Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Pasco,unauandishi mzuri ila UNAPENDA KUJISIFIA SANA ndugu.
Kila bandiko lazima ujisifie aka kujiona bora.
The Greatest Love of All, is learning to love yourself, and kujiappreciate mwenyewe, kuwa satisfied na jinsi ulivyo au chochote ulichonacho, regardless wengine wanakuonaje!. Ulifanikiwa katika hili, utakuwa bold, you can speak out your mind bila kujikomba komba kwa mtu, bila kumuogopa mtu, bila kumuofend mtu bali nguzo yako kuu ni "to speak the truth no matter what". Hiki ndicho ninachokifanya humu jf wakati wote!.

Pasco
 
Do I lack those things you said?

By the way thank you.
 
Ikitokea majeshi yakaua mtu ,mtu atakua ameleta fyokofyoko ?? Yaani majeshi ya wananchi wa Tanzania yakatumike kuua watu wake ambao sio wanajeshi halafu hapa unatetea u dikteta fyongo kwamba Magufuli sio dikteta ,nini maana ya utawala wa sheria ?? Kuna tofauti ya kuwa Mkali na kuwa dikteta tofautisha hilo na kwa hali nchi ilipofikia hakika inahitaji kiongozi mkali ila pia anayefuata sheria au la afute utawala wa sheria aongoze nchi kidikteta
Suala la Zanzibar ninkuwa Tanganyika na ccm wanajua kile kinachoendelea na CUF hawatapewa hii nchi, wapende wasipende... Zanzibar ipo mikononi mwa Tanganyika
 
Nimecheka sana, Magufuli msukuma wa watu kajisemea mwenyewe yeye siasa hajui lakini inatakiwa apigwe msasa lugha yake iwe ya kidiplomasia kidogo Haifai kuzungumza kama katibu kata kuna msemo wa Rais na misemo ya kina DC Makonda.
Sio fyoko fyoko
Magufuli sidhani kama anasoma zile hotuba anazoandikiwa.. Keshasema akisoma atakuwa anawasilisha mawazo ya mwandishi na wala sio mawazo yake... Ndio maana maneno kama hayo plus gongo, majipu, yapo kwenye hotuba yake
 
Suala la Zanzibar ninkuwa Tanganyika na ccm wanajua kile kinachoendelea na CUF hawatapewa hii nchi, wapende wasipende... Zanzibar ipo mikononi mwa Tanganyika
Kama walijua hivyo kulikua na sababu gani ya Zanzibar kupeperusha bendera yake ?? Kulikua na sababu gani ya kukubali serikali ya mseto ??? Kulikua na sababu gani Zanzibar kupitisha katiba yake ??
Kwa hiyo kwa sababu CCM na Tanganyika wanajua kinachoendelea na nchi hawata wapa cuf ,ndio ina justify kauli ya Pasco ya wanajeshi kuua raia wake ??
 
Angalizo. Neno Dikiteta sio neno baya kama lengo la matumizi yake ni lengo jema. Tikisema Magufuli ni Dikiteta, hatumaanishi ni Dikiteta Mbaya kama Hitler!, no way, Magufuli ni Dikiteta mwema anayeitwa Benovelent Dictator!. Tanzania hapa tulipofika, tunamuhitaji mtu kama huyu ili mambo yaende!.
Jumapili Njema.

Pasco
Nakubaliana na wewe, nami nilitambua hilo tangu mwaka 2006, na ndiyo maana Signature yangu inabeba ujumbe huo!
 
Aliwapora Wabunge hela na kuzielekeza Dar.

Amewapora hela Mawaziri amezielekeza Dar.

Aliwapora Dodoma Mashine ya CT Scan ikapelekwa Dar

Hela ya Uhuru Day ilipelekwa Dar

Huyu atakuwa raisi wa Dar
 
TATIZO LAO PASCO HUWA SIKUELEWI KWANI MARA UEGEMEE KWA LOWASA MARA USEME HIVI SASA SIJUI MISIMAMO YAKO NI IPI?
Usisahau, mbowe alisema kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu, only permanent interests. Pasco anaangalia wapi penye maslahi kwa wakati uliopo.
 
