Magufuli ndio anatoa 'Coup de grace' kwa CCM

na majority zaidi 2/3 bungen yametoka wapi
..yametokana na tume na vyombo vya dola...jibu unalo...alafu kumbuka hoja kuu hapa ni jinsi JPM alivyoingia madarakani...na utawala wake...naona unakiri figisu zilizomwingiza JPM madarakani kwa kuleta hoja ya 2/3 ya wa bunge....
 
Tafiti zako labda zitakubalika kwa Wanachadema wenzako tu lkn hakuna mtu mwenye akili Dunia hii anayeweza kukubalia kutokana na huu ukweli ufuatao; ukawa (Muungano wa vyama vyote) umepata Wabunge chini ya 80 wakati CCM imeshindwa Wabunge zaidi ya 200, Raisi wa JMTZ (CCM) amemshinda mpinzani wake wa ukawa kwa tofauti ya karibia asilimia 20 (20%) ya kura zote zilizopigwa hii ni tofauti kubwa sana kwa kiwango chochote kile kinachotumiwa na binadamu kwanza ingekuwa Vyama vya Kidemokrasia Viongozi wote wa ukawa walipaswa wajiuzulu kwani wameshindwa kabisa, chaguzi za Serikali za Mitaa ndiyo wala usiseme!

Kumbuka kwamba nimeongelea kuhusu ukawa na wala siyo chama kimoja kimoja, kama tukichukua kwa mfano chadema peke yake hali inakuwa mbaya zaidi!
yaelekea ni mmoja wa vijana ambao kikwete kawaombea kwa Magufuri awakumbuke lakini sidhani kama atawakumbuka
 
Kama unayofikiria ni ya ukweli.. Si mbaki nayo ufipa huko.. Ili myazungumze katika kampeni 2020..Ukiwa mtashika kila mti hamtabaki salama
 
MTANZANIA AMBAYE KUANZIA TAREHE 26/10/2015 BADO ANAONGELEA U-CCM NA U-CHADEMA NA UKAWA ANANIUDHIIIIIIIIIIII.


OOOH CCM HIVI CHADEMA VILE...ESPECIALLY WABUNGE! HAKUNA WAKATI NAKEREKA BUNGENI KAMA NINAPOWASIKIA WAKIJITAMBA NA KURUSHIANA VIJEMBE KISA VYAMA VYAO. (RESPECT TO ZITTO FOR BEING UNIQUE).

NI WAKATI WA KUIJENGA NCHI SASA!!!

TUJENGE NCHI...VYAMA TUSUBIRI TENA BAADA YA MIAKA MITANO TAFADHALI!
 
na majority zaidi 2/3 bungen yametoka wapi
Bro! Usiangalie wingi tu, pia angalia je! Wanastahili kuwa pale, je wanaweza kuunda hoja zenye tija! Ila chaajabu kati ya zaiid ya wabunge 200 wa ccm awafik atakumi wenyeuwezo wa kutengeneza hoja zenye mashiko na zenye tija kwa taifa "shame"

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
'Coup de grace' ni kitendo au tukio la kumalizia au kuharibu moja kwa moja kitu kilichokuwa kinaendelea kuwa dhaifu kila uchao.

Ni kama kumuua kwa kumpiga risasi askari mwenzako aliyeumia sana katika mapambano ili kumpunguzia maumivi na mateso.

CCM ilikuwa inaumia, ilikuwa inateseka vibaya,ilishachoka kabisa kabla ya Serikali ya Magufuli.

CCM ilikuwa kakikundi fulani hivi ka vibaka, majangili, mafisadi na watu wasiojua utendaji wala ufanisi.

Ila hao ndio waliokuwa wana CCM na ndio iliyokuwa CCM yenyewe na ndivyo ilivyo hata leo hii.

Ni chama chenye saratani ambayo kwakweli hakuna namna ya kuiponyesha na ndio maana Magufuli ameamua kuwa heri tu huyu mgonjwa afe kuliko azidi kuweweseka.

Wana CCM wenyewe wamebaki mabubu wakipambana nyuma ya pazia.
Wamebaki wasiojiamini kwa hoja kiasi kwamba pamoja na wingi wao bungeni hawawezi kujenga wala kujibu hoja na hawataki kabisa watanzania wauone huu upungufu. Hawataki TBC irushe bunge.

Ni wapiganaji waoga, aina ya wale wanaovizia mtu usiku wampige rungu la kisogo.
Wanafanya mikutano ya kisiasa lakini hawataki wapinzani wafanye.

Huku kwenye mitandao ya jamii wameajiri kasuku wa kuwapigia debe japo kwa mkopo ili tu kujaribu kujisitiri.

Coup de grace ni wana CCM kuitana majipu.
~Ni bomoa bomoa ya nyumba za masikini.
~Ni vita na matajiri.
~Ni Magufuli kukwepa mkwamo wa kisiasa Zanzibar
~Ni kupambana na mabenki nchini.
~Ni kuwa na mahusiano mabovu na Mataifa makubwa, jumuiya za kimataifa.
~Ni kunyamazia ubaguzi wa watu weupe na weusi Zanzibar.

Kuna msemo unaosema 'nionyeshe marafiki zako na mimi ntakwambia wewe ni nani'.
Magufuli hana rafiki na hapendi watanzania tuwe na marafiki.

Ni hatari kuwa na rais ambaye hatabiriki na ndio maana naamini kuwa Magufuli anaisaidia CCM kupumzika mapema kwa kuiua.
Lazima unatumia viroba. Umeandika kishabiki hadi unatia kinyaa.
 
MTANZANIA AMBAYE KUANZIA TAREHE 26/10/2015 BADO ANAONGELEA U-CCM NA U-CHADEMA NA UKAWA ANANIUDHIIIIIIIIIIII.


OOOH CCM HIVI CHADEMA VILE...ESPECIALLY WABUNGE! HAKUNA WAKATI NAKEREKA BUNGENI KAMA NINAPOWASIKIA WAKIJITAMBA NA KURUSHIANA VIJEMBE KISA VYAMA VYAO. (RESPECT TO ZITTO FOR BEING UNIQUE).

NI WAKATI WA KUIJENGA NCHI SASA!!!

TUJENGE NCHI...VYAMA TUSUBIRI TENA BAADA YA MIAKA MITANO TAFADHALI!
Utapata vingine vingi vya kukuudhi waza vinavyokufurahisha.
 
Tetemeko la Ardhi linaonyesha Mungu hajaukubali uongozi uliopo madarakani.
 
Chama ni watu. Kama bado watu wapo chama kitaishi. Keep on dreaming.
 
Back
Top Bottom