Magufuli "Nchale!" - Usiteme, Usimeze wala Usimumunye!

Magufuli "Nchale!" - Usiteme, Usimeze wala Usimumunye!

Kwanza. Akiri hadharani kwamba CCM ndio imetufikisha hapa
Pili.akubali kwamba yeye na masisiemu wenzake walikuwa miongoni mwaka waliotusababishia hasara hii. Watuombe msamaha watanzania na wawajibike kisiasa.
MADINI NI YA CCM?
 
Unajua mnisamehe kidogo; kuna hisia mbaya sana ya uduni (acute sense of inferiority complex). Kwanza, tunaamini tutashindwa kama kes itatokea kati ya serikali na Acacia. Tutashindwa kwa sababu hatuwezi kushinda! Lakini kuna kitu kingine pia kinajionesha. Chukulia kwa mfano hoja ya "mikataba"; sote tunajua jinsi gani suala la mikataba mibovu limeisumbua nchi yetu na jinsi ambavyo ukweli kabisa upinzani ulifanya kazi kubwa sana kuonesha. Sasa unajiuliza; kama kuzuia makontena 277 tu tunaambiwa tutalizwa na tutalipishwa vibaya itakuwaje kama tukigusa mikataba?

Ndugu zetu katika woga wao wanasema "tusifanye lolote kwa sababu itatugharimu"; Wanasahau kuwa wakati mwingine mtu inabidi uchukue maamuzi ya kutetea maslahi yako hata kama itakuja gharama kubwa. Kuna watu wanaamua kuachana katika ndoa wakijua kabisa kuwa kwa kufanya hivyo (ni mkataba huo) watatakiwa kulipa gharama kubwa sana kwa yule mwingine. Lakini watafanyaje sasa? Abakie kwenye uhusiano ambao unahatarisha afya yake ya akili na mwili au atoke ili atafute ahueni kwingine hata kama kwa kufanya hivyo atatakiwa kulipa gharama ya matunzo kwa yule mwingine au atalazimika kugawana mali walizochuma pamoja? Kwa wengine, huo siyo uamuzi mgumu kivile.

Katika mahusiano ya biashara ya kimataifa hili pia si jambo geni; nchi, makampuni na hata watu binafsi wanaweza wakafika mahali wakaona kuwa hali iliyopo (status quo) haiwezi kuendelea na watatafuta namna ya kutatua tofauti zao lakini kama ikibidi wataenda mahakamani kutafuta judicial intervention (mahakama iingilie kati). Wanapofanya hivyo ina maana wanakuwa tayari kwa matokeo yoyote lakini hofu ya gharama peke yake haiwezi kuwa sababu ya kutokuchukua maamuzi yenye maslahi kwa upande husika.

NImewasoma ndugu zangu wengi wakitolea mfano wa mambo mbalimbali ambayo yamewahi kufanywa chini ya Magufuli na kuwa yamekuja kuligharimu taifa. Lakini kama ni gharama ya lazima kwanini tusilipe? Ni kweli kuna haja ya kuwa waangalifu; lakini uangalifu usije kugeuka kuwa woga! Jambo jingine la kuzingatia hapa ni kuwa katika sakata hili la makontena ya michanga mwenye maslahi makubwa ni taifa na siyo kampuni; hivyo kama taifa ni lazima tuangalie maslahi yetu lakini kama maslahi yetu yanatishiwa sana ni jukumu letu kuyatetea kwa umakini, weledi na uangalifu. Lakini kamwe tusisite kuyaangalia maslahi yetu kwa sababu tunaogopa wakubwa wanaweza kutushtaki au wanaweza kuamua kuondoa uwekezaji wao.

Mikataba hii ambayo tunasema "tuipitie" na tumeshadai kuwa ipelekwe Bungeni; lengo litakuwa ni nini? Je, tukiipitia au tukiipeleka Bungeni tutataka tuifumue tu tuifute au tuijadili upya? Vipi kama hao "wakubwa" wakigoma kupitiwa tena mikataba yao na wakikataa tusiiguse kwa sababu ni mikataba halali? Je, kama tukifanya hivyo kwa maamuzi yetu wenyewe (unilaterally) siyo kwamba watatupeleka kwenye arbitration ambako tutaweza kupoteza kama tulivyofanya kwenye Dowans? na kesi nyingine?

Wanaosema "tupitie mikataba" - jambo ambalo wengi tunalikubali na tumelipigia kelele miaka nenda rudi - hawajui kuwa wakubwa hawa kama kuna kitu watatubana nacho sana na hawako tayari kukiona ni kupitiwa mikataba hii. Sasa, Magufuli akiamua kusitisha mikataba na kuipitia yote (na ninatabiri hili itakapokuja ile kamati nyingine na matokeo yake) je, tutamuunga mkono au tutahamisha magoli tena na kusema "kwanini anaingilia mikataba halali!? hajui watatunyoa na mchanga!"?

