Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magufuli amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebehi kumtukana na kumsema vibaya.

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wake waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lakini hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magufuli hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magufuli huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahiyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahali zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uongo una mwisho wake uongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magufuli bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango wa kutokea.

inasikitisha sana ipo
siku wa tanzania dhambi ya libya itawakuta kwa maovu yao
 
Sasa mtu aliyetangulia mbele ya haki unamtetea kwa maslahi ya nani mkuu.
Sasa hivi anajitetea mwenyewe huko aliko, Cha msingi marehemu huwa hasemwi vibaya , hata Kama kuna mabaya alifanya cha msingi ni kuendelea kumuombea ili muumba ampunguzie adhabu tu kwa mabaya aliyofanya.

nyerere mbona mnamtetea kadhulumu nyumba za watu na kuwa NHC ukiona nyumba ina alama hiyo kumbuka mwenye nyumba alizulumiwa na nyerere nakuwa nhc wengi walikufa kwa presha lakini hasemwi
 
Watetezi wa Magufuli
2773061_FB_IMG_1620925066257.jpg
 
Ilikua ni huzuni kila mtu akipata nafasi ya kuongea "Namshukuru Rais wa serikali ya awamu ya tano, serikali isiyo ya mchezo mchezo" hata kujenga hoja ilikua dhambi ni kusifia tu
Wote wakageuka kuwa vilema wa akili.😂
 
nyerere mbona mnamtetea kadhulumu nyumba za watu na kuwa NHC ukiona nyumba ina alama hiyo kumbuka mwenye nyumba alizulumiwa na nyerere nakuwa nhc wengi walikufa kwa presha lakini hasemwi
Walinyang'anywaje?Mbona ndiyo haohao wanaendelea kuishi kwa wingi na kurithishana hizo nyumba wenyewe kwa wenyewe?Halafu kodi ndogo ajabu!
 
Wanaomchukia Magufuli👇
-Waliotumbuliwa vyeti fake
-Wafanyakazi hewa
-Wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-Viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-Wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-Mabeberu wapenda dezo za taifa
-Wezi waliotaka JPM nae aungane nao ili waibe wote
Sipo kwenye hayo makundi na sijawahi kumwelewa! Hakuwa kiongozi sahihi. Mkurupukaji, mjuaji, hashauriki, mkali bila sababu, mbinafsi.
 
Sasa mtu aliyetangulia mbele ya haki unamtetea kwa maslahi ya nani mkuu.
Sasa hivi anajitetea mwenyewe huko aliko, Cha msingi marehemu huwa hasemwi vibaya , hata Kama kuna mabaya alifanya cha msingi ni kuendelea kumuombea ili muumba ampunguzie adhabu tu kwa mabaya aliyofanya.
Kama tulimwomba mungu ili afe, ujasiri wa kumuombea tutautoa wapi.

Mtu muuwaji, mtekaji mwizi na mporaji was Mali za umma unamwombeaje Kwa mfano.

Alikataa hata kuchangiwa damu wenzake alioamrisha wauwawe yeye tunamwombeaje.

Huko kuzimu tunaomba popobawa amfire ajue tuliopo duniani hatukupenda tabie zake za uuwaji.

Kauwa wengi bila sababu.

Mungu amuongezee adhabu
 
nimekwambia kapandishe kalio mtaani anza kumponda uone kitakachokupata,hata kama ni mzoefu wa kutofuliwa lazima cha moto utakiona.

haijalishi una uzoefu field hiyo kwa muda gani.
Mtaani namponda sana, nyumbu kama nyie hamna lolote la kufanya, Samia aliwafagia mtaani kwani mlifanya nini?
 
Wanaomchukia Magufuli👇
-Waliotumbuliwa vyeti fake
-Wafanyakazi hewa
-Wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-Viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-Wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-Mabeberu wapenda dezo za taifa
-Wezi waliotaka JPM nae aungane nao ili waibe wote
Hizi ngonjera zilisha enda nae bwashee bado tu unazikumbuka? 😆😆
 
Tutajie mtawala aliyefikia hadi hatua ya kujifananisha na Malaika.

Akifika huko ataongoza Malaika.
Hakukuwa na utawala wa sheria Wala kanuni achilia mbali misingi ya haki.

Watu walitekwa na kuuwawa si kwa kificho
Vikundi vya watu wasiojulikana walitamalaki.
Maiti ziliokotwa kwenye viroba na watu walipo hoji wakaambiwa ni wahamiaji haramu.
Je Wana haki ya kuuwawa?

Hofu ilitanda kila sehemu, sio mitaani Wala kwenye miji.
Watu wachache wakajitwalia ukwasi wa kutisha na wengi wakafuata mkumbo.

Miradi haikufuata sheria ya fedha ya mwaka husika yaani appropriation act ila ikawa one man's show.

