Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Tutajie mtawala aliyefikia hadi hatua ya kujifananisha na Malaika.

Akifika huko ataongoza Malaika.
Hakukuwa na utawala wa sheria Wala kanuni achilia mbali misingi ya haki.

Watu walitekwa na kuuwawa si kwa kificho
Vikundi vya watu wasiojulikana walitamalaki.
Maiti ziliokotwa kwenye viroba na watu walipo hoji wakaambiwa ni wahamiaji haramu.
Je Wana haki ya kuuwawa?

Hofu ilitanda kila sehemu, sio mitaani Wala kwenye miji.
Watu wachache wakajitwalia ukwasi wa kutisha na wengi wakafuata mkumbo.

Miradi haikufuata sheria ya fedha ya mwaka husika yaani appropriation act ila ikawa one man's show.

Ajira hazikutolewa kiasi Cha kupoteza na kutweza Vijana wa nchi hii.
Mfumo wa Biashara uliyumba maana waliokuwa na fedha basi waliwajua Financial Intelligence Unit

Mfumo wa uchumi ulianguka mpaka mabenki kufilisika.
Purchasing power kwa Mtanzania mmoja mmoja ilianguka kiasi Cha kushindwa wabongo kumudu Milo mitatu.

Kutumika nguvu kubwa kwenye ukusanyaji wa mapato na kubambikiwa watu Kodi kubwa kubwa zisizo na uhalisia.

Kudhalilisha kundi la wasomi na taaluma mbalimbali kwa wanasiasa wanaojifanya kujua kila kitu.

Kuminywa na kutozingatiwa kwa stahiki na maslahi ya Wafanyakazi wa nchi hii ikiwemo kutopandishwa kwa mishahara kwa miaka yote alipoongoza.

Kuharibiwa kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kiasi Cha watoto wengi wa familia fukara kushindwa kuendelea na masomo.

Biashara za mazao kufa kipindi chake, chukua tukio la Korosho za Mtwara na Lindi.
Zao la Ufuta
Kilimo Cha mahindi kule Sumbawanga, Nyanya pale Iringa

Kifupi hakuwa na jema ila jiulize kwa nini waliipenda force account itumike kwenye miradi ambayo haikuidhinishwa na Bunge?

Kwa nini walimdisicredit report ya CAG na kazi yake?

Kwa nini hawakutumia Competitive tendering kwenye kupata mzabuni wa Ile miradi?

Kwa nini waliotumika chini yake Vijana wakawa matajiri ghafra?

Kwa nini alidharau Wazee kama mzee Warioba na Wastahafu wengine?
Unayo yasema kwa mtu wa kawaida anayevuka mfugale hawezi kukhelewa. ILA NAKUHAKIKISHIA ULICHO ANDIKA NI UKWELI MTUPU USIO NA PUNJE YA UONGO NDANI YAKE.
 
Watetezi mbona wapo wengi. Hujamsikia Kabudi anavyomtetea kwa kueleza walivyokuwa wakiwadanganya Watanzania kuhusiana na trilioni 360?

Hukumsikia wengi wakimtetea kwenye sifa yake ya kudanganya kuwa alikuwa bingwa kwelikweli wa kudanganya kuwa miradi yetu yote tunaijennga kwa pesa yetu kumbe tunakopa?

Hukumsikia CAG alivyomtetea marehemu jinsi marehemu alivyowaaminisha Watanzania kuwa yeye ni mzalendo kumbe alikuwa mwizi, pesa yote ya aliokuwa amebambikizia kesi za uhujumu uchumi, alizitia mfukoni mwake?

Hujo vijijini hukuwasikia watu wakimtetea marehemu kwa kipaji cha uwongo hadi kuwaaminisha wajinga wote kuwa kuna deni la kodi la kampuni moja la kutosheleza kumnunulia kila rai Noah moja wakati kampuni hiyo ilikuwa haina deni hata la shilingi moja?

Watetezi wapo wengi, wengi wanajua kipaji cha marehemu katika uwongo na hadaa, na hakika sijui kama kuna mtu atamfikia hata kwa karne nyingi zijazo. Kudanganya mamilioni ya watu,na watu wakakuamini na kukupigia makofi na kukusifia kwasababu unawadanganya, siyo jambo rahisi. Ni legacy hiyo ya marehemu lazima itetewe kwa nguvu zote ili kumkumbuka marehemu kwa uhalisia wake.

