kuletwa na tingatina kumkosoa wewe ulitakiwa kutueleza faida tutakazo pata kwa hilo tingatinga au we umeona tu kuwa tingatinga likipaki halitaleta maafa je ulihitaji tingatinga la kupaki je huko kupaki tu sindio hasara yenyewe jadili hoja wacha porojo nivizuri kila mwananchi akawa huru kuwajadili hawa wote wanaomba nafasi za kuwa viongozi wetu maana mwisho wakiwa viongozo kama kuna mateso ni raia watakao kabiliana na mateso hayo na wala sio hao viongozi

acheni kubadili maana wakat mnajua maan.
Wote hapa tunajua kaz ya tingatinga kuwa kazi yake ni kung'o au kusafisha au kurekebhisha sehem yoyote korofi.

Hilo tingatinga kama nyumba sehem isyofaa litasambaratisha tu.

Hyo ni kutokana na maelekezo ya mwongozaji
 
unaweza kunipa mifano hai ya utendaji bora ya Dr slaa mpaka tumwamini kumpa nchi?

Makamba anauongozi gani ambao unakupa iman ya kushika wadhifa mkubwa kias hicho?
Wakat hata ndan ya siasa ana awamu moja tu?

Ndio ulichoonesha japa lwamba Ccm walikuwa hawajaandaa mtu ndio maana wakaja na tingatinga. Na kwa sasa hakuna mtu huko Ccm aliyemsafi.Imagine kwamba Makamba ndiye nimemwona km ana nafuu. Maana yake hakuna mtu huko. By the way uongozi ni busara na kipaji huitaji uwe na rekodi. Elimu ya kawaida ya kutosha na busara tu vinatosha. Dr Slaa anavyo hata Makamba. Nyerere alipochukua nchi hakuwa na rekodi yoyote. Lakini alikuwa kiongozi by nature. Hili Maguful hana.
 
Sasa wewe ndio umekariri. Unamlinganisha Magufuli na Nyerere? Nyerere alukuwa geniuos na alokuwa na kipawa cha kuongoza cha kuzaliwa. Sasa hebu tuambie Magufuli ktk mda wote aliokaa serkalini ameonesha sifa za kiobgozi? Ana kipawa unachosema cha uongozi? Nimesema Magufuli is very mechanical. Nafasi akizofanyia kazi hazisadifu
Kabisa nature ya urais. Waziri wa barabara waziri wa uvuvi waziri wa nyumba na ardhi. Hizi sio post zinazomtengeneza mtu kuwa rais. Km akichaguliwa Tanzania tutaendelea kuwa na marais mediocre. Kwa mfano ungeniambia kuwalinganisha huko CCM heri Makamba Junior mara 10 kuliko Magufuli.

inaelekea baba ako kajenga nyumba kwenye road reserve,, mkuu huu muda unaopoteza hum jf mngetafuta tu sehem nyingine ya kukaa kabla jk hajampisha gongo kwenye steering wheel manake,,,
 
acheni kubadili maana wakat mnajua maan.
Wote hapa tunajua kaz ya tingatinga kuwa kazi yake ni kung'o au kusafisha au kurekebhisha sehem yoyote korofi.

Hilo tingatinga kama nyumba sehem isyofaa litasambaratisha tu.

Hyo ni kutokana na maelekezo ya mwongozaji

Kumbe unapenda kuminyani sasa mbona umejaa povu mdomoni matokeo ya kazi ya tingatinga ni dereva je wamjua dereva?????
 
Mwongozaji wa tingatinga ni nani sasa? Magufuli ndio tingatinga. Nani mwongozaji wake? Faiza Fox kasema ni ccm. Lakini ni Ccm hii iliyofeli miaka yote hii ndio leo itaweza kuliongoza tingatinga lisafishe vizuri?
 
Ndio ulichoonesha japa lwamba Ccm walikuwa hawajaandaa mtu ndio maana wakaja na tingatinga. Na kwa sasa hakuna mtu huko Ccm aliyemsafi.Imagine kwamba Makamba ndiye nimemwona km ana nafuu. Maana yake hakuna mtu huko. By the way uongozi ni busara na kipaji huitaji uwe na rekodi. Elimu ya kawaida ya kutosha na busara tu vinatosha. Dr Slaa anavyo hata Makamba. Nyerere alipochukua nchi hakuwa na rekodi yoyote. Lakini alikuwa kiongozi by nature. Hili Maguful hana.

mkuu unakwepa swaali nataka unambie kuwa Dr slaa kafanya haya hata kama ni ndan ya chama chake, na huyo makamba unambie ni nn kafanya kipind chake cha utendaji.
Uwanja wako mzee tiririka
 
Rais ndiye mwenye Serikali ndiye muamuzi wa mwisho yeye ndiye anaamua serikali yake iwe lege lege au vinginevyo, lawama au sifa zitakwenda kwake mwisho wa siku.

