Magufuli ndio anatoa 'Coup de grace' kwa CCM

unataka ushahidi? CCM imegaragzwa ZANZIBAR vibaya sana CCM Pemba haikupata hata kiti kimoja angalau cha diwani. Ngome ya CCM Unguja imesambaratishwa .CCM watia mpira kwapani. Wamesema wameibiwa. .Wameambiwa toeni ushahidi wameshindwa, wakaamua kufuta uchaguzi.
CCM ni KAPUT
Nakala kwa mnafiki Barbarosa .
 
Moja ya kanuni za msingi kabisa katika mijadala ni hii: "Jikite katika hoja ya mpinzani wako. Kuelewa vizuri hoja ya mpinzani wako ni muhimu katika kuinyoosha na kuirekebisha (refute)". Mtoa mada hapa ametoa hoja nzuri na nzito kuhusu Rais Magufuli na udhaifu wa chama chake CCM. Ametaja maeneo kadhaa yenye udhaifu kiutendaji kama bomoa bomoa, vita na mabenki ya kibiashara, mkwamo wa Zanzibar, uhusiano wa kimataifa na mambo ya ubaguzi. Hii ni mada nzito inayopaswa kujadiliwa kwa hoja za kiuchambuzi ambazo zitatoa mwanga wa ufahamu kuhusu haya masuala. Cha kushangaza na kusikitisha ni baadhi ya wanaJF (ambao kimsingi wanajinasibu kama "great thinkers") kuacha mada na kukimbilia kujadili mambo ya uchaguzi wa mwaka jana, Ukawa na kutaja majina ambayo hayana uhusiano wowote na hoja inayojadiliwa. Huu ni udhaifu mkubwa. Badala ya JF kuwa uwanja wa mapambano ya hoja zenye mantiki, inageuzwa kuwa kijiwe cha kejeli, matusi, vijembe na mipasho. This must stop!
Kiongozi kuna watu wameajiriwa kwa mkopo kulinda chama.
Yani lazima waongee tu hata kama hoja haipo.
 
Sawa basi tuweke pembeni Uraisi ambao mnasema mmeibiwa ingawaje mpaka leo hii haman ushsidi wowote ule mliotoa zaidi ya maneno tu!

Vipi kuhusu Ubunge? Kwa maana matokeo ya Ubunge mnayakubali sasa mbona tofauti ni kubwa sana? Ni zaidi ya mara mbili ukawa Wabunge 78 CCM zaidi ya 200!!!

Hapo vipi utamshawishi nani Duniani akuelewe kwamba Chama kilichoshinda viti zaidi ya 200 dhidi ya chini ya 80 eti kinakufa??
!!!

Ni mtu mwenye akili ndogo tu anayeishi kwenye Dunia yake mwenyewe ambayo kiuhalisia haipo ndiyo anaweza kufikiri hivi!
Mwanzo hicho chama Kulikua na viti vingapi? Je kimeongeza viti au kimepunguza? Na mwanafunzi yupi bora kwako kati ya analipata 30% kutoka 25% na yule aliyepata 70% kutoka 90%?
 
Mwanzo hicho chama Kulikua na viti vingapi? Je kimeongeza viti au kimepunguza? Na mwanafunzi yupi bora kwako kati ya analipata 30% kutoka 25% na yule aliyepata 70% kutoka 90%?

Mada Kuu haisemi hivyo, bali mada kuu inasema kwamba CCM imekufa, sasa Chama kilichokufa hakimshindi mpinzani wake wa tofauti ya asilimia 20 na mara mbili zaidi ya viti vya Ubunge!
 
