Magufuli "Nchale!" - Usiteme, Usimeze wala Usimumunye!

Magufuli "Nchale!" - Usiteme, Usimeze wala Usimumunye!

Binafsi sidhani kuna yeyote anayeweza kusema kwa nia chanya kwamba katika hili la kontena 277 ‘tusifanye lolote'. Huku kufilisika kifikra kuliko kithiri.

Watanzania tunaweza kuwa na raisi mkurupukaji kweli kweli na kwa maoni yangu binafsi hivyo ndivyo alivyo; lakini wazungu wana nusemi unaosema " sometimes it has to get worse before it becomes better".

Kupitia kwa maamuzi haya ya kukurupuka kuna faida maana walipa kodi wataumia kwa kulipia gharama za kukurupuka lakini wawakilishi wao wakirudi bungeni hawatapitisha sheria kandamizi kwa hati ya dharura kama ilivyokuwa sheria ya madini ya 1998.

Kwa kifupi maumivu ambayo walipa kodi watayapata (kama matokeo ya kushindwa kesi) yatafanya kizazi kijacho kiwe makini zaidi na hawa majambazi.
 
Uko huko kwa trump ...unataka sisi tukubebee mzigo wewe ukiwa unakula ma baga huko USA
 
Kwanza akiri hadharani kuhusika na jambo hilo na aombe radhi hadharani ,halafu Avunje mikataba ya wawekezaji kwa kufuata utaratibu wa kisheria , ule utaratibu wa kimataifa ambao Tanzania imesaini kuufuata , then aanze kuchimba mwenyewe madini ya nchini na kuchakata kila kitu kama wafanyavyo wawekezaji
Aombe radhi kwa nani? ? Una uhakika alishiriki? ?
Ni sawa na kusema Mnyika alikubaliana na uwepo wa lowasa Chadema. Na vip Mbowe alipobadilisha gia angani kwa kukiuza chama aliwaomba radhi sirini au hadharani? Hamna sera mmekwisha tupa kule
 
Unaishi nchi gani vile?
Marekani eeh! shubaaamit.
Njoo hapa uone bei ya sembe inavyowakong'ori watu halafu ndio uongelee hizo 'gharama za lazima' wewe na Magu mnazotaka kutuongezea!
Inatia hasira mno ndugu! Itabidi na mimi nitafute ganzi watu wanazodunga bongo zao zinakataa kuona mambo ya wazi kama haya. Haiwezekani kiongozi wa nchi kuchukua maamuzi ya kibabe wakati anajua 100% yeye na wenzake wa ndiooooooo ndio wametufikisha hapa. Pamoja na ubabe anaanza kuwaita wezi. Kwani nani aliwapa hayo madini na vingine vyote walivyopewa?

Sioni sababu ya kuzuia makontena kabla ya kuwaita hao wawekezaji mezani na kuzungumza nao. Mtendaji mkuu wa ACACIA Brad Gordon ameshakiri na kusema mikataba haina usawa, na 2016 wakaanza kulipa corporate tax. Kwanini jambo kama hili lisichukuliwe kama utayari wa kutaka kurekebisha makosa ya watawala?
 
Mi nashangaa sana,kuna watu ukiwaona na kuwasikiliza au kusoma maandiko yao utagundua wanaombea sana serikali ishindwe na hili sakata la mchanga.ni upinzani gani wa kutokubali hata jambo lenye tija kwa taifa? Kwa hili Magufuli aungwe mkono hata kama tutalipishwa hayo mnayodai tutalipishwa.kwa hiyo ni bora kuendelea kuibiwa au kusitisha? Najiuliza huu ni uzalendo wa aina gani? Mtu kachukua hatua bado anabezwa.angekuwa kimya pia tungesema na.kumbeza sana.watanzania hawana jema
Hawa watu ndugu yangu ni kama viatu. ..wanaona vibaya sasa serikali inachukua hatua. Ni kama fisi wanasubiri mkono udondoke wauchukue. Ni watu hatari sana kwa usalama na afya ya nchi hii
 
Mr MM katika hili bandiko lako umedhihirisha namna gani ulivyo mnafiki..

