Mikataba ya madini ina mambo mengi ambayo tunaamini tunaibiwa. Hili halina mjadala kabisa ...kinachotusikitisha wengi ni jinsi mnavyobeza hatua za JPM kuchunguza usafirishaji wa mchanga nje....hili la mchanga ni sehemu ya wizi lakini kwa kumkamata mwizi na kidhibiti kama hiki ndio fursa ya kurudi mezani kwenye maeneo mengine ya Mkataba. Tume imekiri kuwa kwenye hili eneo la mchanga kusafirishwa mkataba haupo wazi, lakini pia kupitia uzembe wa taasisi zetu ikiwemo vifaa duni kuweza kubainisha madini yaliyomo kwenye mchanga ni source ya huu WIZI ....hebu tujadili hoja za tume one by one badala ya mijadala ya jumla jumla na kutuondoa hata kwenye issue iliyoletwa na kamati ambayo mwanzo ilipongezwa Tundu Lissu kabla hajabadili gia angani na kuanza kuleta historia ambazo zinawahukumu wenyewe ...
Hili la kwamba Acacia ni wezi, ni dhana tu inayopandikizwa kwa kudhani kila mmoja ni UVCCM kwa weledi , akili na fikra. No!
Kuongelea ya kamati ni kutaka kufunika kombe, wakati hakuna kipya.
Walikuwepo wizi huu ukifanyika leo nini kipya kiasi kudhani kamati imegundua 'sayari nyingine''.
Nothing new, hii ni syndicate, huyu alipiga upande huu yule upande mwingine
Kuna dhana ya kusombwa tu na mkumbo wa kushangilia chochote, yes kwa baadhi, si wote
Hili jambo tukitaka kujua ukweli, waliosaini mikataba wapo waletwe watueleze nini kilisainiwa
Kutuambia kamati imeseam haitoshi, wako wapi waliosaini hiyo mikataba?
Tuunge tela kuunga mkono walionufaika na mikataba wamepunzika pengine South Africa, Seyechelles, au London, New York n.k. wanafaidi matunda ya madini. Hao ndio wanatakiwa kurudi na kuunga mkono kwamba kuibiwa miaka zaidi ya 10 inatosha, sasa Taifa nalo lipate
Ngurumbili wengine tunauliza, tuhoji, tukemee wajue wenye mali wapo na wana akili ingawa ni wajinga wa kuzitumia. Japo wajue wenye mali wanajua
Muhimu ni kujua Acacia ni mfanyabiashara, tulimwalika tukampa kila kitu. Hajatuibia
Waliotuibia ni ndugu zetu waliosaini mikataba, Wabunge CCM na ndiyoo, serikali yao
Hao ndio wa kuuliza imekuwaje tumefika hapa, si Acacia aliyekuja kufanya biashara