Pia ile sifa yake nyingine kubwa ya ujasiri wa kutenda uovu dhidi ya raia, tena bila woga: kuua, kushambulia, kuteka, kutesa na kuwabambikia watu kesi kisha kuwanyang'anya pesa, na pesa alizowanyanga kuzitia mfukoni mwake bila ya hofu ya kuhojiwa chochote na yeyote. Ule ni ujasiri wa pekee ambao lazima utetewe.
Kuanzisha uzi juu ya mtu huyu ni kama kuchokoza watu na kutaka waendelee kuzungumzia juu ya madendo ya ubaya na uovu wakati wa utawala wake.

Kuhusu utawala wake;
1. Utawaambia nini wafanyakazi kuhusu nyongeza zao za mishahara na kupandishwa madaraja?
2. Utawaambia nini wanasiasa wa vyama vya siasa katika undeshaji wao wa shughuli zao halali za kisiasa.
3. Utawaambia nini wafanyabiashara kuhusu 'task force" yake.
4. Je! Vipi kundi lile la wasiojulikana?
5. Vipi manunuzi ya kile kivuko cha MV. Bagamoyo kugeuzwa kuwa zana ya kijeshi isiyoweza kuhojiwa?
6. Vipi matumizi ya jeshi katika mgogoro juu ya bei ya korosho na kangomba?
7. Vipi kuhusu kuongezeka kwa zigo la deni la taifa huku tukiaminishwa kuwa sisi "dona kantri"
8. Je makinikia na ripoti za Prof. Mruma & Ossoro huku zipigiwa promo na Prof. Kabudi ili kuhalalisha madai ya TZS 360Tn
9. Vipi kuhusu uzalishaji wa wakimbizi na kesi za uchochezi wa kisiasa kutokana na chuki dhidi ya kutopenda kukosolewa?
10. Sakata la MKIRU na vifo vya mamia ya raia na wengine kukutwa katika viroba vikielea baharini.
11. Vipi kuhusu mhimili mmoja kujichimbia chini na athiri hasi za kiutendaji wa mihimili mingine?
12. Yure mupe, yule muruke kwa wakazi wa Kimara na wale waliompigia kura kule Mwanza.
13. Vipi kuhusu mbuga ya Burigi na uhamisho wa hayawani wa mwituni
14. Vipi kuhusu mradi wa ustawishaji wa maendeleo ya Chato!?
15. Vipi kuhusu chafuzi za 2019 na 2020 na ushindi wa kishindo wa chama chake.

Dug! Orodha ni ndefu sana, pengine mengi bado hayafahamiki na wala hajaweza kuwekwa hadharani kutokana na tabia zake za kuminya uhuru wa vyombo vya habari.
 
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magufuli amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebehi kumtukana na kumsema vibaya.

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wake waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lakini hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magufuli hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magufuli huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahiyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahali zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uongo una mwisho wake uongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magufuli bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango wa kutokea.
Ukiona hakuna anayemtetea ujue haya hao unaosema walikuwa wanamkubali ila wameshagawanyika nao pia walikuwa hawamuelewi ila Iliwalazimu wakubaliane na mazingira yaliyopo. Kwa Sasa hata ukimtetea Haina faida yoyote, hata ukihuzunika haina faida yoyote cha msingi MAISHA yaendelee
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hata wanaotumika chini ya Samia watakuwa matajiri wa kufuru, NB Marope, Lameki na Bao la Mkono
Tutajie mtawala aliyefikia hadi hatua ya kujifananisha na Malaika.

Akifika huko ataongoza Malaika.
Hakukuwa na utawala wa sheria Wala kanuni achilia mbali misingi ya haki.

Watu walitekwa na kuuwawa si kwa kificho
Vikundi vya watu wasiojulikana walitamalaki.
Maiti ziliokotwa kwenye viroba na watu walipo hoji wakaambiwa ni wahamiaji haramu.
Je Wana haki ya kuuwawa?

Hofu ilitanda kila sehemu, sio mitaani Wala kwenye miji.
Watu wachache wakajitwalia ukwasi wa kutisha na wengi wakafuata mkumbo.