Kwa sababu baada ya ile Kamati Magufuli anaweza kuleta usitiswhaji wa muda (Moratorioum) ya hata miezi sita ili kulipa taifa na wataalamu wake kupitia mikataba hiyo. Je, tutakubali na kuunga mkono au tutakimbia tena na kusema "mamaaa wee kagusa mikataba sasa, nchi itakimbiwa"?

Matokeo yake ni kana kwamba tunaambiwe kile alichoambiwa yule mwizi kwenye simulizi fulani 'ukisimama nchale, ukikimbia nchale, ukizungumza nchale, ukiguna nchale, usimeze, usiteme, wale usimumunye"! Ndio maana unaona kuwa Magufuli amefanya kile ambacho Wasambaa wanasema kama ni 'mbwai na iwe mbwai'!

Nawatakieni Mfungo Mwema wa Mwezi wa Ramadan.


Hili swala ni rahisi sana kulielewa kwa wale walio upande wa Muzungu hasa chadema, ni kwamba walitaka wao ndiyo walifanye sasa kwa kuwa limefanywa na Raisi wetu Magufuli ndiyo maana wanapinga ni kama vile Raisi Magufuli amechukuwa share yao, kwa maana nyingine hakuna jinsi ambavyo Serikali ingedili na hili halafu chadema wasipinge, kama Serikali ingefanya chadema wanavyopendekeza wangekuja kivingine na kusema wako upande wa Wananchi, kama Raisi Magufuli angeipotozea Ripoti ya Tume pia wangepinga na sasa hivi pangekuwa hapatoshi kwamba Raisi anawalinda wahusika, amechukuwa hatua wanasema ripoti ni ya Uongo na ya Muzungu kwa maoni yao ndiyo ya kweli, mwisho wa siku Tanzania hakuna Upinzani bali kuna wachumia tumbo tu!
 
Unataka Magufuli achukue hatua gani kwenye suala la mikataba mibovu?
Kwanza akiri hadharani kuhusika na jambo hilo na aombe radhi hadharani ,halafu Avunje mikataba ya wawekezaji kwa kufuata utaratibu wa kisheria , ule utaratibu wa kimataifa ambao Tanzania imesaini kuufuata , then aanze kuchimba mwenyewe madini ya nchini na kuchakata kila kitu kama wafanyavyo wawekezaji
 
Kujua unafiki wa Magufuli tumshinikize aweke mikataba yote ya nchi ya awamu ya tatu, nne na sasa hadharani ikiwemo ile ya ununuzi wa ndege. Watanzania tuichambue kwa kina tukishirikiana na Wabunge.

Kwa unafiki wake hili hawezi kulikubali.
We nyumbu kweli, ikishawekwa nini kifanyike?
 
Kujiuzulu ni kukubali kwamba ulihusika kwa namna moja au nyingine katika maamuzi ambayo yameliingiza Taifa kwenye hasara kubwa sana, Mwinyi alijiuzulu. Samia aweke hadharani mikataba yote ya nchi tuichambue kwa kina kama Watanzania ili kuangalia namna ya kuepuka mikenge mingine miaka ijayo.

Halafu akijiuzulu nini kitokee kwenye hiyo mikataba; maana akijiuzulu Bi. Samia Suluhu Hassan atakuwa RAis; yeye afanye nini?
 
Kwanza akiri hadharani kuhusika na jambo hilo na aombe radhi hadharani ,halafu Avunje mikataba ya wawekezaji kwa kufuata utaratibu wa kisheria , ule utaratibu wa kimataifa ambao Tanzania imesaini kuufuata , then aanze kuchimba mwenyewe madini ya nchini na kuchakata kila kitu kama wafanyavyo wawekezaji
Ni utaratibu huo wa kisheria? Lowassa na Sumaye si walikuwa mawaziri wakuu? Walishakiri wao kuhusika na hii mikataba mibovu na kuomba radhi?
 
Tulidhani lisu kwa utaalamu wa sheria alionao ataonesha kuisaidia na kuishauri nchi Tanzania kumbe keshaonesha woga na kuanza kuwatetea mabwana wazungu.
Lisu ni mwanasheria lakini naamini sheria za mikata hajui chochote kile, na ndo maana Mh.Raisi kachagua wanasheria nguli kufuatilia hiyo mikataba na kutoa majibu yenye faida kwa nchi.
 