Unafiki wako unakuja pale unapotaka hatua zichululiwe juu ya ACACIA huku ukijua kabisa hawa jamaa hawakujikatia wenyewe eneo la kuchimba madini, hawakuamua tu kusafirisha huo mchanga wakiwa wenyewe chumbani, pia hawakujipangia kodi ya kulipa.. Kila hatua waliopitia katika hiyo biashara yao kuna mikataba tulisign nao, na lazima ujue hao ni wafanyabiashara wamekuja hapa kutafuta faida.

Kwenye bandiko lako loote hukuzungumzia chanzo cha tatizo ambacho ni mikataba ya kipumbavu iliyosigniwa na wapumbavu wetu na wengine weeengi bungeni wakasema ndiyooooo.
Adhabu gani tunampa MKAPA&Co ??? ambaye ndie chanzo cha hili, adhabu gani tunawapa CCM?? wanaotutia hasara kila uchwao??
 
Binafsi sidhani kuna yeyote anayeweza kusema kwa nia chanya kwamba katika hili la kontena 277 ‘tusifanye lolote'. Huku kufilisika kifikra kuliko kithiri.

Watanzania tunaweza kuwa na raisi mkurupukaji kweli kweli na kwa maoni yangu binafsi hivyo ndivyo alivyo; lakini wazungu wana nusemi unaosema " sometimes it has to get worse before it becomes better".

Kupitia kwa maamuzi haya ya kukurupuka kuna faida maana walipa kodi wataumia kwa kulipia gharama za kukurupuka lakini wawakilishi wao wakirudi bungeni hawatapitisha sheria kandamizi kwa hati ya dharura kama ilivyokuwa sheria ya madini ya 1998.

Kwa kifupi maumivu ambayo walipa kodi watayapata (kama matokeo ya kushindwa kesi) yatafanya kizazi kijacho kiwe makini zaidi na hawa majambazi.

Mkuu CCM sio wakuwaamini kabisa, wametutia hasara nyingi sana uzembe wao na kutuletea mateso lakini bado wanaendeleza uzembe tu, kumbuka mikataba ya gas ambayo tulipaza sauti na kuonya tusirudie makosa kama tuliyofanya kwenye madini lakini wapi wakarudia yaleyale tena kwa ubabe..
 
mh.lissu hajakataa kama jamaa hawatudhulumu, hajakataa kwa sababu rais ni wa CCM bali alichosema ni ushauri kuwa iko namna nzuri ya kuliendea jambo hili ila sio kama rais afanyavyo kataja mpaka MIGA sijui ndo nini hii,lakini naye ameonesha hisia juu ya hili , waligoma kuteuliwa kwa muhongo magu akajua ni siasa lakini leo hii yeye mwenyewe AMEMTUMBUA!Tujifunze kuelewa mapema kabla ya kushindwa!!
 
Halafu wakifanya hivyo utaridhika; mikataba ikiendele akubakia ilivyo au unataka wakishafanya hivyo wafanye kitu kwenye hilo la mikataba?
Wakishatuomba radhi watupishe kuongoza nchi imeshawashinda hii mkuu MMM.
 
Halafu akijiuzulu nini kitokee kwenye hiyo mikataba; maana akijiuzulu Bi. Samia Suluhu Hassan atakuwa RAis; yeye afanye nini?
Kwani Mkulu atafanya nini, kwa kukurupuka kwa aina hii. Untegemea mwisho mwema kweli, inatakiwa hekima na busara na sio bla bla na mbwembwe nyingi.
 
Ndugu yangu MM nakushukuru sana kuonyesha mfano halisi wa kumsapoti Raid wetu,Mimi nasema acha nchi ianguke wote tukae chini nampenda sana Magufuli!
Wakati anasema ndiyoooooo alikuwa hajui kama na yeye ni mmoja kati ya watu walioingiza nchi katika janga Leo kastuka nini au umaarufu wakisiasa wapinzani waliposema hii mikataba ni mibovu walitupwa selo mbona yeye alikaa kimya hakusema chochote au alikuwa anachumia tumbo kwanza? Sasa tumbo limejaa anaamua kusema wakati tushaibiwa kwa kiwango kikubwa na tushatia sahihi paka miaka mia ipite naniwakutengua Leo mikataba tuliotia saini mwenyewe na kuiandaa mwenyewe wanasiasa wanafki sana utathani kashuka tokambinguni kumbe na yeye alikuwa ni mmoja kati ya wale waliosema ndiyoooo
 