Suala la Zanzibar ninkuwa Tanganyika na ccm wanajua kile kinachoendelea na CUF hawatapewa hii nchi, wapende wasipende... Zanzibar ipo mikononi mwa Tanganyika

CCM hawana uwezo wa kupambana na nguvu ya umma.

Wanaamini kuwa wana wana Silaha za kutosha, Wana magari ya Upupu, Wana polisi na wanaJeshi wengi...

Wanapaswa kutambua kuwa hawataweza kuzuia nguvu ya umma...
 
Aliwapora Wabunge hela na kuzielekeza Dar.

Amewapora hela Mawaziri amezielekeza Dar.

Aliwapora Dodoma Mashine ya CT Scan ikapelekwa Dar

Hela ya Uhuru Day ilipelekwa Dar

Huyu atakuwa raisi wa Dar
Kwa kauli yake Mwenyewe amesema Dar ndio Tanzania ,ukifikiria kwa undani kauli hiyo acha dodoma wale viwavi tu
 
Magufuli sidhani kama anasoma zile hotuba anazoandikiwa.. Keshasema akisoma atakuwa anawasilisha mawazo ya mwandishi na wala sio mawazo yake... Ndio maana maneno kama hayo plus gongo, majipu, yapo kwenye hotuba yake
Ukimtazama huyu jamaa unamuona Kama alikua na mengi sana kichwani siku nyingi juu ya nchi hii na utaona kama alijiapiza kupambana na kilichoko mbele yake, hii ni nzuri lakini kuna jinsi ya kushughulikia mambo na jinsi ya kuyahandle lazima afundishwe tatizo msukuma ni mbishi ila naamini ataelewa.

Hata kwenye kikao cha wabunge wa CCM walizungumzia hii, pamoja na uteuzi wa mawaziri kwamba wasomi wengi walimuunga mkono Lowasa, kuna mengi ya kusema.....
 
CCM hawana uwezo wa kupambana na nguvu ya umma.

Wanaamini kuwa wana wana Silaha za kutosha, Wana magari ya Upupu, Wana polisi na wanaJeshi wengi...

Wanapaswa kutambua kuwa hawataweza kuzuia nguvu ya umma...
Kaka ingekuwa nchi za uarabuni sawa ila sio kwa waafrika.. Watakinukisha watapigwa mabomu siku moja mbili watatulia.. Watakimbilia kenya mombasa ... Ndaninha mwaka mambo yanatulia watu wanaendelea na maisha.. Cha kufanya wakubali tu kuwa ccm ni kama malkia elizabeth wao..
 
