Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Kila mtu ana namna ya kipekee ya kupokea matendo aliofanya mtu mwingine hivyo kwenye ulimwengu huu.
Usipoteze muda wako kuwaza anachofanya au kutendewa mtu mwingine ima yu hai au amefariki. Sote tunajua marehemu hasemewi vibaya hata kama alikua jambazi au hata mchawi huwez kuta anaongelewa vibaya ni kukosa malezi tu kunatusumbua japo kua kila mmoja wetu ana namna yake ya kupokea jambo na kulitafsiri kwenye kili yake.

Tungekua tuna akili sisi sio watu w akukaa kungalia mazuri na mabaya ya kiongozi sisii tungetakiwa tusimamie tupate haki zetu kama wananchi tutendewe yale yanayoendana na tulipo sasa hivi ila wengi wetu tunajua kuponda na kuwa machawa.
 
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magu amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebei kumtukana na kumsema vibaya

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wako waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lkn hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magu hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magu huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahari zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uwongo una mwisho wake uwongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magu bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango was kutokea.

Nani amtetee muuaji?. We uliona wapi mtu anakufa watu wanafanya sherehe. Hakika Mungu yupo.
 
Wanaomchukia magufuli
-waliotumbuliwa vyeti fake
-wafanyakazi hewa
-wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-mabeberu wapenda dezo za taifa
-wezi waliotaka jpm nae aungane nao ili waibe wote

Usisahau na familia ya Ben Saanane na Lissu pia.
 
Kuna nyimbo moja ya zamani ina mashairi yanayoimbwa

Kila mtenda wema atakumbukwa kwa wema x2

Ukatili ukatili ni unyama, Mashujaa tutawakumbuka kwa weema

Jibu unalipata ukiitafuta hiyo nyimbo.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app

Kwangu Magufuli nilimuona Kama mtu mmoja mwenye kiburi na mwenye chuki. Kama hakupendi utakiona Cha moto.
 
Acheni kukuza hakuna utawala nchi hii ambao haujaumiza watu, punguzeni kujiliza.

Ubaya wa x hauwezi kuzuia ubaya wa y usijadiliwe. Magufuli alikuwa mwovu Sana. Leo wasiojulikana hawapo au mbunge kupigwa Risasi hadharani.
 
Tutajie mtawala aliyefikia hadi hatua ya kujifananisha na Malaika.

Akifika huko ataongoza Malaika.
Hakukuwa na utawala wa sheria Wala kanuni achilia mbali misingi ya haki.

Watu walitekwa na kuuwawa si kwa kificho
Vikundi vya watu wasiojulikana walitamalaki.
Maiti ziliokotwa kwenye viroba na watu walipo hoji wakaambiwa ni wahamiaji haramu.
Je Wana haki ya kuuwawa?

Hofu ilitanda kila sehemu, sio mitaani Wala kwenye miji.
Watu wachache wakajitwalia ukwasi wa kutisha na wengi wakafuata mkumbo.

Miradi haikufuata sheria ya fedha ya mwaka husika yaani appropriation act ila ikawa one man's show.

Ajira hazikutolewa kiasi Cha kupoteza na kutweza Vijana wa nchi hii.
Mfumo wa Biashara uliyumba maana waliokuwa na fedha basi waliwajua Financial Intelligence Unit

Mfumo wa uchumi ulianguka mpaka mabenki kufilisika.
Purchasing power kwa Mtanzania mmoja mmoja ilianguka kiasi Cha kushindwa wabongo kumudu Milo mitatu.

Kutumika nguvu kubwa kwenye ukusanyaji wa mapato na kubambikiwa watu Kodi kubwa kubwa zisizo na uhalisia.

Kudhalilisha kundi la wasomi na taaluma mbalimbali kwa wanasiasa wanaojifanya kujua kila kitu.

Kuminywa na kutozingatiwa kwa stahiki na maslahi ya Wafanyakazi wa nchi hii ikiwemo kutopandishwa kwa mishahara kwa miaka yote alipoongoza.

Kuharibiwa kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kiasi Cha watoto wengi wa familia fukara kushindwa kuendelea na masomo.