Mkuu CCM sio wakuwaamini kabisa, wametutia hasara nyingi sana uzembe wao na kutuletea mateso lakini bado wanaendeleza uzembe tu, kumbuka mikataba ya gas ambayo tulipaza sauti na kuonya tusirudie makosa kama tuliyofanya kwenye madini lakini wapi wakarudia yaleyale tena kwa ubabe..
Ni kweli Samurai! Sasa tufanyeje? Kupigwa tumepigwa tena kwa uzemve wetu. Kuumia tutaumia na naamini CCM itabomoka.muda si mrefu na hivyo kizazi kijacho hakitakubali kuumizwa kwa kuibiwa tena. Usijali, mwisho wa ccm uko karibu!
 
Nikweli kusiyishwa kwa Mikataba ya kibiashara inayolipa Taifa letu hasara na kuwanufaisha wawekezeji na waliyo saini hiyo mikataba inayolighalimu Taifa letu hasara ,Rais tumuunge mkono kwa maslahi ya Taifa pindi akiamua kuvunja Mikataba hiyo kama ni Mahakamani ok wataenda na Kweli tutashindwa kwenye kesi za aina hiyo ila Nitoe ushauri walioingia mikataba hii mibovu wachukuliwe kuwa waliihujumu Nchi yetu hivyo Bunge litunge sheria ambayo kwa namna fulani tutawaadhibu kwa sheria hiyo waliolipa hasara Taifa kwani ijkithibitika mkataba fulani wa Uwekezaji ni mbovu tambua aliesaini mkataba huo alikula mlungula yaani Rushwa kubwa ,alitanguliza Ubinafsi wake na si Mzalendo yeye ndie afirisiwe mali zake zifidie hasara na fharama za mdai yaani mwekezaji
 
Unataka Magufuli achukue hatua gani kwenye suala la mikataba mibovu?
Aiweke wazi hiyo mikataba.

Aache kusaini mikataba kwa siri bila kujadiliwa kwa mapana bungeni na wadau muhimu.

Apige stop michakato ya leseni za madini na gesi hadi hapo tutakapobadili sheria zilazimishe uwazi kwa LAZIMA.

Kwenye kila mkataba kipengele cha kuvunja mkataba kiipe nguvu serikali.

Madini yote yasiuzwe nje kuoitia third party countries. Badala ya kuuza kupitia LME tuuze kupitia Dar Mineral Exchange. Kama hawataki yaachwe yalipo.

Mwisho kabisa tuache kugawa madini na kusubiri kupewa mrahaba. Tuingie mikataba ya kuwpa kandarasi wachimbaji tu.
 
Waambie pia basi lowassa na sumaye nao wajiuzulu kamati kuu ya chadema wanakichafua chama kinachopinga uchafu
Tujadili hoja, hao tayari wako upinzani wakikutwa na hatia watashughulikiwa. So kuwajadili ni kupoteza mwelekeo, hapa wa kudeal nao ni hao waliopo madarakani yaani Chama tawala na serikali yake. Na ninakuhakikishia hawatowafanya kitu kwani itabidi uwaguse na wasiogusika na hawa wengine hawatokubali kufa peke yao. Kazi kweli kweli
 
Unajua mnisamehe kidogo; kuna hisia mbaya sana ya uduni (acute sense of inferiority complex). Kwanza, tunaamini tutashindwa kama kes itatokea kati ya serikali na Acacia. Tutashindwa kwa sababu hatuwezi kushinda! Lakini kuna kitu kingine pia kinajionesha. Chukulia kwa mfano hoja ya "mikataba"; sote tunajua jinsi gani suala la mikataba mibovu limeisumbua nchi yetu na jinsi ambavyo ukweli kabisa upinzani ulifanya kazi kubwa sana kuonesha. Sasa unajiuliza; kama kuzuia makontena 277 tu tunaambiwa tutalizwa na tutalipishwa vibaya itakuwaje kama tukigusa mikataba?

Ndugu zetu katika woga wao wanasema "tusifanye lolote kwa sababu itatugharimu"; Wanasahau kuwa wakati mwingine mtu inabidi uchukue maamuzi ya kutetea maslahi yako hata kama itakuja gharama kubwa. Kuna watu wanaamua kuachana katika ndoa wakijua kabisa kuwa kwa kufanya hivyo (ni mkataba huo) watatakiwa kulipa gharama kubwa sana kwa yule mwingine. Lakini watafanyaje sasa? Abakie kwenye uhusiano ambao unahatarisha afya yake ya akili na mwili au atoke ili atafute ahueni kwingine hata kama kwa kufanya hivyo atatakiwa kulipa gharama ya matunzo kwa yule mwingine au atalazimika kugawana mali walizochuma pamoja? Kwa wengine, huo siyo uamuzi mgumu kivile.