Hapa ndio naposhindwa kuelewa na niseme wazi labda itanichukua miaka mia kuelewa ZANZIBAR SIO NCHI NI SEHEMU YA JAMUHURI PASCO ,naomba unijibu swali langu
1. katiba tuliyo nayo imeweka hayo maswala ya usalama kwenye Muungano ,ila mambo mengine kama ya ZEC hayapo kwenye Muungano ,kulikua na tatizo gani wa Zanzibar kudai haki yao kama nchi kamili ??
2. Ikiwa wanaona haki yao ya kufanya maamuzi imechukuliwa na bara ? Kwanini Warioba na Wananchi wengi waliona serikali tatu ni suluhisho la matatizo ya Muungano ??
3.Na kwa kauli hiyo Wanzanzibar si watanendelea kuona Tanganyika imewakalia kimabavu ,kwamba baba kama mzazi kwa mtoto wa kambo jukumu lake ni kumridhisha mama wa mtoto kimapenzi ila sio kumsomesha huyo mtoto ,huoni hilo ni tatizo ??
4.Kilicho kufanya uandike tunachotaka sisi ni adabu ,heshima ,amani na utulivu ,sisi ni kina nani ???
5. Kudai haki kama unaona umedhulumiwa ni kukosa adabu na heshima ???
6. Au kauli hiyo umetoa baada ya kuskia Manyerere Jacton kasifiwa unataka usafirie nyota yake ???.
7.NB Nyerere alishaona hili na akasema kwa katiba tuliyo inaweza kumfanya mtu kuwa dikteta wa ajabu ,
Kwanini tuendelee kuing'ania katiba hii ambayo hata walio itengeneza wametoa angalizo zao ??
1. Hakuna tatizo kwa Zanzibar kudai haki yao kama nchi kamili, ila ili liwezekane hatua ya kwanza ni kwa Zanzibar kudai kuwa nchi, ndipo ije idai hizo haki zake!, kwa sasa Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT yenye mamlaka yake ya ndani ikiwemo ZEC!, hivyo Zanzibar as it is and as of now ni subject wa JMT until otherwise!.
2. Haki yao ya kufanya uamuzi haijachukuliwa na bara, imechuliwa na ZEC, hiyo ZEC ni yao, ilichokifanya ZEC wamekikubali ndio maana wametulia, wasingekubali wangechukua hatua!. Hili la Warioba hapa sipo pake!.
3. Tanzania haikalii Zanzibar kimabavu, bali ukiishakubali kuingia kwenye mahusiano ya kindoa, unapaswa kuheshimu mapatano ya ndoa na kuiheshimu ndoa. Wako wanandoa wengi wanawatamani watu baki, ukiishajicomit kwenye ndoa, yuo in for it. Muungano wetu ni kama ndoa ya Katoliki, once in, you in for good till death do you apart!. Hati za muungano ziliweka namna tuu ya kuingia kwenye muungano hakuna namna ya kutoka!, huu muungano wetu ni wa milele, hakuna wa kuuvunja wala jinsi ya kuuvunja!.
4. Sisi Watanzania, wakiwemo Wazanzibari ambao ni sehemu ya JMT!. HESHIMA, ADABU, AMANI NA UTULIVU!, atakayeleta fyoko fyoko cha moto atakiona!, au atakipata!, ikibidi hata zile 'za moto' zitafyatuliwa na kupenyeza miili ya waleta fyoko kuwashikisha adabu!.
5. Kudai haki sio kukosa adabu au heshima, tena haki inapaswa kudaiwa, kwa sababu hailetwi kwenye kikombe cha chai, ila hiyo haki inatakiwa kudaiwa kwenye heshima, adabu, amani na utulivu, kudai huko haki kusitishie amani na utulivu uliopo kutahesabiwa ni fyoko fyoko na kutushughulikiwa kikamilifu!. Haki ya kweli inadaiwa kupitia vyoto vya utoaji haki!.
6. Manyerere ni mwandishi nguli, na mimi namkubali sana, ila mapito yake ni tofauti kabisa na mapito yangu, hivyo kamwe siwezi kutaka kusafiia nyota yake au nyota ya mtu mwingine yeyote!, hapa nilipo tuu nyota yangu imenielemea, hivyo hiyo ya mwingine nitaiwekea wapi ili nisafiie?!.
7. Kama umelitambua hili la katiba inaweza kumfanya ais wetu kuwa dikteta wa ajabu, na Magufuli ni dikteta by nature, kama nayo inamuongezea huo udikiteta, tuungane kuwasihi wenzetu Wanzanzibari wasilete fyoko fyoko, chamoto watakipata!.

Pasco
 
sasa wewe ulitaka Amiri jeshi mkuu aseme urojo pale?hivi kama hamna cha kupost si bora mtulie tu. Watu wengine mnajitafutia matatizo kiaina. kabla haujapost kitu,soma kwanza siasa na ngazi za uongozi. Ukiambiwa udhibitishe kama ni dictator utatoa ushahidi gani?Tulia na tafakari kwanza kabla ya kupotosha umma.
 