Biashara za mazao kufa kipindi chake, chukua tukio la Korosho za Mtwara na Lindi.
Zao la Ufuta
Kilimo Cha mahindi kule Sumbawanga, Nyanya pale Iringa

Kifupi hakuwa na jema ila jiulize kwa nini waliipenda force account itumike kwenye miradi ambayo haikuidhinishwa na Bunge?

Kwa nini walimdisicredit report ya CAG na kazi yake?

Kwa nini hawakutumia Competitive tendering kwenye kupata mzabuni wa Ile miradi?

Kwa nini waliotumika chini yake Vijana wakawa matajiri ghafra?

Kwa nini alidharau Wazee kama mzee Warioba na Wastahafu wengine?
Utumbo mtupu, hao waliokuwepo kabla yake waliwaheshimu hao wazee? Waliifikisha nchi hii wapi?

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
1650378620964.jpg
1664915659087.jpg
1651065655734.jpg
1642307456516.jpg
1649495794948.jpg
JamiiForums1655508168.jpg
Screenshot_20210729-122400_Instagram.jpg
20220528_225720.jpg
20220405_125947.jpg
1362054776.jpg
 
Attachments

  • 5625ad4da35aa34e52ebd33c9eb09fc1.jpg
    5625ad4da35aa34e52ebd33c9eb09fc1.jpg
    31.2 KB · Views: 7
Hakika SUKUMA GANG kubalini matokeo tu
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magu amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebei kumtukana na kumsema vibaya

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wako waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lkn hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magu hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magu huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahari zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uwongo una mwisho wake uwongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magu bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango was kutokea.
 
Ni humu JF tuu labda na twitter ila huko duniani kwingine wanamuelewa sana JPM.
 
Sasa mtu alivetangulia mbele ya haki unamtetea kwa maslahi ya nani mkuu ,
Sasa hivi anajitetea mwenyewe huko aliko, Chamasingi marehemu hua hasemwi vibaya , hata Kama kuna mabaya alifanya cha msingi ni kuendelea kumuombea , ili muumba ampunguzie adhabu tu kwa mabaya aliyofanya .
😅😅
 
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magu amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebei kumtukana na kumsema vibaya

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wako waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lkn hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magu hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magu huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahari zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uwongo una mwisho wake uwongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magu bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango was kutokea.
Watetezi mbona wapo wengi. Hujamsikia Kabudi anavyomtetea kwa kueleza walivyokuwa wakiwadanganya Watanzania kuhusiana na trilioni 360?

Hukumsikia wengi wakimtetea kwenye sifa yake ya kudanganya kuwa alikuwa bingwa kwelikweli wa kudanganya kuwa miradi yetu yote tunaijennga kwa pesa yetu kumbe tunakopa?

Hukumsikia CAG alivyomtetea marehemu jinsi marehemu alivyowaaminisha Watanzania kuwa yeye ni mzalendo kumbe alikuwa mwizi, pesa yote ya aliokuwa amebambikizia kesi za uhujumu uchumi, alizitia mfukoni mwake?

Hujo vijijini hukuwasikia watu wakimtetea marehemu kwa kipaji cha uwongo hadi kuwaaminisha wajinga wote kuwa kuna deni la kodi la kampuni moja la kutosheleza kumnunulia kila rai Noah moja wakati kampuni hiyo ilikuwa haina deni hata la shilingi moja?

Watetezi wapo wengi, wengi wanajua kipaji cha marehemu katika uwongo na hadaa, na hakika sijui kama kuna mtu atamfikia hata kwa karne nyingi zijazo. Kudanganya mamilioni ya watu,na watu wakakuamini na kukupigia makofi na kukusifia kwasababu unawadanganya, siyo jambo rahisi. Ni legacy hiyo ya marehemu lazima itetewe kwa nguvu zote ili kumkumbuka marehemu kwa uhalisia wake.

Pia ile sifa yake nyingine kubwa ya ujasiri wa kutenda uovu dhidi ya raia, tena bila woga: kuua, kushambulia, kuteka, kutesa na kuwabambikia watu kesi kisha kuwanyang'anya pesa, na pesa alizowanyanga kuzitia mfukoni mwake bila ya hofu ya kuhojiwa chochote na yeyote. Ule ni ujasiri wa pekee ambao lazima utetewe.
 
Leo kaamua kuweka wazi nae kuna siku atalala mavumbini.

Rip jpm
 
Back
Top Bottom