Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
'Coup de grace' ni kitendo au tukio la kumalizia au kuharibu moja kwa moja kitu kilichokuwa kinaendelea kuwa dhaifu kila uchao.
Ni kama kumuua kwa kumpiga risasi askari mwenzako aliyeumia sana katika mapambano ili kumpunguzia maumivi na mateso.
CCM ilikuwa inaumia, ilikuwa inateseka vibaya,ilishachoka kabisa kabla ya Serikali ya Magufuli.
CCM ilikuwa kakikundi fulani hivi ka vibaka, majangili, mafisadi na watu wasiojua utendaji wala ufanisi.
Ila hao ndio waliokuwa wana CCM na ndio iliyokuwa CCM yenyewe na ndivyo ilivyo hata leo hii.
Ni chama chenye saratani ambayo kwakweli hakuna namna ya kuiponyesha na ndio maana Magufuli ameamua kuwa heri tu huyu mgonjwa afe kuliko azidi kuweweseka.
Wana CCM wenyewe wamebaki mabubu wakipambana nyuma ya pazia.
Wamebaki wasiojiamini kwa hoja kiasi kwamba pamoja na wingi wao bungeni hawawezi kujenga wala kujibu hoja na hawataki kabisa watanzania wauone huu upungufu. Hawataki TBC irushe bunge.
Ni wapiganaji waoga, aina ya wale wanaovizia mtu usiku wampige rungu la kisogo.
Wanafanya mikutano ya kisiasa lakini hawataki wapinzani wafanye.
Huku kwenye mitandao ya jamii wameajiri kasuku wa kuwapigia debe japo kwa mkopo ili tu kujaribu kujisitiri.
Coup de grace ni wana CCM kuitana majipu.
~Ni bomoa bomoa ya nyumba za masikini.
~Ni vita na matajiri.
~Ni Magufuli kukwepa mkwamo wa kisiasa Zanzibar
~Ni kupambana na mabenki nchini.
~Ni kuwa na mahusiano mabovu na Mataifa makubwa, jumuiya za kimataifa.
~Ni kunyamazia ubaguzi wa watu weupe na weusi Zanzibar.
Kuna msemo unaosema 'nionyeshe marafiki zako na mimi ntakwambia wewe ni nani'.
Magufuli hana rafiki na hapendi watanzania tuwe na marafiki.
Ni hatari kuwa na rais ambaye hatabiriki na ndio maana naamini kuwa Magufuli anaisaidia CCM kupumzika mapema kwa kuiua.