1. Hakuna tatizo kwa Zanzibar kudai haki yao kama nchi kamili, ila ili liwezekane hatua ya kwanza ni kwa Zanzibar kudai kuwa nchi, ndipo ije idai hizo haki zake!, kwa sasa Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT yenye mamlaka yake ya ndani ikiwemo ZEC!, hivyo Zanzibar as it is and as of now ni subject wa JMT until otherwise!.
2. Haki yao ya kufanya uamuzi haijachukuliwa na bara, imechuliwa na ZEC, hiyo ZEC ni yao, ilichokifanya ZEC wamekikubali ndio maana wametulia, wasingekubali wangechukua hatua!. Hili la Warioba hapa sipo pake!.
3. Tanzania haikalii Zanzibar kimabavu, bali ukiishakubali kuingia kwenye mahusiano ya kindoa, unapaswa kuheshimu mapatano ya ndoa na kuiheshimu ndoa. Wako wanandoa wengi wanawatamani watu baki, ukiishajicomit kwenye ndoa, yuo in for it. Muungano wetu ni kama ndoa ya Katoliki, once in, you in for good till death do you apart!. Hati za muungano ziliweka namna tuu ya kuingia kwenye muungano hakuna namna ya kutoka!, huu muungano wetu ni wa milele, hakuna wa kuuvunja wala jinsi ya kuuvunja!.
4. Sisi Watanzania, wakiwemo Wazanzibari ambao ni sehemu ya JMT!. HESHIMA, ADABU, AMANI NA UTULIVU!, atakayeleta fyoko fyoko cha moto atakiona!, au atakipata!, ikibidi hata zile 'za moto' zitafyatuliwa na kupenyeza miili ya waleta fyoko kuwashikisha adabu!.
5. Kudai haki sio kukosa adabu au heshima, tena haki inapaswa kudaiwa, kwa sababu hailetwi kwenye kikombe cha chai, ila hiyo haki inatakiwa kudaiwa kwenye heshima, adabu, amani na utulivu, kudai huko haki kusitishie amani na utulivu uliopo kutahesabiwa ni fyoko fyoko na kutushughulikiwa kikamilifu!. Haki ya kweli inadaiwa kupitia vyoto vya utoaji haki!.
6. Manyerere ni mwandishi nguli, na mimi namkubali sana, ila mapito yake ni tofauti kabisa na mapito yangu, hivyo kamwe siwezi kutaka kusafiia nyota yake au nyota ya mtu mwingine yeyote!, hapa nilipo tuu nyota yangu imenielemea, hivyo hiyo ya mwingine nitaiwekea wapi ili nisafiie?!.
7. Kama umelitambua hili la katiba inaweza kumfanya ais wetu kuwa dikteta wa ajabu, na Magufuli ni dikteta by nature, kama nayo inamuongezea huo udikiteta, tuungane kuwasihi wenzetu Wanzanzibari wasilete fyoko fyoko, chamoto watakipata!.

Pasco
Tufanye hivi kwenye hii risala yako sijaiona ni wapi umejibu maswali yangu zaidi ya kuendeshwa na mihemko

Eti Muungano ni kama ndoa hivyo unapaswa kuheshimu mapatano ya ndoa ,kwa hiyo kama baba ni mfiraji mama aendelee kuvumilia kuoza sehemu zake za nyuma ??kwa sababu wapo kwenye ndoa ?? Anyway uwe na siku njema
 
Ebu tafuta neno zuri Pasco, Rais Magufuli kanikosha mie!
Ni Rais tuliyemngoja kwa miaka, na ametokea!
Sasa ni kazi tu kuijenga Tanzania.
Naamini, through Magufuli Tanzania yenye maziwa na asali imepatikana!
Mungu ambariki sana atufikishe tunapopataka!
 
Back
Top Bottom