Ajira hazikutolewa kiasi Cha kupoteza na kutweza Vijana wa nchi hii.
Mfumo wa Biashara uliyumba maana waliokuwa na fedha basi waliwajua Financial Intelligence Unit

Mfumo wa uchumi ulianguka mpaka mabenki kufilisika.
Purchasing power kwa Mtanzania mmoja mmoja ilianguka kiasi Cha kushindwa wabongo kumudu Milo mitatu.

Kutumika nguvu kubwa kwenye ukusanyaji wa mapato na kubambikiwa watu Kodi kubwa kubwa zisizo na uhalisia.

Kudhalilisha kundi la wasomi na taaluma mbalimbali kwa wanasiasa wanaojifanya kujua kila kitu.

Kuminywa na kutozingatiwa kwa stahiki na maslahi ya Wafanyakazi wa nchi hii ikiwemo kutopandishwa kwa mishahara kwa miaka yote alipoongoza.

Kuharibiwa kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kiasi Cha watoto wengi wa familia fukara kushindwa kuendelea na masomo.

Biashara za mazao kufa kipindi chake, chukua tukio la Korosho za Mtwara na Lindi.
Zao la Ufuta
Kilimo Cha mahindi kule Sumbawanga, Nyanya pale Iringa

Kifupi hakuwa na jema ila jiulize kwa nini waliipenda force account itumike kwenye miradi ambayo haikuidhinishwa na Bunge?

Kwa nini walimdisicredit report ya CAG na kazi yake?

Kwa nini hawakutumia Competitive tendering kwenye kupata mzabuni wa Ile miradi?

Kwa nini waliotumika chini yake Vijana wakawa matajiri ghafra?

Kwa nini alidharau Wazee kama mzee Warioba na Wastahafu wengine?
Alifa recruitment ya machawa wengi kutoka Kanda ya ziwa ikawa tabu tupu kila sehemu yaani kazini mpaka mtaani.

Kuna mtu anaitwa George Makoye Nyengo, huyo alisimamia kukusanya umbea eneo la mbezi stand mpaka mlandizi pwani.

Yaani yule alikuwa shetani kabisa hakustahili kuwepo ikulu
 
Kama tulimwomba mungu ili afe, ujasiri wa kumuombea tutautoa wapi.

Mtu muuwaji, mtekaji mwizi na mporaji was Mali za umma unamwombeaje Kwa mfano.

Alikataa hata kuchangiwa damu wenzake alioamrisha wauwawe yeye tunamwombeaje.

Huko kuzimu tunaomba popobawa amfire ajue tuliopo duniani hatukupenda tabie zake za uuwaji.

Kauwa wengi bila sababu.

Mungu amuongezee adhabu
Dah!Jamani tupunguze hasira.Yatosha!😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂🙏🙏🙏
 
Pia ile sifa yake nyingine kubwa ya ujasiri wa kutenda uovu dhidi ya raia, tena bila woga: kuua, kushambulia, kuteka, kutesa na kuwabambikia watu kesi kisha kuwanyang'anya pesa, na pesa alizowanyanga kuzitia mfukoni mwake bila ya hofu ya kuhojiwa chochote na yeyote. Ule ni ujasiri wa pekee ambao lazima utetewe.

Mkuu mie naumia sana.

Nafikiri tupiganie katiba mpya Ili watu waovu kama magufuri hats kama amekufa afikishwe mahakamani.

Kauwa watu wengi, kafirisi mitaji ya watu.

Tushukuru mungu
 
Jaribu kuheshimu mchango wake, kama unaona huna hoja yakuichangia hoja yake nyamaza!! Hajazungumza kibaya Ni mawazo na hisia zake zimemsukuma kukumbuka hayo Hana kosa!

Kazikwe nae nikauli gani,, wewe huna umpendae na umempoteza na unamkumbuka kwa matendo yake?? Ulishawahi kuwaza kuzikwa nae kwasababu hiyo!!!?

Wakati mwingine hata kama mnatumia ID ya uwongo basi mawazo yenu yafanye yawe yakweli.. hapa nisehem ambayo tunabadilishana mawazo na kupeana habari mbalimbali ila watu mnapageuza kuwa sehemu ya ujinga na upuuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Utaheshimu mchongo wa kuuwa watu? Mbunge kupigwa risasi kunyimwa pesa ya matibabu pia hata kuchangiwa damu.

Yule abanikwe kama mbwa wa iringa
 
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magufuli amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebehi kumtukana na kumsema vibaya.

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wake waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lakini hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magufuli hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magufuli huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahiyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahali zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uongo una mwisho wake uongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magufuli bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango wa kutokea.
kazikwe naye... ujinga wako unaamini kwamba kazi ya raisi ni kujenga barabara tu,,, hao watu wa kipato cha chini na cha kati aliwatoa wapi kwenda wapi kiuchumi?
 
Back
Top Bottom