Pinda ni Waziri mkuu lege lege kuwahi kutokea ktk nchi yetu ndiye amefanya JK aonekane hivi anavyoonekana, hana maamuzi kichwa wazi kila kitu mpaka aambiwe tukumbuke kisa cha Jairo.

Magufuri kama akishinda na akamteua Waziri mkuu Jembe na akawa anafuatilia utendaji wa Serikali yake atakua kiongozi bora sana.

Mfano wa Watu wanaofaa ni Lukuvi, Pesa akamate kijana wa Singida, Uchukuzi Mwakyembe, Elimu Majaliwa na Kilimo akarudi Mzee wa kutofautisha Vifungo.....
Wizara nyingine hazina Shida sana.
Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli atakuwa rais lakini watakaokuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwet na Mkapa.

Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

TINGATINGA LAZIMA LIONGOZWE LISIPOONGOZWA VIZURI LITALETA MAAFA!
 
inaelekea baba ako kajenga nyumba kwenye road reserve,, mkuu huu muda unaopoteza hum jf mngetafuta tu sehem nyingine ya kukaa kabla jk hajampisha gongo kwenye steering wheel manake,,,

Mimi mwenyewe baba. Yaani wewe unataka kuniambia matatizo ya hii nchi yametokana na watu kujenga kwenye road reserve? Mlikuwa wapi mpaka watu wajenge kwenye road reserve?
 
Hahaha. Sasa kaka rais ana nafasi kumi tu mawaziri wanahitajika zaidi ya 30.

ujue wengi wetu hua tunachukulia mamlaka ya rais wa nchi kama yale ya jamal malinzi ama ya yasin abdallah "ustadhi" wa tpbo! amini nakwambia rais wa nchi ana uwezo wa kufanya chochote anachokitaka na halazimiki kutoa justification ya maamuzi yake kwa MTU YEYOTE...
 
Kumbe unapenda kuminyani sasa mbona umejaa povu mdomoni matokeo ya kazi ya tingatinga ni dereva je wamjua dereva?????

sasa subiri kijana utajua maana halisi ya tingatinga likianza kufanya kazi.
 
Mimi mwenyewe baba. Yaani wewe unataka kuniambia matatizo ya hii nchi yametokana na watu kujenga kwenye road reserve? Mlikuwa wapi mpaka watu wajenge kwenye road reserve?

aaah kuruka ruka kwa maharage ndo kuiva kwake bwana,,, na by the way mbona huyu jamaa mnamgwaya sana??
 
NDugu yangu umenena vema zaid ya 200%, tatizo ni wachache wanaolielewa hili, weng wetu tumekalili kwamba CCM wakiteua mgombea raisi,basi ndiye raisi moja kwa moja kana kwamba Uraisi kwa CCM ni mali yao wao tu.

Ndugu yangu CCM tayari wana mgombea wameanza kampeni/kumtambulisha mikoa mbali mbali kwa hiyo wana faida mkononi kabla ya tarehe 22/8 UKAWA bado wanabishana unategemea kweli wako serious?
 
Mimi mwenyewe baba. Yaani wewe unataka kuniambia matatizo ya hii nchi yametokana na watu kujenga kwenye road reserve? Mlikuwa wapi mpaka watu wajenge kwenye road reserve?
by the way mkitisha watu wapinzani wanaweza kuitumia hoja yako kwa watu maskini kwamba Magufuli hana huruma kwa wanyinge amekuwa anabomoa nyumba za watu bila kufuata taratibu na wakakubaliana nalo. Si mnasema ni mtu wa kufuata sgeria km zilivyo? Imagine nwendesha bodaboda mamantilie na machinga ambao wengi wanaishi kwa kutafuta rizki ktk maeneo yasiyokubalika kisheria? Mnachokiona ni strenght ya Magufuli wengine wanaweza wakaidanya ionekane ni weakness kwa wapiga kura maskini km niliowataja hapo juu.
 
Back
Top Bottom