Mada Kuu haisemi hivyo, bali mada kuu inasema kwamba CCM imekufa, sasa Chama kilichokufa hakimshindi mpinzani wake wa tofauti ya asilimia 20 na mara mbili zaidi ya viti vya Ubunge!
Ccm haiwezi kufa haraka hivyo kwani bado wanaliongoza taifa mbumbumbu ambalo 80% ya raia wake hawajasoma. Pili watakao iua ccm ni vijana walioanza kuzaliwa 1992 kuja huku juu. Ndio maana unaona sehemu zenye watu wenye elimu hakuna upumbavu wa ccm kwakua wanajielewa
 
Hawawezi kuiuwa CCM kama hajawapata mbadala wa CCM hilo ndiyo tatizo,mpaka sasa hivi pmj na mapungufu yake yote bado hakuna Chama chnenye kusthili kuitwa Chama kama CCM hilo halina ubishi kwani hata mgombea Uraisi wa ukawa alitoka CCM maana yake ni kwamba upinzani kama Upinzani hawana uwezo wa kuzalisha na kukuza viongozi wanasubiria wale waliotemwa na CCM sasa kwa staili hii hawawezi kuishinda CCM!
 
Ndio maana nimesema watoto waliozaliwa 1992 kuja huku juu ndo wapinzani wa kweli. Maana hakuna mwanasiasa wa upinzani ambaye hajatokea ccm. Hili halina ubishi
 
Ukisoma mawazo ya vijana wa ufipa yanashangaza kweli...kama misukule flan hivi...
 
Hawawezi kuiuwa CCM kama hajawapata mbadala wa CCM hilo ndiyo tatizo,mpaka sasa hivi pmj na mapungufu yake yote bado hakuna Chama chnenye kusthili kuitwa Chama kama CCM hilo halina ubishi kwani hata mgombea Uraisi wa ukawa alitoka CCM maana yake ni kwamba upinzani kama Upinzani hawana uwezo wa kuzalisha na kukuza viongozi wanasubiria wale waliotemwa na CCM sasa kwa staili hii hawawezi kuishinda CCM!
Barbarosa leo unapambana peke yako mno.
Wakwapi waajiriwa wenzako wa mkopo?
Kina Lizaboni, Mcubic, et.al
 
Ndio maana nimesema watoto waliozaliwa 1992 kuja huku juu ndo wapinzani wa kweli. Maana hakuna mwanasiasa wa upinzani ambaye hajatokea ccm. Hili halina ubishi

Kama wataibuka wapinzani wengine labda hapo unaweza kuwa sawa lkn siyo hawa wachumia tumboa akina Tundu Lisu na Mbowe!
 
Kama wataibuka wapinzani wengine labda hapo unaweza kuwa sawa lkn siyo hawa wachumia tumboa akina Tundu Lisu na Mbowe!
Lakini angalau wanatia jambajamba kwa uchumia tumbo wao serikali inakua inapata joto
 
Huko kubebwa na tume ndo unaiita ushindi hata hiyo link kama sio chaguzi hii ccm imeongoza kwa 20% ya kubebwa na time,kama chama che demokrasia waliogopa nini Matokeo ya uchaguzi zenji kutangzwa acha kujitia ukichaaa
Hakuna tume huru ya uchaguzi, na tunahisi yaliyotokea Zanzibar yalitokea Tanzania Bara ila Wa Bara ni wapole lakini wazenj bado wanadai haki as we very well know that sham democracy fuels terrorism!
 
...ccm ilikuwa inaondoka na JK for sure...na ndio maana JPM alihakikisha hata kwenye kampeni yake hamna chagua ccm bali chagua JPM ...hili aliliona mapema na hakika alitumia nguvu ya ziada kujinadi...kama anayotumia sasa kutawala..maana wanajua walivyoingia madarakani...
...ccm ilishakufa...na ccm haikumwingiza JPM madarakani...kilichomuingiza JPM
madarakani ni vyombo vya dola na tume ya lubuva....na ndivyo wanavyotaka kufanya kule zenj...so sad indeed..
 
'Coup de grace' ni kitendo au tukio la kumalizia au kuharibu moja kwa moja kitu kilichokuwa kinaendelea kuwa dhaifu kila uchao.

Ni kama kumuua kwa kumpiga risasi askari mwenzako aliyeumia sana katika mapambano ili kumpunguzia maumivi na mateso.

CCM ilikuwa inaumia, ilikuwa inateseka vibaya,ilishachoka kabisa kabla ya Serikali ya Magufuli.

CCM ilikuwa kakikundi fulani hivi ka vibaka, majangili, mafisadi na watu wasiojua utendaji wala ufanisi.