Katika mahusiano ya biashara ya kimataifa hili pia si jambo geni; nchi, makampuni na hata watu binafsi wanaweza wakafika mahali wakaona kuwa hali iliyopo (status quo) haiwezi kuendelea na watatafuta namna ya kutatua tofauti zao lakini kama ikibidi wataenda mahakamani kutafuta judicial intervention (mahakama iingilie kati). Wanapofanya hivyo ina maana wanakuwa tayari kwa matokeo yoyote lakini hofu ya gharama peke yake haiwezi kuwa sababu ya kutokuchukua maamuzi yenye maslahi kwa upande husika.

NImewasoma ndugu zangu wengi wakitolea mfano wa mambo mbalimbali ambayo yamewahi kufanywa chini ya Magufuli na kuwa yamekuja kuligharimu taifa. Lakini kama ni gharama ya lazima kwanini tusilipe? Ni kweli kuna haja ya kuwa waangalifu; lakini uangalifu usije kugeuka kuwa woga! Jambo jingine la kuzingatia hapa ni kuwa katika sakata hili la makontena ya michanga mwenye maslahi makubwa ni taifa na siyo kampuni; hivyo kama taifa ni lazima tuangalie maslahi yetu lakini kama maslahi yetu yanatishiwa sana ni jukumu letu kuyatetea kwa umakini, weledi na uangalifu. Lakini kamwe tusisite kuyaangalia maslahi yetu kwa sababu tunaogopa wakubwa wanaweza kutushtaki au wanaweza kuamua kuondoa uwekezaji wao.

Mikataba hii ambayo tunasema "tuipitie" na tumeshadai kuwa ipelekwe Bungeni; lengo litakuwa ni nini? Je, tukiipitia au tukiipeleka Bungeni tutataka tuifumue tu tuifute au tuijadili upya? Vipi kama hao "wakubwa" wakigoma kupitiwa tena mikataba yao na wakikataa tusiiguse kwa sababu ni mikataba halali? Je, kama tukifanya hivyo kwa maamuzi yetu wenyewe (unilaterally) siyo kwamba watatupeleka kwenye arbitration ambako tutaweza kupoteza kama tulivyofanya kwenye Dowans? na kesi nyingine?

Wanaosema "tupitie mikataba" - jambo ambalo wengi tunalikubali na tumelipigia kelele miaka nenda rudi - hawajui kuwa wakubwa hawa kama kuna kitu watatubana nacho sana na hawako tayari kukiona ni kupitiwa mikataba hii. Sasa, Magufuli akiamua kusitisha mikataba na kuipitia yote (na ninatabiri hili itakapokuja ile kamati nyingine na matokeo yake) je, tutamuunga mkono au tutahamisha magoli tena na kusema "kwanini anaingilia mikataba halali!? hajui watatunyoa na mchanga!"?

Kwa sababu baada ya ile Kamati Magufuli anaweza kuleta usitiswhaji wa muda (Moratorioum) ya hata miezi sita ili kulipa taifa na wataalamu wake kupitia mikataba hiyo. Je, tutakubali na kuunga mkono au tutakimbia tena na kusema "mamaaa wee kagusa mikataba sasa, nchi itakimbiwa"?

Matokeo yake ni kana kwamba tunaambiwe kile alichoambiwa yule mwizi kwenye simulizi fulani 'ukisimama nchale, ukikimbia nchale, ukizungumza nchale, ukiguna nchale, usimeze, usiteme, wale usimumunye"! Ndio maana unaona kuwa Magufuli amefanya kile ambacho Wasambaa wanasema kama ni 'mbwai na iwe mbwai'!

Nawatakieni Mfungo Mwema wa Mwezi wa Ramadan.
Ni pesa ya 2020 CCM wanaisaka na kulipa madeni ya 2015 na Acacia ndiyo kichochoro kama ilivyokuwa IPTL mwaka 2015
 
Back
Top Bottom