Mi nashangaa sana,kuna watu ukiwaona na kuwasikiliza au kusoma maandiko yao utagundua wanaombea sana serikali ishindwe na hili sakata la mchanga.ni upinzani gani wa kutokubali hata jambo lenye tija kwa taifa? Kwa hili Magufuli aungwe mkono hata kama tutalipishwa hayo mnayodai tutalipishwa.kwa hiyo ni bora kuendelea kuibiwa au kusitisha? Najiuliza huu ni uzalendo wa aina gani? Mtu kachukua hatua bado anabezwa.angekuwa kimya pia tungesema na.kumbeza sana.watanzania hawana jema
 
Yaani Mwanakijiji unataka tukubali hivi hivi kubeba mzigo wa Uzembe wa watu ambao wako hai?, tena wengine wana mali lukuki?
Tukubaliane, kama JPM anataka tuvunje mikataba kitendo ambacho kitatufanya sisi kama taifa kulipa, Basi Mali za wote waliotufikisha hapa ni lazima zitaifishwe, ziuzwe na ziwe sehemu ya pesa ya kulipia deni.

Pili ni lazima hawa waliotufikisha hapa washitakiwe, na wale wenye kinga ya kutoshitakiwa ni lazima utaratibu wa kuwavua Kinga ufuatwe ili sheria ichukue mkondo dhidi yao, tumeumizwa sana na hii mikataba ya kimangungo!
 
kuna njia ambazo serikali ilitakiwa kuchukua mapema kama ambavyo lissu alikua ameshauri
pamoja na kuwepo mpango wa kupitia upya mikataba pia kulikua na option inayoweza kuzuia uwepo wa hasara inayoweza kujitokeza. kutokana na masharti ya mkataba kama anaevinja mkataba anapaswa kulipa fidia kwaio lazima kama nchi iangalie ni kwa namna gani mikataba inaweza kuvunjwa bila kuingiza taifa hasara na huu ndio uzalendo wenyewe
pia kuangalia namna ya kupata maslahi ya nchi bila kuingia mgogoro na mataifa mengine duniani, hapa ndipo tunapohoji uhalali wa mchanga wa madini kama ni haki yetu ama tuliwapa tena kwa sheria tulizotunga wenyewe sasa badala ya kuanza kwenye sheria unaanza kwenye kukamata maanayake ni kwamba fifia italipwa hadi wakati ambapo sheria ilikua inafanya kazi kwa sababu hiyo wawekezaji walikua hawajavunja sheria
ikitokea takwimu ni za uongo mzee mwanakijiji utachukua hatua gani ..? ndio mana watu wengi wana hofu juu ya kamati kua imefanya kazi kisiasa na si kitaalamu sasa tunataka kujua ni kwa jinsi gaani kamati ya mchanga imefanya afiti zake in validity ..? ndio maana acasia wanataka tume huru na serikali haitaki tume huru sasa uzalendo uko wapi auoni kwamba raisi anafanya siasa na mali za watu
kwa nini asianze na taratibu za kisheria ndipo aje kwenye kuzuia mbona kazi ingekua raisi sana au kwa vile hoja ilitolewa na lissu ..?
sisi wengine tunaona kama rais anataka ku change business partners from west to east hii ni kutokana na vyanzo vya ndani kwaio haoni impact yyt ya kuji isolate na west sasa anaweza kuvunja uku akawapa wale na kwa makubaliano yale yale

mzee mwanakijiji unahitaji tafakuri zaidi kwenye jambo hili uzalendo ni kufata ushauri mzuri hata kama anaekushauri sio mwanachaa wa ccm
 
Funga migodi yote acacia warudi kwao huu wizi wa mchana kweupe wa makaratasi yalitengenezwa na Change na genge lake hauvumiliki.

Sekta ya madini hainufaishi ktk Taifa la Tanzania zaidi ya matumbo ya viongozi wa wachache kwahiyo Hata tukisitisha uzalishaji wa madini na kutumia wawekezaji wa migodi yote ni sawa.madini hayaozi.

genge la chenge ni mkapa na wenzake kina yona na kina mramba...hawa watu wanyongwe au wapandishwe kizimbani kwa kuhujumu uchumi wa nchi

pamoja na wote waliokuwa kwenye baraza la mawaziri

tukiamua kutenda tutende kweli sio tufanye unafiki wa kubebana hapa
 
Ni utaratibu huo wa kisheria? Lowassa na Sumaye si walikuwa mawaziri wakuu? Walishakiri wao kuhusika na hii mikataba mibovu na kuomba radhi?
Nje ya mada kabisa ! Hakika vijana wa ccm ni duni sana kichwani .
 
Back
Top Bottom