Ila hao ndio waliokuwa wana CCM na ndio iliyokuwa CCM yenyewe na ndivyo ilivyo hata leo hii.

Ni chama chenye saratani ambayo kwakweli hakuna namna ya kuiponyesha na ndio maana Magufuli ameamua kuwa heri tu huyu mgonjwa afe kuliko azidi kuweweseka.

Wana CCM wenyewe wamebaki mabubu wakipambana nyuma ya pazia.
Wamebaki wasiojiamini kwa hoja kiasi kwamba pamoja na wingi wao bungeni hawawezi kujenga wala kujibu hoja na hawataki kabisa watanzania wauone huu upungufu. Hawataki TBC irushe bunge.

Ni wapiganaji waoga, aina ya wale wanaovizia mtu usiku wampige rungu la kisogo.
Wanafanya mikutano ya kisiasa lakini hawataki wapinzani wafanye.

Huku kwenye mitandao ya jamii wameajiri kasuku wa kuwapigia debe japo kwa mkopo ili tu kujaribu kujisitiri.

Coup de grace ni wana CCM kuitana majipu.
~Ni bomoa bomoa ya nyumba za masikini.
~Ni vita na matajiri.
~Ni Magufuli kukwepa mkwamo wa kisiasa Zanzibar
~Ni kupambana na mabenki nchini.
~Ni kuwa na mahusiano mabovu na Mataifa makubwa, jumuiya za kimataifa.
~Ni kunyamazia ubaguzi wa watu weupe na weusi Zanzibar.

Kuna msemo unaosema 'nionyeshe marafiki zako na mimi ntakwambia wewe ni nani'.
Magufuli hana rafiki na hapendi watanzania tuwe na marafiki.

Ni hatari kuwa na rais ambaye hatabiriki na ndio maana naamini kuwa Magufuli anaisaidia CCM kupumzika mapema kwa kuiua.
Kuna baadhi ya mambo tuwe tunaweka akiba ya maneno la sivyo tutajichanganya soon, mwanzoni Mlisema raisi anatumia ilani ya Chadema, pili ifike hatua siasa za maji taka tuziweke pembeni bali tumulilie Tanzania aliyepotea, hivi unawatetea matajiri wakwepa kodi? unawatetea matajiri wanaoiba mali ya umma? hivi leo tungeshinda Ukawa na sera yetu ya elimu bure mpaka chuo kikuu hela tungezitoa wapi kama si kuwabana hawa matajiri, nawasihi tujifunze kuweka akiba ya maneno, tulimusema Lowasa miaka nenda rudi kuwa ni fisadi lakini tumemusafisha kwa vinywa vyetu.
 
Watuwengine akilizao zitakuwa zimekalia kwenye unyayo. Asa viongozi wa ukawa wajiuzuri kwa hoja ipi ya msingi? Ukiangalia trend ya kisiasa vyama vya upinzani vimepiga hatua tena kubwa sana. Maana tangu vyama vingi vianze ni mara ya kwanza msimuhuu kwa vyama vya upinzani kukamata halimashauri mojawapo ikiwa kinondoni. Mbona hatuwaambii hawa viongozi wetu wa ccm walio gawa halimashauri hizi kwa ukawa. Mm ni kada wa ccm ila nina mashaka juu uwezowako wa kufikiri unaposema viongozi ukawa wajiuzuri.
ni kweli kabisa upinzani umepiga hatua lakini tumekosa msimamo, binafsi mm ni mwana Ukawa kindaki ndaki lakini na laani ujio wa Lowasa tena ndo umetunyima ushindi
 
...ccm ilikuwa inaondoka na JK for sure...na ndio maana JPM alihakikisha hata kwenye kampeni yake hamna chagua ccm bali chagua JPM ...hili aliliona mapema na hakika alitumia nguvu ya ziada kujinadi...kama anayotumia sasa kutawala..maana wanajua walivyoingia madarakani...
...ccm ilishakufa...na ccm haikumwingiza JPM madarakani...kilichomuingiza JPM
madarakani ni vyombo vya dola na tume ya lubuva....na ndivyo wanavyotaka kufanya kule zenj...so sad indeed..
na majority zaidi 2/3 bungen yametoka wapi
 
Back
Top Bottom