Miradi haikufuata sheria ya fedha ya mwaka husika yaani appropriation act ila ikawa one man's show.

Ajira hazikutolewa kiasi Cha kupoteza na kutweza Vijana wa nchi hii.
Mfumo wa Biashara uliyumba maana waliokuwa na fedha basi waliwajua Financial Intelligence Unit

Mfumo wa uchumi ulianguka mpaka mabenki kufilisika.
Purchasing power kwa Mtanzania mmoja mmoja ilianguka kiasi Cha kushindwa wabongo kumudu Milo mitatu.

Kutumika nguvu kubwa kwenye ukusanyaji wa mapato na kubambikiwa watu Kodi kubwa kubwa zisizo na uhalisia.

Kudhalilisha kundi la wasomi na taaluma mbalimbali kwa wanasiasa wanaojifanya kujua kila kitu.

Kuminywa na kutozingatiwa kwa stahiki na maslahi ya Wafanyakazi wa nchi hii ikiwemo kutopandishwa kwa mishahara kwa miaka yote alipoongoza.

Kuharibiwa kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kiasi Cha watoto wengi wa familia fukara kushindwa kuendelea na masomo.

Biashara za mazao kufa kipindi chake, chukua tukio la Korosho za Mtwara na Lindi.
Zao la Ufuta
Kilimo Cha mahindi kule Sumbawanga, Nyanya pale Iringa

Kifupi hakuwa na jema ila jiulize kwa nini waliipenda force account itumike kwenye miradi ambayo haikuidhinishwa na Bunge?

Kwa nini walimdisicredit report ya CAG na kazi yake?

Kwa nini hawakutumia Competitive tendering kwenye kupata mzabuni wa Ile miradi?

Kwa nini waliotumika chini yake Vijana wakawa matajiri ghafra?

Kwa nini alidharau Wazee kama mzee Warioba na Wastahafu wengine?
Wan
 
Ukiona hakuna anayemtetea ujue haya hao unaosema walikuwa wanamkubali ila wameshagawanyika nao pia walikuwa hawamuelewi ila Iliwalazimu wakubaliane na mazingira yaliyopo. Kwa Sasa hata ukimtetea Haina faida yoyote, hata ukihuzunika haina faida yoyote cha msingi MAISHA yaendelee
Kauli ya kukata tamaa...Hakuna binadamu anayemzidi Mungu, weka alama kwenye haya maneno....Mungu hajawahi dhihakiwa akabaki kimya!
 
Kauli ya kukata tamaa...Hakuna binadamu anayemzidi Mungu, weka alama kwenye haya maneno....Mungu hajawahi dhihakiwa akabaki kimya!
Mtu anayejiona hana hadhi ya kuongoza binadamu wenzake anataka akaongoze Malaika, Mungu kamchukua Ili akaongoze hao Malaika huko, sisi tubaki tunamtetea nini sasa, muache aongoze hao Malaika huko
 
Wauza madawa ya kulevya
Wanaomchukia Magufuli👇
-Waliotumbuliwa vyeti fake
-Wafanyakazi hewa
-Wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-Viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-Wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-Mabeberu wapenda dezo za taifa
-Wezi waliotaka JPM nae aungane nao ili waibe wote
 
Kuna wajinga wajinga wengi huko mtaani ambao aliwahadaa na yale mauongo yake ndio watetezi wake.

Hapa JF kwa Great Thinkers hana watetezi wengi sana sababu wengi wanajua kuchambua pumba na mchele

hapa jf kuna watu chini ya laki 6.member walio active hawazidi 150k,wanaomchukia ukiwamo wewe hamzidi 50 .
tukiongezea na mbuzi wengine kutoka twitter wote kwa ujumla hamtoboi watu 150 msiompenda jpm.

kama huamini simamisha kalio unakoishi anza kumponda,mpaka mkeo atakuingizia kidole.
 
Nani amtetee muuaji?.
snoop-dogg-crip-walk.gif

Ubarikiwe Mkuu.
 
kwahiyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahali zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uongo una mwisho wake uongo una ukomo wake.
Mkwara mbuzi huu na dua hili la kuku ni sawa na panya kumtishia nyau
 
Back
Top Bottom